Mwizi Mzoefu Atobolewa Macho Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwizi Mzoefu Atobolewa Macho Yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Mar 11, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwizi mzoefu katika kituo cha magomeni mapipa ameambulia kisago cha nguvu na kutobolewa macho yake baada ya kukwapua hereni za dhahabu kutoka kwa abiria mmoja aliyekuwa kwenye daladala iliyokwama kwenye foleni.

  [​IMG]

  [​IMG]

  Kibaka huyu alinusurika kuuliwa baada ya wananchi kukimbia wakijua wameua lakini dakika kumi baadae kibaka aliamka na kuanza kuondoka zake.

  [​IMG]

  Source: Nifahamishe.com

  Redio mbao zilidai kibaka huyu anatumia dawa za kienyeji kujilinda asiuliwe


  mhh zipo kweli dawa kama hizo?
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Vibaka na wezi ni moja ya vitu vinavyo nikera sana bongo
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  BM21 Heshima yako!

  Suala la vibaka na wezi ni chachu tu ya mifumo mibovu ya ulinzi na Usalama wa raia, Tanzania. LM hupo hapo?
   
  Last edited: Mar 11, 2009
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Watanzania wapenda amani!!
   
 5. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Babuji!

  Picha yako inachezesha matumbo, lakini sielewi maana ya picha yako ni nini? Je unaonyesha unyama tulionao binadamu, au unaonyesha kushidwa kwa mkono wa sheria? Unajua picha zozote za kuumizana sio nzuri, zinaacha taswira mbaya kwenye kumbukumbu za binadamu, ama zinamfanya binadamu ahalalishe hukumu iliyotolea.

  Sipendi, wezi, lakini sipendi pia kuona damu zao zinazagaa. Ni kweli tunatatizo la usalama wa raia, lakini kuadhibiana mkononi sio sahihi!

  Wazo langu ni kila mtaa uwe na mti wa kusulubu. Mtu akikamatwa wizi, anapelekwa kwenye mti huo - halafu anakaa hapo kila mpita njia amuone na kumkebehi. Mwisho wa siku kalandinga la polisi lipite liwachukue - najua sio njia mathubuti lakini nimejaribu kufikiri... hebu na wewe toa suluhu yako.
   
 6. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hebu toa wazo lako vibaka wafanywe nini? kwa sababu hata kama akienda magereza baada ya majuma mawili ametoka na ataendelea na hako ka mchezo magereza yamejaa hakuna pa kuwaweka. Tena bora wangemchoma moto akafie mbali. Wle vijana pale Magomeni na Mwananyamala wanakea sana hata kama ukiwapa vipesa kidogo ndio utakuwa adui wao manake watajua unazo. Mi naonelea bora kuwachoma au kuwe na mtu kama JUDGE JUDY amalize hayo matatizo haraka haraka kuliko kuwapeleka Kisutu na Hakimu kuwaachia kwa sababu upelelezi wa Police haukuwa na ushahidi kumbe wanakula nao.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni jambo la kusikitisha jamii yetu ilipofikia, inatia simanzi mno..
   
 8. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Judge Judy, ni mfano mzuri, lakini unahitaji jamii ambayo inaweza kujikamatisha - na kivutio cha washtakiwa kujipeleka na watu kupeleka kesi zao. Watu wanaoenda kwa Judge Judy, sio wa mtaa tu, wanamahusiano ya kijamii yanayotambulika, wanakwenda pale kushtakiana wakati wanajuana. Sasa kibaka wa kariakoo, au magomeni itakuwa ngumu kweli kumpeleka pale, maana pa kulala hana na akitoka kesho yake harudi. Marekani utarudi tu, maana rekodi zako zinajulikana. Pili, uasilia wa sheria wa marekani na tabia za wananchi wake ni tofauti na za kwetu tofauti kabisa. Tabia zao zinalazamishwa kufuata mkondo wa sheria. Kwa mfano, kuliko mtu apelekwe mahakamani ambako gharama kibao na unaingia kwenye kumbukumbu za serikali, anaona ni bora aende kwenye mahakama za kijamii. Hata sisi tulikuwa nazo hizo, na bado zipo kwenye vijiji. Na sikuhizi wameweka mabaraza ya kata hata mijini yapo, je wanaweza kupiga mchakamchaka na vibaka? Wapi pameporomoka hatuwezi kujilinda?
   
 9. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #9
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Mwinyi amepigwa kofi jana. Kulikuwa na conspiracy ya kutaka kuzuia hizo habari zisitangzwe kabisa. Clouds Radio 88.4fm inayotangaza Kurunzi kila jioni saa kumi na nusu,imesema tu habari katika Alasiri na Dar Leo,zimetuacha mdomo wazi. Radio Free Africa inatangaza habari kila jioni,saa 11,lakini jana hawakuzitangaza hizi habari. Kwa hiyo hizi habari zimetoka kwa ajlil tu the main stream newspapers could not be muzzled.
  Kwa hiyo hakuna ubaya kwa nifahamishe.com kuzitangaza hizi habari za huyu kibaka. Huyu kibaka amefanya mkosa,kwa sababu kuong'oa heleni toka sikioni ni ukatili. Lakini na watu pia wamefanya ukatili sana. Hawa watu vibaka hawana elimu. Hakuna kitu chochote kinachofanyika kuwaelimisha. Mawaziri wanaotakiwa kuwasaidia,wanafanya mapenzi ndani ya gari Masaki.
  Hili jambo linanisikitisha sana,Magazeti yanayo mambo mengi sana ya kuandika,yaliyosemwa na Mtikila,na Zitto, na hawa watu wengine wengi,maneno ambayo hayamsaidii mtu yoyote kitu chochote. Watu wengine hawapati nafasi ya kuonekana katka haya magzeti,mpaka labda wamuue albino, ndio habari zao zinatangazwa katika gazeti.
   
