My last confession CHADEMA imekosa road map

My last confession CHADEMA imekosa road map

Huna akili ...msaliti wewe...kwa nini msiangaike kujenga vyama vyenu hivyo? si mtuache na chadema yetu!!
 
Na wajinga ndio waliwao..,wajinga wataendelea kudumu katika ujinga wao.

Aiseee ngoja mimi nibaki kuwa mjinga lakini kamwe Ccm haitaingia akilini mwangu. Mimi sio mchumia tumbo Please. Nyie wachumia tumbo ndio mtahangaika sana na Chadema. Hata hivyo nilitaka nikushauri kuwa tafuta shughuli itakayokuingizia kipato ujitegemeee otherwise utauza utu wako ili upate mkate wako wa kila siku. Ni ushauri tu
 
Maskini ya Mungu, tokea ujiunge na CCM hakuna mazuri ya ccm uliyowahi kuyaweka humu, zaidi ni kuandika habari za CHADEMA.......... Tunatambua kuwa bado unaipenda CHADEMA, lakini kaka nikuambie tu kuwa CHADEMA haikupendi wewe!! Fanya mambo yenu yale ya Lumumba

wewe huna umuhimu wa kujua mazuri ya ccm...fahamu majinga majinga ya chadema
 
Ulikuwa na hoja nzuri sana ila umefika sehemu umeona kana kwamba MBOWE ni mtu ambaye amefeli masomo yake umefanya ushabiki ambao siyo wa msingi. Sasa wewe kama msomi katika nchi una impact gani kwa ustawi wa jamii? na kama MBOWE ni zero mbona akijukuna kichwani police wanaandamana nchi nzima kumdhibiti huo ni wenda wazimu. Tunataka kuona wewe kama kijana na msomi na hao ambao unawataja akina Zitto na Kitila mnana chakufanya kupiti usomi wenu huo kuleta madiliko ya kimfumo nchini mwetu ili kuondokana na umaskini wa mwili na akiri kupitia elimu yenu, kinyume chake mmekuwa sehemu ya kuleta dhuluma na kurudisha mapambano ya mageuzi nyuma huna cha kutuambia uma wewe acha CHADEMA ishindwe iwe furaha kwako na vibaraka wenzako jionee haibu na uruma kama kijana na mwenye jukumu la kukuza uwazi, uajibikaji na uzalendo. Sasa uko ulipo ni mpiganaji au na wewe ni mwizi na mdhurumaji wa mali za uma jitambu wewe ni nani katika Taifa hili.

Hata tukitumia username na avatar ambazo ni fake bado haibadilishi uhalisia wa kilicho mioyoni mwetu..nauona moyo wako ukiwa unasikitika na kuumizwa na kuporomoka kwa Chama ila kwa vile ni kibarua ambacho umekabidhiwa kuhakikisha unamsemea bwana mkubwa nawe umekuja hapa kukisema usichokiamini kwa ID fake.

Amka kijana.,siku za mwisho za utawala wa kilofa zimeisha.,huu ni wakati mpya wenye falsafa mpya. Vijana lazima tuamke na tulipiganie hili taifa kila mmoja pale alipo na kwa uwezo, busara na hekima zake. Acha kutumika kwa vipande vichache vya thamani.
 
Sikusoma mleta post ninani?
kumbe??

nimeishia njiani nimekimbilia kucomment nilichokicomment.
 
Wewe gamba unawezaje kumwambia Mbowe kuwa CHADEMA kwake ni njia ya kutokea kimaisha? Kabla CHADEMA haijawa tayari Mbowe alikuwa na pesa ya kulisha familia kama si ukoo mzima wa akina Mwampamba. Hebu jaribu kutumia akili kidogo tu ulinganishe maisha ya familia yenu na maisha ya Mbowe uone hiyo tofauti.
 
