My last confession CHADEMA imekosa road map

My last confession CHADEMA imekosa road map

attachment.php

78WSY GH2cMAAAAASUVORK5CYII=

chadema.jpg
 

Attachments

  • chadema.jpg
    chadema.jpg
    26.9 KB · Views: 107
Umemtusi na mama y@ko ambaye ni diwani kupitia chama makini 'chadema'!
 
another joker! pilipili iko shamba inakuwashia nn?
 
katika kumbukumbu zangu wakati najiunga na chadema, kwa nguvu za ushawishi na hoja kutoka kwa kaka yangu, mwanasiasa makini na mwenye maono thabiti ya kesho yake na kesho ya watanzania walio wengi, kijana wa kanda ya magharibi mwa nchi hii dr. Zuberi zitto ruyagwa, aliniambia kuwa

"..tunajenga chama hiki ili kiwe chama bora kitakacholeta maendeleo ya kweli kwa watanzania, ndugu zetu wamechoshwa na umasikini uliokithiri na hawana namna nyingine yeyote isipokuwa matumaini yao yapo juu yenu nyie vizazi vyao ili kuwakomboa kutoka katika umasikini wao, na njia pekee ni kwa kushiriki na kupata nguvu ya maamuzi na utawala.."

akaendelea kwa kusema kuwa;

"..chama chetu (chadema) bado ni chama kichanga na hakina sura ya chama cha siasa, bado tu-wanaharakati, tunao wajibu kama vijana ndani ya chama hiki kuleta mabadiliko kwanza ndani ya chama chetu kukifanya kuwa chama bora zaidi kitakacholeta matumaini mapya mioyoni mwa watanzania kisha tupate kuungwa mkono zaidi na tuweze kushinda chaguzi na kufanya maamuzi ya kimamlaka kama chama tawala, lakini hatutofika huko bila kuwa na shabaha, pamoja na mpango kazi wa kutimiza na kutekeleza shabaha yetu hiyo, sisi wana-chadema hatuna budi tukubali hali yetu ya ndani ya chama na hata nje, halafu tufanye bidii kuibadili hali hiyo ilingane na shabaha yetu.."

mazungumzo haya tuliyafanya mwaka 2006, takribani miaka miaka tisa (9) iliyopita, nasikitika nikisema kuwa bado chadema ya leo haina shabaha wala muelekeo wa kutimiza shabaha hiyo, nasema na kwa ushahidi uliyo bayana kuwa chadema ya leo ni more worse kuliko ya miaka tisa iliyopita, wakati huo vijana walikuwa na matumaini at least ya kuleta mageuzi chanya ndani ya chama chenyewe ili kiwe bora na imara kuweza kukitoa ccm madarakani, lakini leo hata hayo matumaini kwa vijana ndani ya chama yamekwishaondoka achilia mbali matumaini ya kuingia magogoni.

Lakini haya ndio matokeo ya kuruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa, ni jambo lisilowezekana kuwa form six failure yaani mtu aliyepata zero form six ajione mwenye maana na atake kudharau mawazo ya wengine wote na afuate mawazo yake pekee, kisha mawazo hayo yalete mafanikio na yazae matunda..haiwezekani.

Hakuna namna kuwa maandamano iwe ndio hoja ya siku zote, iwe ndio mfumo na shabaha ya kupima mafanikio ya chama, yaani siku niliyokuwa nasikiliza mkutano mkuu wa chama ilikuwa ni kama vile mtu anatania, anasema moja ya mafanikio ya chama chao ni kuendesha maandamano, tena maandamano yaliyopoteza maisha ya watanzania, eti hayo ndio mafanikio, kama sio akili ndogo ni nini..?

Wakati mwingine ninapokumbuka dhamira, ari na kujitoa kwa dhati kutoka katika mioyo ya wazalendo wa kweli wa nchi hii katika kujaribu kukijenga chama hicho zilipozimwa na manyang'au na wapiga dili wa mjini waliokimbilia siasa kama njia ya "nitoke vipi" ni jambo linalokera na kutia uchungu.

