Bila kuongea maneno mengi, mtu asilia wa zanzibar ni mwafrika mweusi. Aliishi pale kabla hata ya utumwa. Walikuwa na miji yao na tawala zao kama utawala wa Mwinyi Mkuu ambaye ndiye aliyekutwa mji mkongwe (Stone Town kama ilivyo maarufu leo).
Hawa waarabu wanaopigapiga kelele ni wanyanganyi tu, wemeendesha biashara ya utumwa na kueneza imani ya uislamu ambayo ilienezwa kwa nguvu. Wame wakandamiza waafrika weusi kwa miaka mingi, kwa kuwauza kama watumwa na kuwatumikisha katika mashamba na shughuli zao nyingi kwa kuwalipa ujira mdogo. Faida iliyopatikana ilitumika kujenga majumba ya kifahari yanayoonekana leo hii Mji mkongwe ambayo walikuwa wakiishi wao na wahindi wafanya biashara mpaka mwaka 1964 waafrika walipochoka na kufanya mapinduzi wakiongozwa na Marehemu karume. Sasa wanataka kurudi tena kupitia kwa wajomba zao, na ndugu zao waliobaki huko Pemba sana sana, japo na unguja wapo kidogo.
Maelezo ni marefu sana kwa kweli, lakini nitakwenda moja kwa moja katika point ili nifikishe ujumbe bila kuchosha msomaji.
Kwanza tuanze kwa maana ya neno Zanzibar.
Zanzibar ni muunganiko ma maneno mawili ya kiarabu Zangi + bar (Zangibar) Zangi = mtu mweusi, na bar = pwani. Kwahiyo waarabu walipofika pwani hiyo ya Afrika mashariki waliwakuta watu weusi wana kaa pale, na wakapaita pwani ya watu weusi. Nadhani jibu mmeshalipata.
Waarabu waliwakuta wareno Zanzibar, na makanisa yalikuwepo pia. Ngome kongwe maarufu sana leo hii, ilijengwa na Wareno. Na katika hiyo ngome kongwe kulikuwa na kanisa ambalo lilibomolewa na waarabu.
Kabla sijaondoka kwenye point, nadhani nimesha jibu swali linalouliza mzawa wa Zanzibar ni nani? Kama mtataka niendelee kumwaga historia hii tamu zaidi niambieni.