Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Katika wiki hii na hasa siku mbili zilizopita nimefuatilia mijadala kuhusu uchaguzi wa Spika wa Bunge kwenye media zetu (TV na Magazeti). Wengi wa waliochangia walikuwa wanaonyesha kwamba Samuel Sitta anafaa ila anawekea mizengwe na mafisadi ndani ya CCM.
Maoni yangu ni kwamba kama vyombo vyetu vya habari vinataka tupate Spika mzuri visiegemee upande mmoja na kuanza kusema upande mwingine vibaya (tabia ambayo ilifanyika na wanamtandao 2005). Vinachotakiwa kufanywa ni kuweka mizani sawa ya uchambuzi katika masuala yaliyofanywa na wagombea wote (mabaya kwa mazuri). Kwa mfano wagombea wawili Chenge na Sitta mimi kwa kuanza ningeweza kuwaweka ifuatavyo. Chenge amekuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa muda mrefu, hivyo ana uzoefu katika masuala ya sheria na upeo ambao unaweza kusaidia kuongoza bunge. Lakini katika kipindi chake cha uanasheria mkuu ndipo serikali iliingia mikataba mingi ya kiufisadi kwa kisingizio ambayo inaitia hasara kubwa nchi yetu. Kwa upande wa Sitta naweza kusema kuwa amekuwa mbunge kwa muda mrefu, ameshawahi kuwa waziri wa sheria, amewahi kuwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji na kwa sasa ni Spika aliyemaliza muda wake. Ukiangalia uzoefu wake anafaa kabisa kuongoza bunge, lakini katika kipindi chake cha kuwa Mkurugenzi wa TIC ndipo wawekezaji wanaoitia hasara nchi waliingia, akiwa Spika alionyesha kutokuwa na msimamo kwa kutumia mamilioni ya pesa katika ugomvi wa Mengi na Malima na mkosaji kutopewa adhabu yeyote, kumsimamisha Zitto Kabwe nk.
Wengine mnaweza kuongezea mengine kwa hawa wawili na wengine wote wanaogombea ili tuweze kusaidia kuwapata viongozi ambao kweli wana uchungu na nchi na siyo wenye kuendeleza bifu zao mjengoni.
Nawakilisha