Mwongozo Chadema baada ya uchaguzi mdogo

Hivi wewe, umeshafanya tafiti za kina za HUJUMA ZA CCM KWENYE CHAGUZI NA UKAZIJUA KISAWASAWA NA KIUNDANI NA IMPACT ZAKE KWA CDM? au umefanikiwa tuu kuchambua kasoro za CDM???

Majimbo na viti vingine vya udiwani ambako Chadema wameshinda hujuma hizo hazikuwepo? Kama Chadema ilifanikiwa kuzima hujuma katika viti walivyovichukua kwa nini ishindikane hilo viti vingine ambavyo hawakuvichukua?

Chadema isimamishe watu wenye sifa ambao wanauzika kwa wapi kura amini Chadema itazoa viti vingi. Akina Samwel Sitta walishaliona hili waliposema Chadema hawana safu ya kutosha, ndio hapo. Kufanya jitihada kusimamisha watu wanaokubali ndio ushindi si wa kuokoteza wasio na ushindani.

Kumbuka kuwa kushindanisha watu kadhaa katika kutafuta mgombea wa kiti ndiko kupata anayefaa, lakini sehemu nyingi utakuta Chadema anajitokeza mmoja tu kama mbovu au mzuri, anauzika au hauziki ndiye ataakayepeperusha bendera ya chama dhidi ya vyama vingine. CCM wanao wengi na anayeibuka huwa amewazidi wenzake na hivyo kuuzika katika kampeni.

Pamoja na kuwa makini hujama katika chaguzi, lakini tusifikirie msingi wa ushindi CCM ni hujuma tu, la hasha, sifa ya mgombea inawasaidia zaidi.
 
Huyu mtoa mada au muongozo inaonekana hajui hata uongozi wa tawi ukoje. uongozi wa chadema wa chini unaazia kwenye misingi ngazi ya kitongoji na msingi moja una viongozi .18. sasa fanya hesabu vitongoji vya nchi mzima mara 18 tawi lina viozozi 12 fanya vijiji vyote nchi mara 12 kata ina zaidi ya viongozi 14 fanya kata zancinini mara 14 jimbo lina zaidi ya viongozi 15 fanya majimbo yote mara 15 haya kila kiongozi mpe posho ya 5,000/ utatakiwa kutoa kiasi gani. ndio maana nasema wewe mtoa mada hujui hata tawi.
 

Uchanganuzi wako umejengeka katika kuangalia pato la ruzuku tu kama ilivyo. Hii ni sawa nawe mshahara unaoupata uufanyie uchanuzi wa matumizi kama ulivyo bila kulifanyia kazi ya ziada pato lako ili kulirudufu liwe na mafao zaidi.

Chadema kama chama kikuu cha upinzania kinatakiwa kiwe na mbinu za:

  • Kujijenga kisiasa na kujitanua
  • kubuni miradi ya kiuchumi
  • kutumia ruzuku kama mtaji mojawapo wa kuendeshea miradi ya uzalishaji
  • Matumizi ya chama yangetakiwa yawe faida baada ya mzunguko wa pesa katika kuchuma nyingine
  • Kushirikiana na vyombo vya kimataifa katika kupata misaada ya kuboresha miradi ya maendelo ya chama kiuchumi na kisiasa.

NB: CCM haijajenga uchumi wake tokana na mapato ya


  1. [*=1]ada za uanachama tu
    [*=1]kujimilikisha mali za taifa kama majumba, viwanja vya michezo, vyombo vya habari tu
    [*=1]Kuhodhi viwanja na kuvijenga kwa kupangisha watu tu
    [*=1]CCM imepata misaada mingi kutoka nchi za kijamaa za Urusi na nchi nyingine za mahariki kujenga miradi ya uchumi kama:


  • [*=1]Ofisi Kuu Dodoma ni msaada kutoka nchi za Mashariki
    [*=1]Jengo la mikutano lililokuwa ilipo chuo kikuu Dodoma ilikuwa ni msaada toka nchi za kijamaa za mashariki
    [*=1]Jengo la makao madogo Lumumba walipewa

Chama kinatakiwa kuwa na wataalamu wa uchumi si kwa malengo ya kisiasa tu, bali pia kwa nia ya kukijenga chama kiuchumi. Kutegemea Ruzuku si vema kwani kutatokea muhula viti kupungua hapo shughuli za chama zitaendeshwaje?

Chama kinahitaji kuwa na malengo ya muda mfupi na mrefu katika kujenga kisiasa, kiuchumi na kimtandao.

Note:
Hakuna chama cha siasa kilichoimarika bila kusaidiwa
 

Nimeleta mapendekezo au maoni yangu, kuna ambayo wachangiaji wataona yanafaa au la, lakini jambo la msingi chama kiwe na malengo ya kuwapa pasho watumishi wake, na kama pato halitoshi kuna umuhimu wa kubuni vyanzo vya kiuchumi ili chama kijitoe na ukata wa pato la matumizi yake. Rejea mchanganuo wangu kuhusu mapendekezo kuhusu namna inayotakiwa chama kujijenga kisiasa na kiuchumi katika bandiko #64 katika mada hii. Ina maana Chama kiwe na malengo ya muda mfupi na mrefu na pia kutafuta wahisani kimataifa kama CCM ilivyofanya ili kupata mitaji ya kuendeshea miradi ya kiuchumi kwa ajili ya kuendeshea chama.

Chama kuomba pesa na kuzitumia tu ni sawa na ombaomba ambaye anachokipata ni kula kisha kesho anarejea tena barabara kuomba. Chama kina wasomi wengi na wachumi wengi na wapenzi wengi nje na ndani ya nchi.

Mpango wa kununua Chopper
Nilisikia kama wana mpango wa kununua chopper, ni jambo zuri kwani chopper hizo zinapohitajika na chama kama katika kampeni na kusafirisha maofisa wake itakuwa ni ukombozi. Lakini chopper hizo zinaweza kuwa pia vitega uchumi katika nchi hii katika nyanja za kibiashara na utalii jambo ambalo litakisaidia chama kiuchumi kukua zaidi badala ya kuwa tegemezi.​

Huwa nafurahi kama chama kinaomba misaada ya kuweka vitega uchumi badala ya pesa ya matumizi ambayo ni utumwa wa kurudia kuomba tena kesho.
 

Binafsi nimevutiwa na mwono huo, huenda wengine wakaona isovyo kwa sababu tunapendelea kusifiwa tu na kuonyesha na madhafu tunaona kero fulani kwa watu wa uchambuzi wa aina hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…