My cup runeth over ~ Na Kikombe changu kinafurika

B. TEAM BUBAA



Ismail kanogewa na penzi la Chura Hidaya, siku wamekaa wanakunywa chai anamwambia Hidaya me nataka kukuona ivoo ujue, nipo serious
Hidaya: na mke wako je?!
Ismail: yule marehemu mtarajiwa, achana nae! Anakufa siku yoyote
Hidaya akaumia roho, sio kwa mwanamke mwenzake kunyanyapaliwa vile! Akamwambia ngoja kwanza nifikirie nipe miezi 2 nitakujibu, Ismail akajaa mapumbu akawaka mpaka usoni, Ismail sijui kawaje hamwangalii tena mke wake anashiiinda kwa hidaya mpaka Hidaya anaona ai u anataman kuhama lakini katumwa kazi tu pale lazima apige! Tobaa!

Mazishi ya Selina yakatimia, wakajaribu kutangaza kwenye redio ndugu wajitokeze hakuna kitu akaishia kutokea Pendo na mimba yake kubwa ya miezi 8 na Joseph wakaamua wamzike makaburi ya pale pale Lusaka! Wakamfanyia ibada pale! Wakaaga akazikwa, Drogba analiaaaaa ameshikiliwa na baba yake mzazi na pacha wake Didie! Oga anaangalia tu movie linavyoenda anachekea moyoni huku wamesimama na mama yake
Saa ya kwenda kumwaga mchanga akajitumbukiza kwenye kaburi na yeye anataka kwenda na Selina,tobaaa! Watu wakaingia ndani kumtoa akiwepo Oga na Pacha wake wakampeleka kwenye gari wakafukia maiti, jioni anarudi nyumbani anaona nyumba chungu wazazi wakakaa nae kwa wiki 2wakaona hawezekani kuishi tena pale wakapangisha nyumba akahamia kuishi na Didie wazazi wakarudi kwao Lagos!



Pendo akawa anaongea na Joseph haelewi Selina amekufaje kufaje, akawa anashangaa taarifa za ghafla! Wakawa wanaongea pale na kupoozana, bado wiki 1 ajifungue

Kandi ana mimba ya miezi 7 akasikia Maringo amejifungua ana mtoto wa kiume akamweleza mumewe Joe, tobaaa Joe akamind habari za wapenz nilioachana nao usinieleze akawa mkali ghafla ananuna akaleta vitimbwi Kandi hakuelewa kwanini, akanyamaza kimya

Maringo ameshazoea maisha ya uzazi, toto limesogea limenenepa, akawa anamalizia siku zake za clinic mamake anamhudumia, akawa amenenepa kidogo hata kutembea hawezi miguu imejaa alipoona amekaa fresh bado mwezi m1 arudi kazini akaanza mazoezi ya kutembea mdogo mdogo ilimradi arudishe mwili, akammiss sana Patric anampigia simu akiwa anafanya mazoezi njoo basi me nipo pekeyangu jaman, Patric anakuja wanapigana miti wee anarudishwa mpaka getini Patric anasepa.
Tabia ikawa kama mazoea, siku anarudishwa Rasheed akaona gari ya Patric, Maringo akashuka Patric kumwona akaondoa gari fastaa, Rasheeda akamwuliza nani huyu?! Maringo akamwambia rafkiangu kwanini?!
Rasheeda: akaguna! Mh mbona anaendesha gari la mtu ambae namjua?!
Maringo: nani unamjua mama zaidi ya familia yako au hachikoko?!
Rasheeda: hapana bwana me najua ile gari ya mpenz wangu
Maringo: akapotezea pale bwana magari yanafanana mama na wewe! Au unataka aje siku moja umfahamu?!
Rasheeda: mwambie aje kesho nimfaham aje na gari iyo iyo asibadilishe!
Maringo: akamjibu sawa mama tutapanga moyoni anasema tobaa Yesu na mie nakamatwa mwizi, kwanza hapa mama analea mtoto au mjukuu wake?! Akajichekea mwenyewe. Kweli Maringo kichwa panzi!

