My first ebay shipping

shanediesel

Senior Member
Joined
Apr 11, 2014
Posts
103
Reaction score
26
Kwanza kabisa nichukue fursa hii kuwashukuru Wanajf kwa kutoa elimu kuhusiana na manunuzi mtandaoni,kutokana na hilo nikaona ni vyema nami nijaribu kufanya manunuzi kupitia ebay,kwanza nilijisajili kwenye website ya ebay then nikajisajili kwenye website ya Paypal ambayo inakuwezesha kufanya maninuzi mtandaoni kwa usalama zaidi.

Baada ya kujisajili na Paypal wakaniambia nilink kadi yangu ya benk na nikafanya hivyo,baada ya siku chache wakatuma paypal code kwenye benk ya Stanbic ambayo ndiyo ninaitumia, kwakuwa ninatumia huduma ya Bank sms alart ilikuwa rahisi kuzipata zile code '4'digits kupitia smsa toka stanbic bank.

Baada ya hapo ndipo nikafanya uamuzi wa kununua Power Bank ya kuchaji simu ili nione kama itafika bongo maana kumekuwa na uzushi mwingi kwamba Posta wanaiba parcels za watu. Nilinuanua tarehe 20 mwezi wa pili na kwa mijibu wa seller aliniambia mzigo utafika baada ya wiki 2, nikasubir baada ya wiki 2 lakin mzigo haukufika,

nikaongeza kusubiri wiki ya 3 ili nione mzigo kama utafika lakini haukufika ndipo nikafungua kesi paypal na baada ya kufungua kesi paypal wakampa seller muda wa kujibu na ikachukua hadi mwezi na nusu toka siku niliyonunua lakin seller hakujibu ndipo paypal wakanirefund pesa yang yote na wakaniambia kwamba itaonekana kwenye bank statement baada ya siku 20 lakin haikuwa hivyo baada ya siku 5 kunirefund ile hela iliingia moja kwa moja kwenye acc.

yang ya stanbic bank bila hata kujaza fomu wala nin na niliweza kuitoa siku iliyofuata na hata sms alart iiliyoingia ilionyesha ni refund toka paypal na hata kwnye bank statement ikaonyesha hivyohivyo,bas nikajua ule mzigo hautafika lakini cha kushangaza leo nimeenda Posta nimekuta card ya mzigo na nilipoenda dirishani kuwaonyesha wakanipatia mzigo wanga wa Power Bank niliyoagiza toka mwezi wa 2 ndio imeku kunifikia mwez wa 6.

Ndugu zangu wana jf Ebay ni waaminifu msisite kununua vitu toka kwao na benk nzuri naona ni Stanbic bank maana hata wakikurefund huna shida ya kujaza fomu ili upokee pesa yako bali wao huiingiza direct kwenye account yako. Ni hayo tu.
 
Mkuu kwa hiyo ndo tuseme umepata power bank ya bure? Hongera
 
EBay,Amazon ni reliable Sana Na kogan Mimi kitu cha dola 700 Na nunua dola 300 ni mzoefu ingawa sababu Niko Australia watu waoga pia ni associate marketer wa Amazon
 
Wako vizuri eBay ni kampuni kubwa Na hawawezi Fanya uhuni hata siku moja ila kuwa makini kusoma maelezo ya muuzaji wa bidhaa unayonunua
 
shanediesel Kuna umuhimu sana kuwa na sanduku la posta, maana nishawahi kujaribu kununua kitu ebay (SSD External Drive) na nikafikia hata hatua ya kutakiwa kujaza namba ya Mastercard yangu (CRDB) lakin sehemu pa sanduku la posta nilipaacha wazi na haikuleta error yoyote na cha zaid wakanipa uhakika wa kufikishiwa bidhaa, ndipo nikasita kuendelea, Hebu nipeni elimu hapo, sanduku la posta linahusika sana katika huduma hii

cc; chief-mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri muhimu ni physical address ndo muhimu zaidi maana wanaoleta mzigo wanataka usaini Kama umeuchukua
 

Hapana mimi huwa ninaagiza bila kuandika sanduku la posta , kama wakinipa tracking # inakuwa rahisi kidogo, bika tracking # mzigo wako utaupata pia pale posta watakupa maelekezo
 
Last edited by a moderator:
Sio kwamba seller atawasiliana na paypal na bank ili ulipe hiyo fedha? Au ni zawadi ili kujenga good will?
 

Mkuu sanduku la posta linahusika sana maana ukisha nunua seller anakuuliza unataka kuship kwa address gani,siyo maseller wote wanatumia Fadex na Dhl,wengine hutumia shipping za kawaida tena huwa inaandikwa shipping cost ni bei kazaa!...,

ukitumia njia ya posta mzigo ukifika utaikuta card kwenye box yako then unaichukua ile kadi na kitambulisho chako unaenda dirishan wanakupa mzigo wako.
 
EBay,Amazon ni reliable Sana Na kogan Mimi kitu cha dola 700 Na nunua dola 300 ni mzoefu ingawa sababu Niko Australia watu waoga pia ni associate marketer wa Amazon

Mkuu Amazon naona kama hawatumii paypal? sasa kama mzigo haujafika wanakurefund vipi upande wa Amazon ?
 
Hapana mimi huwa ninaagiza bila kuandika sanduku la posta , kama wakinipa tracking # inakuwa rahisi kidogo, bika tracking # mzigo wako utaupata pia pale posta watakupa maelekezo

Hiyo cjawahi jaribu mkuu ila ntajaribu kununua kitu cha bei rahisi then nisiandike address then nione kama utafika
 
EBay,Amazon ni reliable Sana Na kogan Mimi kitu cha dola 700 Na nunua dola 300 ni mzoefu ingawa sababu Niko Australia watu waoga pia ni associate marketer wa Amazon

Mkuu hao jamaa wa kogan masharti yao yakoje? na wanapokea malipo kwa mfumo upi ?
 
Sio kwamba seller atawasiliana na paypal na bank ili ulipe hiyo fedha? Au ni zawadi ili kujenga good will?

Mkuu walisha nilifund toka mwezi wa 4 so sidhani kama seller atawasiliana na bank na paypal.
 

Mkuu wala usisite hawa jamaa ni waaminifu sana. jaribu theni uje utupe ushuhuda hapa
 
Kogan unatumia MasterCard policy ya kuwarefund ipo karibu. Kila kampuni kubwa cha muhimu kuhakikisha ni website yao niliagiza Google Nexus kwa Au$389 wakati dukani ni dola Aus $697
 
Mimi jamani kwenye hilo sanduku la posta imekua kikwazo kikubwa kwangu....nasina hilo sanduku la posta ss cjui niagize vp ili kinifikie...na nikiagiza bila sanduku la posta ntajuaje kma mzigo umefika....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…