Pole ndugu we vumilia tu kama unampenda huyo bimdada japo alifanya jambo hilo bila kufikiria mara mbili.wanawake wengi wanapopenda huwa wanachanganyikiwa na huweza kufanya lolote bila kujiuliza nini yatakuwa madhara endapo penzi litaisha.huwa hawafikirii kuachana zaidi ya kuendeleza penzi na hiyo ndio tofauti kubwa sana kati ya wanawake na wanaume katika mapenzi. nakushauri usimsumbue huyo mpenzi wako kwa hiyo tatoo naamini na yeye anaijutia sana ila hana cha kufanya.ukiendelea kuiongelea atajua kwamba umeshindwa kumpenda na utampunguzia kukuamini na kujiaminikiasi cha kutopata nafasi ya kuendelea kuyaona mazuri yake.japo ni jambo baya lakini piga moyo konde kama mwanaume.yaliyopita si ndwele ganga yajayo.amua kuona kawaida kwani huyo mpenzi aliyechorewa tatoo alikuwa zamani. zaidi kama mpenzi wako aliweza kuchora tatoo ya huyo mwanaume mwingine bila kufiiria mara mbili,amini kwamba mwanamke wako akipenda huwa anapenda hasa hivyo thamini hilo na muoneshe mapenzi ya kweli ili na yeye akupe moyo wake wote.muoneshe kwamba wewe ni tofauti na wanaume wengine na hakika utamfurahia huyo mwanamke.