nashukuru Tabutupuila sidhani kama nnaamini asilimia mia hao washauri kwa kuwa kama binaadam nadhani nitawaeleza sehemu ya tatizo tu,nafikiri wa kujisaidia zaidi ni mimi mwenyewe,sielewi kwa nini kila nikisoma Signature yako nasikia msisimko fulani naomba usiibadilishe tafadhali,huwezi jua unalisha nini baadhi ya mioyo ya watu
Tunaomba mwisho wa huo mwanzo wako!!!
mimi yangu itajaza kurasa ila ndio sababu ya kutokuwa na mwenza mpaka leo,nikimwangalia mwanaume machoni namwona yuleyule aliyenitenda
4.unatakiwa ufanye bidii ya kuwa karibu na wanaume, zungumza nao, chat nao, tembea nao hadi uone huna hofu tena mbele yao.
sasa hapa ndio tatizo kila nikiwa nae nikimwangalia machoni naona kama macho yake kuna kitu yananiambia,naanza kumchukia ndani kwa ndani mpaka mwisho chuki inatokeza hadharani
yaani nashindwa ongeza neno hapo,ila nashukuru angalau uko ok now,swali moja huwa najiuliza kila siku kwanini watu wanaumiza wenzao kiasi hiki,je huwa wanajua kuwa wanakuumiza au inatokea tu,nikipata jibu sawia la hili naweza jaribu tena kinyume cheke sorry siwezi kuwa mhanga ena
Lakini darling si tulikubaliana hutawaeleza watu hii stori. aargh umeniudhi sana..........ila nimekusamehe kwa sababu bado nakupenda.haha, basi ngoja nikupe brief
kuna mtu wakati anaanza mazungumzo ya mapenzi na mimi alipata medical case akafanyiwa surgery ambayo iliyotishia reproductive health yake alilazwa hospitali muda mrefu na alikuwa amechanganyikiwa sana. mimi nlikuwa safarini, niliporudi tu moja kwa moja kutoka airport nilifika hospitali kumuona na mabegi yangu kwenye gari. kudhihirisha alivyonipenda mbele ya ndugu zangu na zake, alinitaka niombe chochote kutoka kwake naye atanipa. mi nilimuomba anifanyie mambo mawili tu, moja asahau tatizo lake na pili atoke hospitali na kurudi nyumbani.
kila mtu alinishangaa na wengine walinilaumu kwa masharti yale kwaani waliona kama namshawishi atotroke matibabu. yeye aliniambi hataweza na hajaruhusiwa na dk lakini atajitahidi kumuomba dk amruhusu kutoka hospitali. nilimuahidi kuwa kesho yake nitakuja kumchukua, kwa hiyo ajiandae na amfahamishe dr kuwa amepona kesho anarudi nyumbani. alijitahidi akaanza kwanza kumwambia nesi mmoja aliyekuwa anamhudumia na nesi alimueleza dk, dk alikataa na kesho yake alipopita kukagua wagonjwa, alimkumbushia. mimi nilifika kama saa 5 asubuhi nikaambiwa amechukuliwa na dk kwa uchunguzi zaidi, baada ya kama dk 45 hivi, alirudi na kutuambia ameruhusiwa kutoka hospitali!
ndugu zake walicharuka, wengine wakasema nataka kumuua ndugu yao, walimfuata dk kumuonya kuhusu kumruhusu ndugu yao kirahisirahisi vile hasa baada ya ushawishi wangu, dk alishangaa kusikia kuna mtu ameshawishi ile ruhusa kwani alikuwa hata hajawahi kuniona. baadaye nilimfuata chemba nikamueleza kuwa mimi ndiye ninayelaumiwa. akaniambia kuwa amempima kwa kina na ameridhka na amemruhusu na kuwa matibabu mengine atakuwa anafuatilia akitokea nyumbani. kweli tuliondoka na ndio ulikuwa mwanzo wa yule ndugu kupona hadi leo.
kwa kweli familia yao inanipenda sana hadi leo na baba yake alinipa zawadi kubwa sana amabayo napenda niiache siri kwa leo
Lakini darling si tulikubaliana hutawaeleza watu hii stori. aargh umeniudhi sana..........ila nimekusamehe kwa sababu bado nakupenda.
Ni demu anitwa rozi nilimzimika ile kivile/
aliniweka chini sikufurukuta ka msukule/
alinifanya niamini niitarajie harusi
lakini alicho nitenda/ ni bora ninge ugua virusi.....
Nikikumbuka sad ending yangu, machozi hunitoka na niliapa kutopenda tena mpaka pale mama yangu mzazi aliponiuliza usipowapenda wanawake nani atakuwa mama wa watoto wako au na watoto nao umewachukia?
yaani nashindwa ongeza neno hapo,ila nashukuru angalau uko ok now,swali moja huwa najiuliza kila siku kwani watu wanaumiza wenzao kiasi hiki,je huwa wanajua kuwa wanakuumiza au inatokea tu,nikipata jibu sawia la hili naweza jaribu tena kinyume cheke sorry siwezi kuwa mhanga ena
Mimi nina ya mshkaji wangu, alikuwa anampenda kweli binti na akawa amepanga kumfanyia surprise ya kumvisha pete ya uchumba. Yaani jamaa alikuwa ameshadhamiria kumwoa binti. Siku ya siku ikafika jamaa kajiandaa na surprise yake tupo tunamngojea binti aje, basi ile kufika yupo na rafiki yake kumbe binti naye ndo alikuwa amepanga kumwaga jamaa siku hiyo....
Jamaa akaitwa pembeni, binti akamwambia Bwana samahani ila inabidi nikueleze; kuna Bwana nimempata na naona kuwa tunaendana naye zaidi na ameomba kunioa na mimi nimemkubalia, ila naomba tuendelee kuwa marafiki na tuwe tunasaidiana kama kaka na dada. Jamaa karibia azimie, kama jitihada za makusudi hazikufanyika....
Baada ya hapo Binti akaolewa na Bwana chaguo lake na rafiki yangu Mungu si Athumani akapata mke (tena yule rafiki yake binti aliyekuja naye siku ile) jamaa amebahatika kupata mapacha wawili na Binti naye Mungu kamjalia kabinti na muda si mrefu anategemea kupata kitoto kingine cha kiume. Mpaka leo wanaendelea na maisha vizuri kabisa na ni family friends na binti amemtambulisha jamaa kwa mumewe kama kaka yake na wanaheshimiana na kushirikiana utafikiri watoto mapacha vile. Kinachonifurahisha zaidi, jamaa ndiye mshauri mkuu kwenye ndoa yao, na Binti halikadhalika amebeba jukumu la kuishauri familia ya jamaa yangu kwa maana anawajua wote vizuri.
Mwanangu kwa kutengeneza story nimekuvulia kofia....