mwongozo wa speakeri-upitishaji wa bajeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mwongozo wa speakeri-upitishaji wa bajeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njowepo, Jul 8, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi jamani unakuta cdm kama akina lissu,mnyika,zitto etc bungeni wanaongea mambo ya maana na kufikia kutoa shilingi hatiamae mwenyekiti anaishia kusema tupige kura.Wabunge wanajibu ndio au sio hii imekaaje hamna means ya kupiga kura za siri labda electronically unabofya mahara speaker anapata votes kuliko haya ya bora liende na kuishia kusemaa ndiooooo au hapana!Hii itaweza kupunguza kusema ndio kwa mkumbo but individual accountability na committment on the notion of uzalendo wa nchi na sio kushabikia chamaAm sure something can be done on thisImenikera sana hasa bunge la leo jioni na la juzi on rada hasa makamanda lissu na mnyika walipokuwa wanaongea Nawakilisha!
   
 2. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Naungana na wewe, kwa kweli inakatisha tamaa, hebu fikiri mtu anakuja na mchango mzuri, lakini kulingana na tofauti za Kichama mchango wake unashindwa kupita kutokana na hizi kura za ndiyo na siyo. navyoona uendeshaji wa namna hii hauko realistic kabisa, sitofautishi na udikteta, halafu bila aibu Naibu spika anapitisha fagio bila aibu. Tunaiangamiza nchi kwa ushabiki usio na tija, kama kuna uwezekano wabunge wa upinzani nawaomba waikane hali hii mapema, la sivyo wataendelea kuburuzwa hivyo hivyo mpaka mwisho.
   
 3. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Akili ni nywele...
  Ila naibu spika ana kipara.
  Spika anavaa wigi.
  'Hii nafikiri inaenda bila kusema'
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa kasumba ya 'chama kushika hatamu' wabunge wa ccm wanatumia wingi wao bungeni kupitisha bajeti yenye utata. Marekebesho mengi yanayoletwa na CHADEMA ni ya msingi na yanauzika kwa wananchi lakini wao wanakataa bila hata ya kutafakari madhara ya hatua zao. Matokeo yake CCM watapitisha bajeti ambayo itakuwa haiuziki huku uraiani. Na CHADEMA watakuwa na mtaji huku mtaani.

  Ukishakuwa na mpango, mswada, bajeti inayokoselewa na walengwa halisi (yaani wananchi) basi kaa mkao wa kufeli, only this time, wa kufeli atakuwa serikali ya ccm. Na wabunge wake watakuwa wamechangia kufeli kwa serikali yao maana walipitisha bajeti iliyojaa makosa.

  Thinking ndani ya ccm think tank (kama ipo) inabidi wafanye uchambuzi juu ya madhara ya wabunge wao kusema ndio kwa kila kitu.
   
 5. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  mi nna uhakika, kama kura za siri zingekuwa zinapigwa bungeni basi hoja nyingi za upinzani zingekuwa zinapita kwa kishindo....wana ccm wengi wanajibu ndioooo kwa kuogopa wa pemben yake asimsikie akipinga ila moyon mwao wajua hali halisi.
   
 6. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,014
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli wangekua wanajua hawa wanamagamba wangebadilika. Jion hii nilikua mitaa fulani naangalia Bunge wananchi walishikwa na hasira walitamani hata kuivuja ile TV. kwa kweli Ndioooo zao zinazizidi kuwapa mtaji CHADEMA kwa wananchi. nakumbuka Lissu kasema natoa shilingi for the records. Hiyo records watakuja kuinadi kwa wananchi na ni mtaji tosha kabisa. Haingii akilini kabisa unatenga bilion 3 kujenga ofisi temporaly ya Makamu wa Raisi Dar then kwenye mazingira unaweka milion 400 harafu bado mtu anashabikia Ndiyoooooo!
  Nimependa mheshimiwa SITTA alivyotolewa umaana na mnyika hadi akawa mdogo kama piliton
   
Loading...