Mwongozo kuhusu maboresho ya elimu ...

Mwongozo kuhusu maboresho ya elimu ...

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Nimefuatilia tafiti nyingi zinaonesha kwamba vikwazo vingi katika sekta ya elimu husababishwa na mambo yafuatayo:-
1) Umaskini
2) Kupata mimba
3) Mila na desturi
4) Upendeleo wa kijinsia katika kuelimisha watoto
5) Umbali kutoka shule na makazi
6) Ndoa za utotoni
7) Ujinga na kutojali
8) Shughuli za uchumi (kilimo, uvuvi, migodi n.k)
9) Mabadiliko katika makuzi
10) Mazingira.
Changamoto namba 2 na 8 ndo zinaongoza kwa kusababisha watoto wengi kutomaliza masomo yao (primary au secondary). Wazazi wana mwamko mkubwa sana kupambana na changamoto hizi lakini wenye uelewa wa kuwaelekeza hawafanyi hivyo..
Na hata ikitokea ukajitoa mhanga kufuatilia .. waliopewa kazi hiyo wanaona kama unawaingilia kwenye majukumu yao. Nitoe mfano .. mbunge anajua vyema changamoto zilizoko kwenye jimbo lake .. lakini akisikia mtu anaenda kwenye jimbo lake kufuatilia masuala ambayo yeye (mbunge) ndiye alipaswa kuyasemea kwa kuwa ndiye mwakilishi wa wananchi hao ... anaanza kutengeneza vipingamizi.
Ni mwongozo upi unapaswa kufuata iwapo mtu yeyote atabaini changamoto za kielimu katika sehemu husika?
 
Back
Top Bottom