Myanmar yafunga huduma za usambazaji wa intaneti

Myanmar yafunga huduma za usambazaji wa intaneti

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Jeshi la Myanmar limeamuru hii leo kufungwa kwa huduma za intaneti wakati waandamanaji wanaopinga mapinduzi ya kijeshi wakiendelea kupuuza kitisho cha matumizi ya silaha yaliyotolewa na jeshi hilo.

Kulingana na mmoja wa wasambazaji wa huduma hiyo agizo la kuzimwa kwa mtambo huo lilitolewa na wizara ya usafirishaji na mawasiliano jana Alhamisi lililosema huduma zote ya intaneti zimesitishwa kwa muda hadi taarifa nyingine itakapotolewa.

Kampuni ya simu ya Norway, Telenor ambayo ni miongoni mwa makampuni makubwa kabisa nchini humo imethibitisha haitaweza tena kutoa huduma zake za intaneti. Aidha serikali imevifungia vyombo vyote vya habari isipokuwa vichache vinavyomilikiwa kikamilifu na jeshi.

Baadhi ya vilivyofungiwa na ambavyo vimesimamishwa vimeendelea kuchapisha taarifa kwenye mitandao ama njia nyingine yoyote vinavyoweza kutumia.
 
Back
Top Bottom