Baada ya kumbukumbu hiyo fupi ya maisha yangu ndani ya chadema, niseme kuwa nawatakiwa vijana wa bavicha maandamano yatakayowaachia uchungu wasiousahau katika maisha yao.,kwani wajinga ndio waliwao...!!!



i bet you gonna say i am a gay
 
Ningeshauri ungeanza kuufanyia kazi ushauri huu wewe binafsi..,hii posho ya buku 5 za kukesha JF sio dili kabisa na utazeeka ukitumikia watu wasio na fadhila. Jitambue kisha kamata fursa uchangamke, acha kukesha JF doing nonsese...!!!

Hhaahaahaha mtela please please mimi ndio nachangia Chadema! Mimi silipwi bali ndio nawalipa. Si keshi JF ili nilipwe mimi ni interest yangu kuikoa nchi yangu dhidi ya nyie majangili
 
Last edited by a moderator:
Katika kumbukumbu zangu wakati najiunga na Chadema, kwa nguvu za ushawishi na hoja kutoka kwa kaka yangu, mwanasiasa makini na mwenye maono thabiti ya kesho yake na kesho ya watanzania walio wengi, kijana wa kanda ya magharibi mwa nchi hii Dr. Zuberi Zitto Ruyagwa, aliniambia kuwa

"..tunajenga chama hiki ili kiwe chama bora kitakacholeta maendeleo ya kweli kwa watanzania, ndugu zetu wamechoshwa na umasikini uliokithiri na hawana namna nyingine yeyote isipokuwa matumaini yao yapo juu yenu nyie vizazi vyao ili kuwakomboa kutoka katika umasikini wao, na njia pekee ni kwa kushiriki na kupata nguvu ya maamuzi na utawala.."

Akaendelea kwa kusema kuwa;

"..Chama chetu (CHADEMA) bado ni chama kichanga na hakina sura ya chama cha siasa, bado tu-wanaharakati, tunao wajibu kama vijana ndani ya chama hiki kuleta mabadiliko kwanza ndani ya Chama chetu kukifanya kuwa chama bora zaidi kitakacholeta matumaini mapya mioyoni mwa watanzania kisha tupate kuungwa mkono zaidi na tuweze kushinda chaguzi na kufanya maamuzi ya kimamlaka kama chama tawala, lakini hatutofika huko bila kuwa na SHABAHA, pamoja na mpango kazi wa kutimiza na kutekeleza shabaha yetu hiyo, sisi wana-chadema hatuna budi tukubali hali yetu ya ndani ya chama na hata nje, halafu tufanye bidii kuibadili hali hiyo ilingane na shabaha yetu.."

Mazungumzo haya tuliyafanya mwaka 2006, takribani miaka miaka tisa (9) iliyopita, nasikitika nikisema kuwa bado chadema ya leo haina shabaha wala muelekeo wa kutimiza shabaha hiyo, nasema na kwa ushahidi uliyo bayana kuwa chadema ya leo ni more worse kuliko ya miaka tisa iliyopita, wakati huo vijana walikuwa na matumaini at least ya kuleta mageuzi chanya ndani ya Chama chenyewe ili kiwe bora na imara kuweza kukitoa CCM madarakani, lakini leo hata hayo MATUMAINI kwa vijana ndani ya Chama yamekwishaondoka achilia mbali matumaini ya kuingia magogoni.

Lakini haya ndio matokeo ya kuruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa, ni jambo lisilowezekana kuwa form six failure yaani mtu aliyepata ZERO form six ajione mwenye maana na atake kudharau mawazo ya wengine wote na afuate mawazo yake pekee, kisha mawazo hayo yalete mafanikio na yazae matunda..HAIWEZEKANI.