Aiseee ngoja mimi nibaki kuwa mjinga lakini kamwe Ccm haitaingia akilini mwangu. Mimi sio mchumia tumbo Please. Nyie wachumia tumbo ndio mtahangaika sana na Chadema. Hata hivyo nilitaka nikushauri kuwa tafuta shughuli itakayokuingizia kipato ujitegemeee otherwise utauza utu wako ili upate mkate wako wa kila siku. Ni ushauri tu
Ningeshauri ungeanza kuufanyia kazi ushauri huu wewe binafsi..,hii posho ya buku 5 za kukesha JF sio dili kabisa na utazeeka ukitumikia watu wasio na fadhila. Jitambue kisha kamata fursa uchangamke, acha kukesha JF doing nonsese...!!!
 
Naamini umeshatukanwa vya kutosha huko juu ewe mwampamba. Nachofanya mi ni kukupiga singe ya paji ukafilie mbali
 
Wewe gamba unawezaje kumwambia Mbowe kuwa CHADEMA kwake ni njia ya kutokea kimaisha? Kabla CHADEMA haijawa tayari Mbowe alikuwa na pesa ya kulisha familia kama si ukoo mzima wa akina Mwampamba. Hebu jaribu kutumia akili kidogo tu ulinganishe maisha ya familia yenu na maisha ya Mbowe uone hiyo tofauti.
Familia yangu haiwezi kulishwa na fedha haramu za Danguro, kuwa na heshima.
 
nimekutana na wanachadema kadhaa hapa udsm wanaponda sana hizi siasa za kiuanaharakati zisizo na ushawishi
Kimsingi mimi nawafahamu wanachadema wengi sana, kwani nilikuwa miongoni mwao, na wote ninaowajua wanashaka na hawafurahishwi namna ya chama hicho kinavyoendeshwa hivi sasa. Wananung'unika na wanasema pembeni kwa sababu hawana fursa na wanaogopa kuyasema haya kwenye vikao husika na hata kwenye halaiki ya wanachadema. Kimegeuka chama kinachonyima na kuminya demokrasia kwa wafuasi wake kuliko chama chochote kuwahi kutokea duniani.

Ni chama cha hovyo ambacho wanachuo wamekistukia, wataalamu wanaki-dis na hata walalahoi wenzangu mtaani wamestuka kuwa kuna wapiga dili wachache wanaokitumia chama kutengeneza maisha yao huku mamilioni ya watu wanachama wakifa njaa na wengine wakifa kwenye maandamano.
 
Katika kumbukumbu zangu wakati najiunga na Chadema, kwa nguvu za ushawishi na hoja kutoka kwa kaka yangu, mwanasiasa makini na mwenye maono thabiti ya kesho yake na kesho ya watanzania walio wengi, kijana wa kanda ya magharibi mwa nchi hii Dr. Zuberi Zitto Ruyagwa, aliniambia kuwa

"..tunajenga chama hiki ili kiwe chama bora kitakacholeta maendeleo ya kweli kwa watanzania, ndugu zetu wamechoshwa na umasikini uliokithiri na hawana namna nyingine yeyote isipokuwa matumaini yao yapo juu yenu nyie vizazi vyao ili kuwakomboa kutoka katika umasikini wao, na njia pekee ni kwa kushiriki na kupata nguvu ya maamuzi na utawala.."

Akaendelea kwa kusema kuwa;

"..Chama chetu (CHADEMA) bado ni chama kichanga na hakina sura ya chama cha siasa, bado tu-wanaharakati, tunao wajibu kama vijana ndani ya chama hiki kuleta mabadiliko kwanza ndani ya Chama chetu kukifanya kuwa chama bora zaidi kitakacholeta matumaini mapya mioyoni mwa watanzania kisha tupate kuungwa mkono zaidi na tuweze kushinda chaguzi na kufanya maamuzi ya kimamlaka kama chama tawala, lakini hatutofika huko bila kuwa na SHABAHA, pamoja na mpango kazi wa kutimiza na kutekeleza shabaha yetu hiyo, sisi wana-chadema hatuna budi tukubali hali yetu ya ndani ya chama na hata nje, halafu tufanye bidii kuibadili hali hiyo ilingane na shabaha yetu.."

