Tourist man
Member
- Mar 31, 2014
- 34
- 5
Mie nmeitamani Russia mkuu....npe ushauri kama unao?Mi nilijua unaenda kusoma.....Kama ni for leisure umekosa nchi nyingine ya kwenda?
Mie nmeitamani Russia mkuu....npe ushauri kama unao?
Huogopi watakuCrimea?
Lakini mkuu naona umejichanganya Kiev ni ukrain.Pako poa sana me nilikuwa kwenye lile jimbo la Kiev nipoa sana kaka na hasa kwa totozi ila kama ukijitambulisha ur from amerika utaenjoy sana coz wanajua unampunga ila ukisema ur hom place ni tz au east afrika wengiwao hawapajui wanajua sanasana Kenya kaka,jiandae kutengwa kila uendapo kwani hata pesa ukiitoa kwajili yakupata huduma inakaguliwa utadhani nini vile wanaamini sisi wa afrika sijui ni wezi au hatubahadh yakuwa kule ila nipoa tu mwanangu siumesema utakomaa ukifika utupe mrejesho plz.safarinjema mpwa.
Aloo umenifungua macho halafu umenitisha ile mbaya....lakini ntafanyia kazi ushauri wako....thanks man.duh! wewe una hela za kuchezea eti? watu wanalala njaa wewe unataka kwenda Russia kula bata tena miji mitano,duh! for leisure case huwezi kuinjoi Russia,ni bora ungeenda serengeti,hifadhi ya rubondo au kama ni very crucial lazima uende ulaya,at least nenda finland au sweden,japo wazungu wote ni wabaguzi,lakini bora hizo nchi,kwa Russia umepotea mkuu,kwanza moscow ni jiji kubwa sana ambalo lina magenge mengi ya uhalifu,then nje ya jiji hilo kuna mbwa wengi hatari waliozagaa mitaa kibao hufukuza na kuuma watu,wa russia kiuchumi wa mtu mmoja mmoja wapo vibaya sana,na hasa wakijua umeenda kula bata,nao hawawezi hata kutalii nje,you'll be in trouble,kwa uzoefu wako ni wa russia wangapi hutalii kila mwaka? ukilinganisha na wamarekani british japan na canada? think deep.
Thanks alot....hio invitation ntaipata wapi mi mgeni hapo?nategemea kwenda Moscow,st petersburg,volgograd,penza na Kazan.Kwa kutumia treni ili niokoe gharama.Unaenda mji gani??
Karibu Moscow City.
Njoo na hela za kutosha usije ukalala nje kwenye barafu kila kitu kinaenda kwa procedures,kama unaenda kwa kutalii tu piga cost ya hotel na na matumizi ya siku uyakazoishi.Sasa hivi kuna baridi hali ya hewa haitabiriki na kuna barafu za kushtukiza.
Kuhusu visa kwanza hangaikia invitation kama una passport,ukipata invitation uende angaza kupima H.I.V utalipia fomu ya majibu kwa 20,000,nakushauri nenda hospitali ya Mnazi Mmoja,ukipewa hiyo fomu hapo hapo uwaambie wakupe chanjo ya Yellow fever,utalipia kadi 5,000 nadhani,then kabla ya kwenda ubalozi wa Russia nenda Russian Culture ipo karibu na Agha Khan hospital uwape hiyo fomu ya H.I.V test,kama ni express watakutafsiria kwa kirusi kwa sh 30,000 ,wakitafsiri majibu yako yaliyogongewa mhuri na saini unatakiwa uende ubalozi wa Russia,upo karibu na Ubalozi wa Ufaransa,ukitoka posta unaelekea mpaka Salenda bridge,au unaweza kupanda daladala ya posta-mwenge kisha unashukia ubalozi wa ufaransa au karibu na Stanbic Bank.Ukifika hapo ubalozini kwao uwape invitation ukiwa umeambatanisha vipimo vya H.I.V vilivyotafsiriwa kutoka Russian culture,kama utataka Express visa utatoa sh 1,59,000.
Utakuwa umemaliza kila kitu.
Karibu Russia,hakuna ubaguzi ila kama we mbaguzi utahisi unabaguliwa.
Ingekuwa kwa ajili ya masomo ningejua la kufanya,ila kwa ajili ya tour sijawahi,nadhani itabidi utafute kampuni ya tour ya huko Russia,watafute hata kwa njia ya internet,mnaweza kuelewana na wakakutumia invitation,but kutembea kwa treni mbona kazi sana maana si utakuwa na mizigoThanks alot....hio invitation ntaipata wapi mi mgeni hapo?nategemea kwenda Moscow,st petersburg,volgograd,penza na Kazan.Kwa kutumia treni ili niokoe gharama.
Nenda Mkuu, kama mlevi itakuwa poa zaidi si unajua walevi wanavyopendana! halafu usiende na shem huko maana kuna toto za kufa mtu huko (usisahau kuchukua mkuyati )warusi dada zao wazuri bhana!Habari zenu ndugu zangu wa jf.mimi humu ni mgeni ila nmekuja huku kufuata advice yenu.
Naombeni ushauri juu ya nchi hii ya Russian nna mpango wa kwenda for leisure 2 weeks.najua watz huko hawakosekani.Je visa zake hazisumbui kama za uk?Hotels?nategemea kwenda miji mitano.
Naskia kuna ubaguzi mkubwa ila mi ntakomaa tu.
Naombeni ushauri kwa wazoefu.
Nawasilisha
Ungenishauri nitumie njia gani maana naona train ni cheap kuliko Ndege...?Ingekuwa kwa ajili ya masomo ningejua la kufanya,ila kwa ajili ya tour sijawahi,nadhani itabidi utafute kampuni ya tour ya huko Russia,watafute hata kwa njia ya internet,mnaweza kuelewana na wakakutumia invitation,but kutembea kwa treni mbona kazi sana maana si utakuwa na mizigo