My Dad's Legacy!

ewards

Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
8
Reaction score
15
Hello Guys,

Leo tuambizane nini baba yako ama mlezi wako wa kiume, amekuwa akikufundisha/akikueleza/ kushauri kuhusu maisha na mahusiano kwa ujumla wake ili nasi pia tujifunze/kuchota busara za wazee wetu hawa.

Baba yangu hakuwa mtu wa stories, alitufundisha kupitia matendo yake. Kitu huwa anasisitiza ni upendo kati yetu sisi vijana katika famila lakini pia kujali sana mambo ya kidini na kuhudhuria Ibada.

Mzee hakuwa mtumiaji wa kilevi aina yoyote ile, kitu ambacho naamini kama si yeye basi ningeangukia katika mtego huo.

Kitu cha mwisho kutoka kwake, aliepuka sana ugomvi ama kutoelewana na mtu kwa namna yeyote ile.

Yangu ni hayo, tafadhali tuambizane mambo ya muhimu mlio elezwa ama kufunzwa na wazazi wenu wa kiume, Wale ambao pia mli pata bahati ya kusikia neno la mwisho /wasia kutoka kwa wazee wenu, ikikupendeza tafadhali share nasi hapa.

Karibu.







 
Matendo yake yamenifunza mengi japo yeye si mzungumzaji sana ila tabia zake sijutii kuwa nazo (Baadhi) alinikanya nisipige mwanamke. Mbali na hapo aliamini yeye ni mmoja kati ya walevi wazuri sana japo hatumii pombe, kwa mujibu wa maelezo yake alidai anataka anywe pombe akibaki nyumbani na mke wake baada ya watoto kuondoka kwake.

Mbali na hilo alinifunza ubabe, kazini kwake ukimletea utovu wa nidhamu lazima upitie zahanati wakati unarudi kwako kupima kama fuvu la kichwa liko sawa. (anapiga vichwa huyo).
 
usimchoke mkeo hata awe na mapungufu ya namna gani sababu wewe ndiyo uliyemchagua kwa Mungu ni dhambi

alisema mengi japo hakuwa muongeaji sana pia zile akili za utoto faza akirudi tu kila mmoja anatafuta sababu ya kutoka sitting room ndo maana nilikosa mengi na umri pia ulichangia kutopata maneno ya busara kutoka kwa mzee

hilo ndo linazunguka akilini mara nyingi....Allah amrehemu
 
It is very very funny

Mara nyingi mwenye nguvu za kiuchumi kwenye familia mitoto hua ndio inayompenda and not otherwise..

Mitoto ni minafiki sana na inafuataga penye pesa na uchumi..

Dishonest rascals!
 
Baba yangu huwa ananiambia,
"Hata kama kadri unavyotembea kwenye maji ndivyo maji yanavyozidi kukuzidi ,... Hata mwili wote ukazama kwenye maji kikabaki kichwa tuu ..jua bado lipo tumaini.. Hata kichwa nacho kikaanza kuvaliwa na maji .. Marufuku kukata tamaa bado lipo tumaini."

Kwa maneno yake hayo yamenifanya hata nione ugumu wa maisha kiasi gani .. Sikati tamaa napambana maana najua tumaini lipo.

Bado nafikiria ni zawadi gani nzuri zaidi kwa ajili ya Baba yangu.
 

Hahahahahaaaa

Leo watu wana-quote mistari ya movies na novels as hard as they can...

Utadhani kweli hawa dads walikua wanasema haya yote!
 
Hahahahahaaaa

Leo watu wana-quote mistari ya movies na novels as hard as they can...

Utadhani kweli hawa dads walikua wanasema haya yote!
Movie na novels wahusika wake sio binadamu?
Au wanaandika vitu ambavyo havipo duniani kabisa.. ? Maneno yao yanatoka sayari nyingine?
Unatia huzuni kwa kweli.
Ila siyo mbaya maana kwa Mara ya kwanza umeyasikia kwenye movie na novels..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
''Lishikeshike lingali kichwani, likianguka vigae!!!''........

Elimu ndio ilikuwa wimbo wa taifa wa mzee wangu, japo sikufika (kielimu) alipotaka lakini anakula bonus kutoka kwangu sana tuu.

Kila akikutana na watu anaofahamiana nao, utasikia... ''huyu binti yangu wa pekee kitinda mimba wangu, yuko .......kikazi nampenda sana''.

Kasinde.
 
*He always wanted me to be close to God. Hata nikikengeuka i always find my way back through his words, he built that foundation for me.
Kila tulipovuka hatua fulani +ve or -ve kwenye maisha yetu, alitufundisha kushukuru kwa kutoa sadaka maalumu ya shukrani.
-Nilipokuwa napitia kachangamoto, alikuwa ananiambia "HS kwa nini usifunge then tutoe na sadaka". Ninamshukuru mno kwa sababu alinijengea msingi imara wa Imani, kila siku najitahidi kuwa karibu na Mungu. Siachi changamoto au dhambi zangu ziniweke mbali na Mungu. Naanguka, narudi nyuma, ila I will surely find my way back to God. That's the path he directed me and I finally chose it as my path too.

Bado nayakumbuka maneno yake "Kuwa na bidii na muombe Mungu. Unajua nilipotoka na nilipo leo, sikuwa na mtu yeyote "mkuu" wa kunisaidia, ila ni kwa neema tu za Mungu, ameninyanyua hadi hapa nilipo"

*He valued friendship like nobody's business. And that went directly to my soul. I value friendship and I'm grateful God has blessed me with multiple loyal friends. We have always been far from each other, but we have always got each other back. Mungu tutunzie urafiki wetu

*Standing my ground lol. I guess this is what has made me a lil bit stubborn. Nikisema yes or no ndo itakavyokuwa, though in a very polite way lakini ndo nimeshamaliza. But, I honestly love this "lil man" in me.

*Alikuwa anapenda sana kututania, he had petty names for all of us. Alikuwa anatuambia "nyie me nikifa mtalia sana, wenzenu nyumba nyingine wakisikia tu baba anakuja wanakimbilia uvunguni, nyie ndo kwanza mnakuja tupige story. And yes, only God knows the gap he left in our hearts and lives

*He cared for us too much, and I am over-caring and I like attention too much. My man was always there for me. Still remember nikiwa mdogo ananiogesha ,ikifika jioni we would go for an evening walk. Baada ya kuanza shule, alinisaidia home works zangu zote anytime nilipohitaji msaada wake. Kuna muda weekend hatoki ananisaidia kusikiliza nachotakiwa kwenda kupresent j3 shule. And yes sijasahau how he would write me some short sweet notes on how he loves me. He would send me cards, paying me surprise visits at school/college. Bila kusahau kunitumia messages za "grand warnings", anataka nibehave vipi esp baada ya kuingia chuo. Alijua ratiba zangu zote, kuna muda nipo kwenye mtihani, ananitumia message ya kuniombea kwenye mitihani yangu. He created very beautiful memories of my life. And our bond still today, I believe it was purely made in heaven. Pa, I love you so so much

Ni mengi mengi siwezi kusimulia yote, though it still hurts me, I couldn't understand what he was trying to tell us in his last minutes.......... And till today I always talk of him as if he is still alive. Sijaweza kumuita marehemu not even once........ May you continue to rest in perfect peace swts
 
Baba wa Taifa alisema tudumisha Amani na Upendo pia kuheshim kila mtu!!
 
sio kila mtu wa kumjibu, unampa like tu kuonesha ujumbe wake uliusoma

mwezi ujao tuanze darasa letu ticha ahahaha........GGMU
 
Daaah nitacomment baadae
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…