Hakuna namna kuwa MAANDAMANO iwe ndio hoja ya siku zote, iwe ndio mfumo na shabaha ya kupima mafanikio ya Chama, yaani siku niliyokuwa nasikiliza mkutano mkuu wa Chama ilikuwa ni kama vile mtu anatania, anasema moja ya mafanikio ya Chama chao ni kuendesha maandamano, tena maandamano yaliyopoteza maisha ya watanzania, eti hayo ndio mafanikio, kama sio akili ndogo ni nini..?

Wakati mwingine ninapokumbuka dhamira, ari na kujitoa kwa dhati kutoka katika mioyo ya wazalendo wa kweli wa nchi hii katika kujaribu kukijenga chama hicho zilipozimwa na manyang'au na wapiga dili wa mjini waliokimbilia siasa kama njia ya "nitoke vipi" ni jambo linalokera na kutia uchungu.

Baada ya kumbukumbu hiyo fupi ya maisha yangu ndani ya Chadema, niseme kuwa nawatakiwa vijana wa Bavicha maandamano yatakayowaachia uchungu wasiousahau katika maisha yao.,kwani wajinga ndio waliwao...!!!

Nyie wewe na wenzako mmeachika tena kwa taraka tatu,nashangaa mnavyomzungumzia mume ambaye hawawataki ilihali yeye hana mpango na nyinyi anafanya yake tu.Kama mlikuwa mnampenda mume si mngetulia kuliko megawagawa nje weeee hadi mume wenu kagundua kawapa taraka,nawaasa mtulie kwa huyo mume wenu mpya mliyempata.
 
Mmmh! Watu wengine..,

Usirushe jiwe gizani huwezi kujua litampata nani. Naweza kuhisi ulio walenga kuwapa ujumbe lakni yamkini jiwe hilo likawa limewapata pia ambao hukutarajia/ tegemea, wengine ndugu zako.

Umewahi kujiuliza wale wanao ongeza ruzuku ili mkono wako upate kwenda kinywani wna elimu kiasi gani pale mjengoni? Wengine unajua wanaitwa maprof.

Hata hivyo uwezo / kiwango cha elimu kinaweza kiwe au kisiwe kigezo cha kuwa kiongozi bora. Wezako wakiwemo hao unao watetea ni maprof na madokta lakini usomi wao hauendani na deliveries / proactivity zao.

Na kumbuka pia Rasimun ya pili iliweka kigezo muhimu kupata nafasi mbali mbali ikiwemo ubunge. Umepata kujua kilicho jili kwenye BMK wnao saka mabilioni upate kwenda choo? Kigezo cha elimu ili upate madaraka kimepingwa? Unasemaje mpaka hapo au humjielewi?

Upande wa pili si shangai, mnachoaminisha watu sicho mnacho maananisha kutenda, mwatenda kinyume chake!

Kweheri!
 
"......Dr. Zuberi Zitto Ruyagwa......"

Hivi nyie CCM mna shida gani? kila mtu kwenu Dr.? lini kijana kapata hiyo PhD, Kikwete na degree za kupewa nae Dr., degree za kupewa kisheria huwezi kutumia at official capacity, this include signing documents under the prefix Dr.
Afterall ukiona mtu anapenda kutumia prefix Dr. Prof. blalala ujue hana imani na uwezo wake, ndo maana anatanguliza hizo Dr. ..... Prof kudraw attention.

Mkuu itapidi ugonge!! Mimi nimesoma ujerumani maprofessor wangu walikuwa hawataki tuwaite Dr. prof. Hawakutaka kabisa mmoja anasema niite tu Mr. Schiller etc. Hapa nyumnbani bila kuitwa Dr. blaablaa basi .............
 
Chadema ndiyo basi tena haina kitu tena imeshatoka kwenye reli.

Mtanyosha tu maelezo si muda mrefu! Chadema ingekuwa hipo Polisiccm wangekesha kwenye viwanja vya wazi kuzuia maandamano ya chadeama? Kuzuia maandamano haijawahi uzima hamu ya mabadiliko ila ni kuichelewesha tu lakini iko palepale!
 
Back
Top Bottom