Suzana nae mimba imesogea miezi 8 sasa anasubiri wiki ajifungue, Bank manager amepandishwa cheo zaidi ya kile alichokuwa nacho akawa anafanyia makao makuu na Musa, na mshahara ukaongezeka akawa anam pimp Suzana manguo, viwalo, magari, vacations, holidays na watoto! Watoto wakampenda Musa, akawa ameshakuwa kama baba yao, hata Luwi akienda pale wanamsifiaaa Bank Manager as usual Luwi akamind lakini afanyaje akawa anasubiri tu muda wa mahakama anyakue chake!

Neema yupo na zee lake Masoud, wanapigana miti mimba ya miezi 7 inaenda 8 sasa! Kiila week kwao wanaenda outings, date night na mimba kubwa! Watoto wako boarding wakirudi hawatoki, Neema akawa anayapenda maisha yake mapya na zee la kiislam, J2 anaenda zake kanisa lingine sio lile la mumewake, Masoud anamsindikiza ivo ivo, Masoud akienda msikitini Neema anabakia ndani.

Pastor David akaumwa sana nadhani na mawazo yakachangia, akampigia simu mke wake akamwambia njoo na mumeo mpya nataka kuacha mirathi! Sina muda mrefu natakiwa kutubu mje na watoto. Wakafika pale akaanza kufunguka akaomba msamaha Neema nimekutoa mbali Tanzania nimekuja kukuharibia maisha karibu na uzee naomba unisamehe, mimi sioni kama bado naishi, sina muda mrefu nimekukosea sana na watoto naomba unisamehe akaomba msamaha watoto, watoto wanashangaa na kulia hawarlewi wakamwambia daddy dont talk plz unaumwa wewe! Huku anakohoa akaendelea kuongea, Masoud take care of your wife kwao ni tz ametokea Upanga, akueleze vizuri wazazi wake wanaishi Upanga bado wanafanya serikalini, ukimshindwa mrudishe kwao me nimeshindwa kutekeleza ahadi ya kama nikimshindwa nimrudishe kwa wazazi wake la sivyo nitalaaniwa sasa nakukabithi wewe kijiti Masoud, lazima uende ukajieleze kuwa wewe ndio mume mpya wa Neema! Masoud akajibu sawa hamna neno, akamwambia Masoud weka mkono wako kwenye paja langu na ushike Mapumbu ishara ya kuapa kuwa utatekeleza ulichoahidi. Masoud akafanya kama alivyotaka Pastor, akampa na barua toka kwa Baba yake Neema! Neema anashangaa tu, akaroa boxi lina mali zoote za Pastor, na mirathi akampa mke wake nikifa hivi vyote ni vyako na watoto, wapeleke watoto expensive schools uza hivi vitu pl watoto wasome vizuri watakusaidia baadae! Neema hasira imeshamwisha analia tu sasa kweli mtu akiondoka unajua tu! Akawabusu watoto wake 3 Paul, Mathew na Esther. Akaomba Pastor Msaidizi aje na mwanasheria, Mwanasheria akaambiwa me nimeshakabithi kila kitu kama mahakama ilivyotaka nikifa kimi watoto watabakia na mama yao kama Masoud atatekeleza kurudi Tz kuwaona wazazi wa Neema na kupeleka huo mzigo wa bahasha kwa baba yake na Neema, Mwanasheria akasema sawa, akishapeleka kwa babake mzazi atapewa barua ingine atakuletea kwa uthibitisho then mahakama itoe full custody kwa Neema kuwa mwangalizi wa maisha yote ya hawa watoto! Pastor David akamwambia Pastor junior amwongoze sala ya toba! Akaongozwa pale akawaambia mkae kwa amani nitakuwa nawaangalia toka juu, naamini aends Mbinguni nina amani zote rohoni, akafunga macho ndio ntoleeee, Pastor is Dead!
Watoto wanaliaaa baba jaman rudiii, mwanasheria akawazoa watoto nje na Masoud Neema akaliaaa maskini hurumaa!



