My ex gf's husband ananitishia maisha

My ex gf's husband ananitishia maisha

Salaam wakuu, mimi ni Yule yule wa kanaida.

Huyu jamaa alinichukulia demu niliyekuwa nae kwenye uhusiano kwa miezi 18, alimdanganyadanganya na hela yake ya sembe, akamshawishi aitoe mimba yangu ili amuoe, demu akaingia kingi, akaitoa akaolewa, hiyo ni karibu miaka minne iliyopita, ndio nikaamua sitaki tena mke kwenye maisha yangu.
Hivi karibuni jamaa alienichukulia demu naona amezidisha chuki dhidi yangu, ananifanyia vioja kibao. Za chini ya kapeti zinasema kuwa kutokana na makosa ya kidaktari yaliyotokea wakati wa kutoa mimba, demu hawezi tena kushika mimba, jamaa anapanga kunibambikia kesi ya sembe, na jamaa Ana mkwanja mrefu, akiamua anaweza.

Nifanyeje?

Huyo Bwana akuchukie wewe kwa sababu mkewe hawezi kujifungua tena kutokana na kosa walilolifanya wao?? basi atakuwa mwendawazimu huyo. Baada ya kuishi na mke miaka mine pengine amegundua kuwa Mkewe bado anakuota wewe na hivyo kutishia ndoa yake au wewe na huyo mkewe bado mwawasiliana.
 
mwite muulize anataka nini?

kinacho msumbua huyu jamaa ni hiki..!
quote_icon.png
By kijani11
we hujaendelea kumfuatilia huyo demu baada ya kuolewa kweli? Maana kwa nn atake kukupoteza?!




Ni kweli nilikuwa nabofya Mara moja moja, Lkn muzee ya sembe hajashtukia, inaonekana bifu ni kwasababu mkewe hashiki tena mimba na anaona Mimi ni chanzo
 
Just google, uncut men are gud on bed. Ni wale tu wasiojua.

mimitungi,google is just a search engine,si kila unachokisoma google ni kweli na sahihi,naweza nikaandika habari yoyote isiyo sahihi na ikawa online wewe ukiingiza maneno sahihi wakati unasechi ikaja habari yangu hiyo hivyo kuanzia leo habari yoyote utakayosearch tumia akili yako kutafakari ukweli wake

lakini pia kuwa uncut haimzuii mr uncut kuwa good on bed.....na kinyume chake ni kweli!
 
Ujasiri wako ni kumtumia huyo mwanamke amlegeze, asiwe anakufautilia kihivyo, Hafu unaonekana unamwogopa sana mume mwenzio nakuomba ugangamale.

Mkuu, ujasiri utatoka wapi kupambana na mtu mwenye pesa. Yasikie kwa mwenzio wala si kwako.
Juzijuzi my bro katoka gerezani kwa kesi ya kusingiwa kuua kwa kisa kinachofanana kwa karibu na hiki.
 
Ni wewe tu umekuwa ukimfuatilia mtaani,
miaka minne leo akufuate kwani huyo demu alisahau nini kwako.

Ndo tatizo la kutoa mimba; unakuta umeandikiwa katoto hako kamoja
na unakatia kwenye pipa; ni lazima ubaki hivyo hivyo.
 
Nashukuru huyu jamaa ametajwa
kwenye list ya wanaotuhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya na sasa ananyea debe
 
Dogo na usipotajwa list ya kesho we mwanaume, huwezi nitombea mke wangu afu unaongea uongo humu
 
Back
Top Bottom