#COVID19 Mwongozo wa Serikali kwa Vituo vya Polisi, Magereza na Mahakama kukabiliana na UVIKO

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,583
6,633
Vituo vya Polisi vitatakiwa kufanya yafuatayo: -

1) Kuweka maeneo ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni

2) Watumishi na watu wote wanaoingia katika vituo vya polisi wavae barakoa muda wote.

3) Kutoa kipaumbele cha dhamana kwa Mahabusu wenye makosa yanayodhaminika kisheria ili kupunguza msongamano.

4) Kufanya kipimo cha haraka cha UVIKO -19 kwa mahabusu wote wanaofikishwa gerezani kwa mara ya kwanza.

5) Kuwapima joto la mwili watu wote kabla ya kuingia kituoni na chumba cha Mahabusu.

6) Kuruhusu ndugu mmoja tu kumtembelea mfungwa, kumuona mahabusu katika siku iliyotengwa na kuhakikisha wafungwa na ndugu wote wanavaa barakoa na wanakuwa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu.

7) Wasikilizaji wa kesi mahakamani wazingatie kuvaa barakoa na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu
 
Back
Top Bottom