Patric kesho yake akaamka akaenda kwa Pastor maana maluwe luwe ya ndoto hayaisgi, akafunguka pale kwa Pastor wa kanisa lingine kabisa sio la mume wa neema.
Pastor: nimekuelewa muheshimiwa. Hauna siku nyingi chini ya jua, usipobadilisha maisha yako mapemaa, utakufa na dhambi utaenda motoni!
Patric akachoka. Sa me nina wake 2 nabadilishaje maisha wakati wote nawahudumia lakini hawajuani
Pastor akaguna! Mmh na kawa wakija kujua itakuwaje!
Patric: Pastor embu tufanye kwanza toba ya hii kitu yangu ya ndoto mambo ya ndoa baadae maana sina mchepuko nina wake 2 tu sa ivi ndio ninawahangaikia
Pastor akamwambia kuna dhambi umeifanya na mtu kijijini itakuumbua au la kajisalimishe both ways utawekwa ndani maisha, ukitubu seriously unaweza kubaliwa dhamana, ukakaa nje ila mali zako zoote zitafilisiwa na kazi utafukuzwa sasa utaweza wahudumia bado hao wake 2?!
Patric akachoka akakumbuka dhambi yake na Ismail. Sasa nafanyaje Pastor nina muda gani mpaka tukio litiki?
Pastor: una wiki 3 tu.. ulitubu hata ukifa hautaenda motoni, kuna vitu Mungu atakuepusha navyo ukitubu!
Patric akaomba aombewe pale ataenda kufikilia kuhusu dhambi ya kujisalimisha kwa pilato! Akaombewa pale akatubu akarudi nyumbani anawaza wiki 3 na anamtoro itakuwaje? Waza wZa na wewe akapata akili

Kungwi amekaa zake mwenyewe anawaza maisha yake kama ndio yatakuwa mabaya vile bora ajisalimishe kwa muumba! Tobaa akaenda dukani akanunua sumu ya panya akaenda akaandika kikaratasi, kweli wa kungwi anaakili mbovu za kujiua kama akina nanii wale wa kusini, hehe! Me siwataji msije mkanifunga!
Kaandika barua reeefu akameza sumu akalala kitandani, wakarudi akina Caroline na Pendo na Joseph wanarudi saa 11 jioni wanamwangalia hawamuoni, Pendo akaenda chumbani kwake akamkuta amelala akamwacha akaendelea na kazi, jioni wanataka kula mh mbona maza kalala, embu niende kumcheki, kumsogelea lahaula hamna cha kungwi wala nini? Amsha amsha na wewe akapiga makelele akaja Joseph na Caroline nini?! Mama amekufa, Joseph kumcheki hamna kungwi saaa nyingi alishasepa mbele za haki, wa bariiidi kama barafu akamfunika akamtoa Caroline na Pendo ambae alikuwa analia kama chizi! Akapiga simu polisi wakaja kusolve kesi wakakuta barua na ile sumu imemwagika chini, wakachukua vyote wakatoa maiti wakapeleka mochwari
Pendo analiaaaaaa hana baba wala mama, uuuwi you can imagine Pendo ana mimba ya miezi 9 alafu mama unaemtegemea mama ndo kasepa!
Majirani wakajaa pale pendo analia hataki kubembelezwa wakamchoma sindano ya usingizi akalala



ITAENDELEA KESHO SAA 5 ASUBUHI NIKITOKA CHURCH MIEEE
LOVE YOU ALL
 
B. TEAM BUBAA




Selina akatoka kuoga, akamkuta Drogba amekaa kwenye kiti, akasmile anamfuata akamkumbatia Nimekumiss mume wangu, wakaanza kupigana mechi! Kwichi kwichi kwichi kwichi! Drogba anaskia utam, baadae akaskia mtu anamshika began, Drogba Drogba! Drogba wake up Ooo, time is running ooo wake up naaaw! Akaamka kumbe ni ndoutoooo! Du! Kuangalia dyi dyu imesimama noma noma mshkaji akaenda kuoga anatamani Selina angekuwepo bafuni na yeye, akavaa nguo wakaondoka na Didi na Oga kwenda kanisani. Ilikuwa jumapili wanatoa sadaka ya shukrani baada ya Selina kufariki

Ibada ikaendeshwa pale wote wapo happy, wakatoa sadaka ya Shukran Drogba analia anasema my life will never be the same again! Without my Selina lakini namshukuru Mungu sana.

