JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Wakati dunia ikiendelea kupambana kudhibiti mlipuko wa CoronaVirus, Tanzania imetangaza kuendelea kwa shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii.
Hii inapelekea Watanzania kulazimika kutafta namna ya kuishi na gonjwa hili miongoni mwetu huku tukiendelea kutimiza majukumu.
Katika mchakato huu, inawezekana kuna watakaopata maambukizi. Hili si mwisho wa maisha, taratibu za kujikinga zinazoshauriwa na Wataalamu wa Afya zifuatwe.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kulingana na hali yako
(a) Kwa Mtu anayeumwa/ anayeonesha dalili| Muathirika
Endapo una dalili zinazoashiria umepata maambukizi
Hii inapelekea Watanzania kulazimika kutafta namna ya kuishi na gonjwa hili miongoni mwetu huku tukiendelea kutimiza majukumu.
Katika mchakato huu, inawezekana kuna watakaopata maambukizi. Hili si mwisho wa maisha, taratibu za kujikinga zinazoshauriwa na Wataalamu wa Afya zifuatwe.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kulingana na hali yako
(a) Kwa Mtu anayeumwa/ anayeonesha dalili| Muathirika
Endapo una dalili zinazoashiria umepata maambukizi
- Piga namba 199 au fika kituo cha afya cha karibu nawe kwaajili ya matibabu – ni muhimu kufika kituo cha afya endapo unahisi unadalili za Ugonjwa wa Corona ili kuthibitisha na kupata tiba sahihi. Hakikisha hauwaweki watu wengine hatarini uendapo kituo cha afya.
- Zingatia kanuni za kujitenga na watu hadi utakapothibitika umepona kabisa ili kuepusha kusambaa kwa ugonjwa kwa watu wengi zaidi (Wanaokuzunguka)
- Fuata ushauri wa kidaktari – endapo utathibitika kuwa na Virusi vya Corona ni muhimu kufuata ushauri wa Wataalam
- Zingatia kula matunda na vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi
- Jitahidi kufanya mazoezi
- Kutakasa kila anachokishika – unapaswa kutakasa kila utakachokishika ili kusaidia kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo
- Vaa barakoa na gloves muda wote endapo unaugulia nyumbani ili kuwalinda wanaokuzunguka. Virusi vya Corona vinasambaa kwa vitone vinavyotokana na kukohoa, kupiga chafya ,mafua, kuongea na pumzi. Unapaswa kuvaa barakoa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu.
- Kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka au kutumia kitakasa mikono
- Kuepuka kushikana mikono au kugusana/kukumbatiana na watu
- Kuepuka mikusanyiko na kutoka nyumbani pale inapokua na umuhimu sana
- Kuvaa Barakoa kila utokapo nyumbani
- Kufuatilia taarifa na kufuata ushauri wa kiafya unaotolewa na wataalam
- Kwa yule aliyeumwa na kupona anapaswa kuwaelimisha wengine juu ya dalili za ugonjwa na namna ya kujikinga
- Kuepuka kugusa macho, uso , pua na mdomo
- Kula matunda na aina za vyakula vyenye vitamin C
- Kuongeza umakini na kuzingatia taratibu unapoenda sehemu za umma kama sehemu za starehe, saluni, benki na matamasha mbalimbali
- Unashauriwa kufanya manunuzi na malipo kwa njia ya kidigitali mfano, Lipa kwa M-Pesa, Tigopesa.
- Hakikisha unachangamana na watu unaojua mfumo wao wa maisha na kuhakikisha wanafuata taratibu za kujikinga
- Kufanya Mazoezi
- Kuosha au kutakasa vitu unavyonunua kabla ya kuvitumia au kuvihifadhi ndani