 10. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Katika uchumi tunaita '' is a forced income distribution'' hivyo ni ishara kuwa kuna matabaka ya wenye nacho na wasionacho. Mbaya zaidi hakuna unemployment benefit. Tabu tupu
   
 11. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duuh,I know this guy.hakuuwawa kwa sababu kwao ni hapo hapo.
  Anapokuwa anapita pembeni mwa magari yaliyo kwenye foleni utafikiri ni muungwana,nisikilize speed anayokata Chain,heleni au simu.Halafuhuwa anamalizia kwa kucheka.Haya sasa wakadaiane na huyo mganga wake amrudishe mimacho ya kuibia.
  Angekuwa Mwananyamala,wao wanamaliziaga kwa kutoa viungo,haijalishi ni Albino au mweusi.
   
 12. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  vibaka wangewatengenezewa kama ka shade wafungiwe huko wafundishwe kutengeneza vitu mbali mbali wakitoka hapo, NGOs au taasis za fedha wawape kianzio cha fedha uone kama wataiba tena. They are forced to still kwa sababu hana income ya aina yoyoe. HIvi unajua kujitoa muhanga kuiba hadharani needs courage?

  Inauma sana imagine huyo umemtoboa macho ndiyo mwisho wa story.
   
 13. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ni kitu ambacho tunakiona kila siku lakini kwa kusema ukweli hatukai chini kukifiria hata mara moja,tunaishia kusema ''saizi yake''.mi nafikiri kuwa swala hili la kuuliwa kwa vibaka ni kubwa sana kuliko tunavyolichukulia.tumekuwa wepesi sana tukisikia tu mtu kaitwa mwizi basi kinachofuata ni kutafuta wapi mawe,wapi petroli na wapi kibiriti.mara nyingi tunafanya hivi bila hata kujua hasa ni kitu gani kibaya huyu kaiba,lakini tunaingia kwenye sulubu yake na baadae ndo tunakuja kusema,''..aaaah!kumbe aliiba hareni!''.ni swala nyeti sana ambalo kwa kweli ufumbuzi wake ni vigumu kuupata.kama alivyosema bwana mmoja hapo juu,magereza yamejaa labda na mahakimu kwa kujua hilo ndo maana kila siku tunaona vibaka wanaachiwa huru bila adhabu yoyote.
  sasa hili swala la kutoa adhabu kwa vibaka,sijui linatueleza vipi sisi kama Taifa!(and what does it say about us as PEOPLE,as a SOCIETY!)tunajionaje sisi wenyewe,kwamba thamani ya maisha ya mtu ni ndogo sana,hatusiti kutoa maisha ya mtu kwa sababu tu tumesikia kakwapua kitu fulani.NINI KIFANYIKE BADALA YAKE?kwa kweli ni vigumu kusema kwani hakuna jibu la haraka haraka,lakini mi nna wasiwasi kuwa kwa namna hii tunakoelekea sio kuzuri.wakati wa mauaji ya Rwanda tulikuwa tunashangaa kuwa ni vipi binadamu anaweza kugeuka kuwa mnyama kiasi hiki,lakini je ni nini tofauti ambacho nasi twakifanya?mara ngapi tumeona mtu kupoteza maisha tena kwa ukatili wa hali juu kwa sababu kakwapua kitu fulani?na yote haya yanafanyika mbele ya macho ya watoto wadogo.TUNAJENGA UTAMADUNI AMBAO KESHO TUTAKUJA KUTAFUTANA MCHAWI NA TUSIMPATE.na kwa bahati mbaya sana viongozi wetu sidhani kama wanona kuwa hili ni tatizo,na hii inajionyesha kama ukiangalaia kwa mfano kwa kauli aliyotoa Waz.Mkuu wakati fulani kuhusiana na swala la mauaji ya wenzetu maalbino.alipobanwa badala ya kurekebisha kauli yake akiwa kama Kiongozi wa Serikali aliishia kutoa machozi na kusema kuwa alipatwa na uchungu sana kutokana na ushuhuda alioupata kuhusiana na mauaji haya.tujiulize kwa kweli tunakokwenda hivi NDIKO?.......
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Inasikitisha, both ways! hiyo picha inatisha na haifurahishi kuona binadamu mwenzetu kafanyiwa hivyo. Upande wa pili, hawa jamaa wakikutime pia wana uwezo wa kuondoa uhai wako. Vyombo vyetu vya ulinzi viwe macho, lakini kubwa zaidi ni kuimarishwa kwa uchumi ambao walau unaweza kuwategemeza asilimia kubwa ya watu!
   
Loading...