Hiyo ni moja ya Nukuu maarufu za Baba wa Taifa ,Hayati Mwl.Julius K.Nyerere miaka ya 1995 wakati harakati za kuzima vuguvugu la " Tanganyika na G55" alipoutaka Uongozi wa chama wa wakati huo kutangaza Rasmi kwam Umma wa Watanzania kwamba Tanganyika Sio Sera ya Chama Cha Mapinguzi . Msingi wa hoja hii ya Mwalimu ndio ya SIRI kubwa sana ambayo Watanzania hawaijui kuhusiana na Muundo wa Muungano wetu,nina imani Waasisi wa Taifa hili na Wazee wangu ,nawaheshimu sana, wanaijua SIRI hii kuu ambayo ndio chimbuko ya mvutano mkubwa sana wa Kisiasa unaoligawa Taifa Letu.
Kwanini Tanganyika Sio Sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)?
Tanzania ni ni matokeo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Nchi hizi mbili zilikuwa na Vyama viwili vya Siasa,Tanganyika – TANU na Zanzibar – ASP. Ukweli ni kwamba, vyama hivi viwili kutoka kwenye Mataifa mawili tofauti vilikuwa na Itikadi na Sera tofauti na swala hili lilidumu kwa takribani miaka 12 na zaidi.Huu ulikuwa ni muungano wa DOLA .
Kwa busara za waasisi wa Muungano Muungano, manamo mwaka 1977 wakaona ili kujenga Muungano ulio Imara na dhabiti ni vyema kuunganisha vyama hivyo (TANU na ASP) ili kuunda CHAMA Kimoja ambacho kitaungana na DOLA (Tanzania) kushika hatamu za uongozi, ndipo CCM kikazaliwa. Sasa basi kwa maana hiyo muhimili wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Muungano wa TANU na ASP, nje ya Muungano huo hakuna CCM, bali kuna TANU- Tanganyika na ASP –Zanzibar. Nadhani hapo kila mtu anayesoma hii thread ameleewa ni kwanini Mwalimu alisema Tanganyika Sio Sera ya CCM.
Kwa Mantiki hiyo, Muundo wa Serikali Tatu ukipitishwa una maana kwamba,Zanzibar ambao Tayari wana Katiba yao wenyewe wataondoka na ASP na Tanganyika watalazimika kuandika Katiba mpya (ya Tanganyika) na kubaki na chama chao cha TANU na huo ndio utakuwa mwisho wa CCM! Mtu mwenye akili na anayefirkiri sawa sawa atakuwa anaelewa dhima ya Mwl. Nyerere kuunganisha TANU na ASP mwa 1977, ilikuwa ni Kujenga na kuuimarisha Muungano wa mwaka 1964 ili kujenga Taifa imara kabisa ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka 50 sasa.Kwa maana hiyo, Serikali TATU ni kuvunja Muungano wa TANU na ASP ambao ulizaa CCM ambayo ndiyo Muhimili wa DOLA.
Tunaomba Waasisi wa TANU na ASP waliopo watumabie nini ilikuwa Sera za ASP na zipi zilikuwa Sera za TANU ambazo ziliunganishwa na kuunda CCM ambayo inashika DOLA ambayo ni Muungano wa Tanganyika –TANU na Zanzibar –ASP.
Kwa maoni yangu,bila kuulewa huu Muungano wa DOLA Na CHAMA natutaweza kujenga hoja ya kuunda Serikali Tatu nchini ya Mwamvuli wa CCM, kuunda Serikali tatu maana yake CCM haipo tena.!!!!Mwalimu Nyerere alionya Jambo hili mapema kwakuwa alijua kuvunjwa kwa Muungano huu utakuwa ndio mwisho wa Chama Cha Mapinduzi.
Hakuna mwana CCM atakayeunga Mkono Serikali TATU hata iweje, kwa maoni yangu na kama yupo AFUKUZWE mara moja kwenye chama maana hiyo siyo sera ya Chama chake.
Nakaribisha Mjadala