Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 18,798
- 57,301
Part one
Najua haya maandishi tunayoandika humu yataishi na kusomwa humu hata baada ya sisi kuondoka Duniani miaka 50 ama 100 ijayo. Hivyo yanalengo la wengine waweze kujifunza.
Wewe Mwanaume, kama halijakutokea leo, basi kesho linaweza kukutokea maana kwa utafiti wangu mdogo, huu mchezo umeshamiri sana miongoni mwa Wanawake wengi miaka hii.
Binafsi lilinitokea miaka mingi iliyopita, kwa kuwa umri wangu umesogea sana, basi nitasema lilinitokea mwaka 47 😎
Iko hivi;
Niliingia kwenye mahusiano ya siri na mrembo mmoja miaka mingi iliyopita, nikiwa tayari kwenye Ndoa
Miaka ile kulikuwa na uhamasishaji wa upimaji wa HIV sana, kwani rate ya maambukizi ilikuwa kubwa, hivyo nami nilifanya mpango tukacheki afya kabla ya kuanza mahusiano
Baada ya miezi 6 hivi ya mahusiano ya siri, kuna siku kama nne mfululizo hivi mwenzangu alikuwa anaforce sana tuonane, of course tulikuwa tunaishi mikoa tofauti
Sikuwa tayari kuonana naye, hivyo nikamdanganya sikuwa na hela ya nauli hivyo ningependa anitembelee mwezi unaofuata
Ajabu alisafiri kwa nauli yake, akaja tukaonana
Baada ya wiki tatu hivi akanijulisha hazioni siku zake
Nilizipinga sana hizi taarifa, kwani tangu mwanzoni mwa mahusiano yetu, nilimweleza sitarajii kupata naye mtoto/watoto hivyo asiniletee habari zake.
Tukaingia kwenye mivutano then baadaye nikaamuru aitoe ile mimba, nikamtumia kiasi cha pesa ili aitoe
Alikula ile pesa na ujauzito hakutoa, kwahiyo ni kama aliamua kufanya kusudi (alikuwa na mipango yake na Ile mimba).
Mahusiano yaliendelea lakini sio kama awali, mivutano ilikuwa mingi na kisa kikiwa Ile mimba aliyobeba.
Wakati haya yanaendelea, nilikuwa nimempangia nyumba na by that time nilimlipia Kodi ya miezi 8 kwenye mji aliokuwa anaishi huku nikiendelea kumtumia hela ya matumizi
Yule Binti aliamua kutumia mimba yake kuni-blackmail, kwamba atafanya kila mbinu hadi Bibi yenu ajue kwamba ana ujauzito wangu.
Hivyo nikawa naendelea kumtunza huku napanga mipango ya kumchomoa Ile mimba kimya kimya, lakini bila mafanikio
Miezi 9 sio mingi, akajifungua mtoto wa kiume mweupe hatari, wakati huo Mimi Baba wa Mchongo ni mweusi kama lami.
Nikasafiri kwenda kuwaona Mama na huyo mtoto nikimbebea zawadi lukuki
Baada ya kumwona mtoto, ugomvi ukaanza upya, nikamwambia huyu mtoto amtafute Baba yake Mzazi sio Mimi
Mtoto hafanani na yeyote upande wetu, nimemkagua mara mbili mbili alama zetu, hana hata moja
Yaani nimekaa pale lakini akili hainipi kabisa, kichwa kinawaza hili mara lile...
Nikiwa nimepanga safari kurudi kwa Bibi yenu kesho yake, jioni moja aliniomba atoke kwaajili ya mazoezi mepesi hivyo Mimi nilibaki pale nyumbani na yule mtoto....
Mungu sio Athumani, wakati nipo pale nyumbani wakati napekua rimoti ya TV kwenye droo ya Meza na mtoto amelala kwenye sofa si nikakuta bahasha ya A4 ndani ikiwa na bahasha nyingine ndogo nne
Kukagua zile bahasha, nikakuta zina makadi ya Kliniki yenye majina ya yule mtoto tofauti kwa Baba wengine manne.
Kumbe mtoto ana Baba wengine wanne, Mimi nakuwa watano 🙌
Itaendelea sehemu ya Pili
Part Two: My Confession: Nilivyohudumia Mimba iliyokuwa na Baba 5 pasipo Kujuana