Mwl Nyerere anaheshimika sana Duniani kote

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,566
8,613
Kwa kumheshimu Mwl Julius Nyerere nchi ya Guinea iliamua kukiita chuo kikuu cha nchi hiyo jina la Rais wa awamu ya kwanza Tanzania.

Mimi nilikua sijui niliambiwa na rafiki yangu wa Guinea niliyekutana naye hapa ughaibuni.

Nilivyo mweleza kwamba natokea Tanzania alinipokea kwa ukarimu mkubwa sana kitu kilicho pelekea urafiki wetu uzidi kushamiri kupitia kiongozi huyu.

Hiki ndio chuo kikuu kikubwa nchini Guinea kilicho anzishwa mwaka 1968.

Julius Nyerere University of Kankan

Julius Nyerere University of Kankan (UJNK), also known as Université de Kankan is a university in Kankan, Guinea. It is named after Julius Nyerere, the first President of Tanzania.
Julius Nyerere University of Kankan
Université Julius Nyerere de Kankan
Established1968
LocationKankan
,
Guinea
Websitewww.ujnk.org
 
Mwalimu Nyerere alijiheshimu yeye binafsi, aliheshimu wasaidizi wake na kubwa zaidi aliheshimu wananchi wake. Mwalimu hakua na double standards (angalau ya waziwazi) katika kuendesha mambo ya nchi

Mwalimu alikua na upeo mkubwa sana wa masuala mbalimbali japo hakua na Shahada ya Uzamivu. Alikua mpenda mijadala na mwenye kusikiliza. Mwalimu aliichukia rushwa in the real sense of the word na wala sio ile ya "yule mushike yule muruke".

Mwalimu alikua na lugha za staha kwa watu wote ikiwemo wanawake na kamwe hakupata kutoa lugha za kuudhi na kudhalilisha utu wa mtu. Nakumbuka aliwahi kumfuta kazi John Malecela aliyekua Waziri wa Uchukuzi pale alipotoa kauli kuwaambia abiria waliokua wanasubiria usafiri wa treni "Anayesema kuna tatizo la usafiri wa tren nchi hii nawaambia they should go to hell". Mwalimu alimshusha cheo na hakupanda zaidi ya ukuu wa Wilaya hadi pale Mzee Mwinyi alipokuja kumkumbuka na kumteua Mkuu wa Mkoa, Balozi wetu London na kisha Waziri Mkuu

Mwalimu aliheshimika kimataifa kwa sababu alikua mtu wa kimataifa. Alipenda umoja na uhuru wa Afrika akisaidia nchi na Vyama vilivyokua vinapigania uhuru sehemu yotote ulimwenguni hasa Afrika. Alikua akipinga ubeberu sio dhidi ya Tanzania pekee bali dhidi ya wanyonge popote walipo duniani
 
Kitu nilichokifahamu baada ya kutembea huko duniani na mpaka leo najiuliza why ni kuwa nje ya Afrika tena ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara Nyerere hafahamiki kabisaaaa. Niliwahi kuwa China nikajaribu kudodosa kuhusu Nyerere yani hajulikani ila Tanzania wanaijua. Ukitaka kunielewa kwanini wanaijua Tanzania ni kuwa kila nilipokuwa nikitua viwanja vya ndege vya Beijing na Pudong lazima niwekwe lockup kwa muda nikiwa uhamiaji.
 
Kitu nilichokifahamu baada ya kutembea huko duniani na mpaka leo najiuliza why ni kuwa nje ya Afrika tena ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara Nyerere hafahamiki kabisaaaa. Niliwahi kuwa China nikajaribu kudodosa kuhusu Nyerere yani hajulikani ila Tanzania wanaijua. Ukitaka kunielewa kwanini wanaijua Tanzania ni kuwa kila nilipokuwa nikitua viwanja vya ndege vya Beijing na Pudong lazima niwekwe lockup kwa muda nikiwa uhamiaji.
Mkuu Sam, mataifa makubwa watu wake wakati mwingine wanakua na ignorance ya habari za nje ya nchi zao inayotokana na arrogance ya ukubwa wao. Maranyingi kujifunza habari na taarifa za vinchi masikini kama vyetu huwa ni nadra sana isipokua labda kujua kuna rasilimali gani ziko upande huu wa dunia ambapo wanaweza kuja "kuzichukua"

Ujinga huo upo kwa Wamarekani, Waaustralia, Warusi na mataifa kadhaa yenye uchumi mkubwa na yaliyoendelea
 
Dah yaani madai yako umeyatetea kwa mfano mmoja tu? Maana yake Guinea ni dunia yote au ni representative sample?ningekua mhadhiri ningekugonga F mapema sana.

Mzee wetu, Mungu amlaze mahali pema, anajulikana kwa vizazi vilivyokua kwenye harakati za kugombea uhuru. Alisimamia ukombozi wa nchi nyingi Africa na alikua na misimamo mikali kwa nchi za magharibi kuhusu ukoloni mamboleo na ubeberu.

Ila kwakua hakuwa malaika, anayo mapungufu,ila si vizuri kusema mapungufu ya marehemu.

Huyu ni icon ya taifa na ni baba wa taifa letu.
 
Back
Top Bottom