Mazungumzo haya tuliyafanya mwaka 2006, takribani miaka miaka tisa (9) iliyopita, nasikitika nikisema kuwa bado chadema ya leo haina shabaha wala muelekeo wa kutimiza shabaha hiyo, nasema na kwa ushahidi uliyo bayana kuwa chadema ya leo ni more worse kuliko ya miaka tisa iliyopita, wakati huo vijana walikuwa na matumaini at least ya kuleta mageuzi chanya ndani ya Chama chenyewe ili kiwe bora na imara kuweza kukitoa CCM madarakani, lakini leo hata hayo MATUMAINI kwa vijana ndani ya Chama yamekwishaondoka achilia mbali matumaini ya kuingia magogoni.

Lakini haya ndio matokeo ya kuruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa, ni jambo lisilowezekana kuwa form six failure yaani mtu aliyepata ZERO form six ajione mwenye maana na atake kudharau mawazo ya wengine wote na afuate mawazo yake pekee, kisha mawazo hayo yalete mafanikio na yazae matunda..HAIWEZEKANI.

Hakuna namna kuwa MAANDAMANO iwe ndio hoja ya siku zote, iwe ndio mfumo na shabaha ya kupima mafanikio ya Chama, yaani siku niliyokuwa nasikiliza mkutano mkuu wa Chama ilikuwa ni kama vile mtu anatania, anasema moja ya mafanikio ya Chama chao ni kuendesha maandamano, tena maandamano yaliyopoteza maisha ya watanzania, eti hayo ndio mafanikio, kama sio akili ndogo ni nini..?

Wakati mwingine ninapokumbuka dhamira, ari na kujitoa kwa dhati kutoka katika mioyo ya wazalendo wa kweli wa nchi hii katika kujaribu kukijenga chama hicho zilipozimwa na manyang'au na wapiga dili wa mjini waliokimbilia siasa kama njia ya "nitoke vipi" ni jambo linalokera na kutia uchungu.

Baada ya kumbukumbu hiyo fupi ya maisha yangu ndani ya Chadema, niseme kuwa nawatakiwa vijana wa Bavicha maandamano yatakayowaachia uchungu wasiousahau katika maisha yao.,kwani wajinga ndio waliwao...!!!
Hata yule professor Muongo badala ya kuangalia hoja aliangalia performance ya muuliza swali eg. Ole sendeka etc. Wewe pamoja na wenye mawazo mgando kama wewe na wasaliti wenzio wanafikiri degree ndiyo inayoendesha nchi. Muulize huyo mwenyekiti wa chama ulikohamia alikuwaje wakati anasukumwa na tawi la TANU Udsm!! hadi akakimbilia jeshini nako akafeli!! muulize vizuri jinsi anavyoendesha nchi bila kujua chanzo cha umaskini wa anaowaongoza!!
A traitor is always a traitor!!!!
 
Hata yule professor Muongo badala ya kuangalia hoja aliangalia performance ya muuliza swali eg. Ole sendeka etc. Wewe pamoja na wenye mawazo mgando kama wewe na wasaliti wenzio wanafikiri degree ndiyo inayoendesha nchi. Muulize huyo mwenyekiti wa chama ulikohamia alikuwaje wakati anasukumwa na tawi la TANU Udsm!! hadi akakimbilia jeshini nako akafeli!! muulize vizuri jinsi anavyoendesha nchi bila kujua chanzo cha umaskini wa anaowaongoza!!
A traitor is always a traitor!!!!
Akili za kuambiwa changanya na zako.,ukidanganywa nawe ukaenda kutoa ushuhuda mbele ya watu juu ya uongo ulioambiwa watu wanakusema wewe kuwa ndio muongo. Linda heshima yako, jiepushe na ujinga.
 
Akili za kuambiwa changanya na zako.,ukidanganywa nawe ukaenda kutoa ushuhuda mbele ya watu juu ya uongo ulioambiwa watu wanakusema wewe kuwa ndio muongo. Linda heshima yako, jiepushe na ujinga.
Nirudie kwa herufi kubwa: YOU ARE A TRAITOR!!! and you can not be trusted by thinking humans
 
Back
Top Bottom