Mary nae akawa anajiandaa kwa mazishi ya Pastor David, jioni saa 10, Neema akaja amevaa gauni nyeusi analia, ndio mume wangu cheated ila inaumaje sasa watoto wamelia mpaka wamechoka, ibada ya mazishi ikafanyika pale wakaaga kila mtu analia kila msharika analia jaman Pastor David wanamwangalia hawaamini, dah majanga! Pastor kafa na ukimwi, kweli ukimwi hauchagui dini wala rangi, unababua tu!
Wakaenda kuzika wana familia wanatakiwa kumwaga mchanga, wakamwaga pale wote akina Neema na watoto, baadae Mary nae anataka amwagie Neema akamkata jicho, wakati anasogea akaenda kumzaba kibao akaangukia ndani ya Jeneza, Neema akamwambia ukome kufakamia vya watu hata kaburini unataka kuwa mwana familia? Jini Jezebel mku wa wewe! Kufa na wewe embu mwagieni michanga afie mbele tutamkuta ahera kama sio peponi, Mary analia waumini wakatumbukia pale kumtoa, hehe chezeiya 6 feet under wewe! Noumer sanaa
Baada ya watu kutawanyika watoto wanamwuliza mama yao what is like to be in heaven? Neema akakosa jibu akawaambia some day mtajua, wakamwambia we wanna go to heaven one day maam, please! Neema akakosa nguvu Masoud akawachukua wakaenda kuoga kwenda kulala!



J3 mazishi ya Kungwi yakafanyika pendo analia haachi, Caroline nae anamsindikiza kulia tobaa! Joseph alikuwa na wakati mgumu sio kitoto! Msiba ukajaa pale ikabidi Rasheeda na wamama wa kijijini waje, wakasaidiana na majirani pale, wakaaga, wakaenda makaburini, Masoud na Neema nao walikuwepo Masoud analia lakini sa afanyaje, ndo ishatokea tena akatoa pole kwa Pendo na Joseph na Caroline, Masoud akaweka mchanga na familia ya Pendo, Rasheeda akaweka pia na wamama wa kijijini hata mwl mkuu alikuwepo wanasikitika tu basi sasa wafanyaje, Drogba na Didie walikuwepo walisikia kwenye redio hawakuelewa amekufaje fasta vile?! Wakaambiwa alijiua! Du wakachoka!
Mazishi yakaisha kila mtu akatawanyika, kabla ya kiza kuingia Manoa akaja, akasimama kwenye kaburi wee baadae akapiga magoti akawa anaongea, analia, ana mourn, mara akaskia mtu anamshika begani, kuangalia ni Maringo! Maringo hakujua kwanini aliombwa apelekwe pale baada ya mazishi, kweli baba atakuwa alimpenda sana Kungwi mpaka kuja kwa spare time yake, akambembeleza baba yake Manoa akaomba awe alone na kaburi!
Akalia weee mpaka uchungu ukaisha akaomba msamaha, akaomba Mungu akatukanaa kila kitu kikafanyika alipomaliza akapata amani moyoni, akaondoka! Njiani anapelekwa nyumbani akaanza kukohoa, kohoa na wewe Maringo akaona sio kawaida, akampeleka hospital, akawa anatapika damu, wakamlaza kumcheki, akapimwa akakuta na ukimwi na gonorea na kiswendo, Maringo akachoka hakujua kuwa baba yake ameathirika ikamfanya amhurumie zaidi!

Pendo akiwa nyumbani siku 1 baada ya mazishi akawa amelala akamwota mama yake anamwambia nisamehe mwanangu nimekuacha kwenye matatizo makubwa, nakupenda sana nipo pamoja na wewe kila uendapo, akaanza kulia, mumewe anamkuta analia akamwamsha, amsha na wewe ikabidi achukue maji ya baridi kwenye chupa amwekee kwenye paji la uso na shingoni, akafungua macho, kumbe amelala, akawa anainuka aende toilet, amesimama tu chupa ya uzazi ikapasuka, wakaamsha amsha popo mpaka hospital, baada ya masaa 8 Pendo akajifungua mtoto wa kike na kiume, Akafurahi, mapacha wa kike na kiume Joseph akafurahi baada ya msiba ni aibu! Baada ya kilio ni furaha, wakawapa majina watoto, wa kike akaitwa Rhoda jina la Kungwi, wa kiume akaitwa Andrew jina la baba yake Joseph!

Patric akawaza na kuwazua kuliko maelezo akaangalia bank ana hela nyingi akazionea imani zile hela akampigia Rasheeda akamwambia nipe bank akaunt yako akapewa unazo ngapi?! Akasema mbili akapewa akaenda kumwekea hela nyingi sana kwenye akaunt zote 2 mpaka bank wakashtuka wakamwita akasema amepewa zawadi na watoto wake wamemchangia, wakamwacha

Patric akampigia simu Maringo waonane akaja hotelin kwa Patric wakawa wanapanga na kupangua, mke wangu najua nimekuahidi nitakuoa lakini kuna shida imetokea kazini na wewe umeshajifungua ngoja tusubiri unalize uzazi, Maringo akaitikia tu sawa
Patric akamwambia nataka ufungue akaunt swiss bank nakuwekea hela zaki na mtoto, Maringo akakubali sawa. Patric akamwekea hela keenye bank yake ya Lusaka wakafungua saving ya mtoto wao junior wakaweka hela nyingi, baada ya wiki 3 Maringo akapata swiss akaunt no! Akawekewa hela nyiiingi sana na Patric, roho ya Patric ikatulia akijua sasa wake zangu wapo salama sasa ngoja nitubu mie! Akaondoka akaenda kwa boss wake Waziri, aka confess kiiila kitu kuwa waliiba kura kwenye ushindi wake. Boss akachoka akamwuliza unajua consequences za kuiba kura?! Ni jela maisha au ukibahatika ni nje kwa dhamana ila hauwezi kusafiri nje ya Zambia! Akajibu ndio mkuu!
Waziri akamwambia umefanya vizuri ngoja nitaonhea ma waziri mkuu tuone swala lako in a mean time usikimbie nchi wala kusafiri kwenda kokote kaa hapo hapo hotelini!! Patric kawa mdogo akajibu sawa
Waziri akafanya yake kwa waziri mkuu, Waziri akachoka sasa itakuwaje?! Wakawa wanaumiza kichwa wanawasiliana na mwanasheria mkuu wa mchi waone watawalindaje Ismail na Patric

Baada ya mwezi mmoja, Mrembo akiwa na mimba ya miezi 9 anasubiri muda wowowte chupaivunjike, akawa anatoka kazini akaenda super market, akafanya shopping yake pale akarudi kwenye gari kuweka vitu, item moja ikaanguka ikawa inapeperukia kwenda barabarani, ah Mrembo akafunga gari akawa anatembea mdogo mdogo kwenda kuiokota! Akainama kuokota mara gari likaja likamgonga puuu! Gari likakimbia, kumbe ni gari la majambazi linakimbizwa na polisi, majambazi wakamgonga Mrembo wakakimbia polisi wakaja wanakuta Mrembo anavuja damu kichwani na miguuni, wakamzoa zoa Mrembo mpaka hospital, madaktari wakamcheki hakuna cha Mrembo wala mtoto wote kushnehii!

ITAENDELEA SAA 2 USIKU
 
Duh, mtunzi mbona unaua watu? au ndo unataka kumaliza story kimwendokasi?

Hehe jaman nyie si mlikuwa mnalalamika watu wengi hamwelewi?! Basi ngoja niwapunguze au sio?!

Raha ya dafu ni dafu lenyewe si kama bakuli hupati ladhae

Meona ee

Duh saa mbili hiyo inakuja jamani

Dah poleni mabest me naumwa ivoo! Nitairusha baadae nikitoka hospital

duh naona mwisho unakaribia si kwa kufakufa uko

Huwezi jua huenda picha ndo linaanza!
 
Back
Top Bottom