Mwito kwa watanzania wote

Mwito kwa watanzania wote

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
887
Reaction score
664
Hawa watu wa mitandao tumewatajilisha sana, Kiasi ambacho Tanzania ni Nchi inayoongoza katika Africa ya Mashariki katika matumizi ya simu, leo wanatugeuka, kodi ambayo wanatakiwa walipe kutoka katika lifaida likubwa wanalopata wametutwisha sisi kweli!!!
Naomba nitoe mwito kwenu wote baada ya kutumia Tsh1000 kwa siku kwa simu tupumguze tutumie 300/- tu, tupige simu za maana tu zile za Mpenzi nakumiso, kuku hawajambo Ngombe wamekamuliwa tuachane nazo, ili na wao waone umuhimu wetu.
Haya mapesa wanayomwaga kwa matangazo yasiyo na maana ambayo kila siku wanabadilisha yakekuwa kelo na uchafu katika miji yetu wayapunguze walipie kodi kwa maendeleo ya Taifa.
Wateja wa simu Nchini wanakadiliwa kuwa millioni 25 kwa bilioni 160 wanazotakiwa kulipa kwa mwaka kama kodi watatuchanja kila mtu Tsh 33 kwa kila 1000 na kwa wastani Mtanzania anatumia zaidi ya Tsh 1000 kwa siku. watamaliza kodi hiyo kwa siku 182 vipi makato watakayoyafanya kwa siku nyingine 183 za mwaka, hawa ni wezi. Serikali tusaidieni waache visingizio. Nawasilisha.
 
Hiki ulichokiwasilisha hakina tofauti na kumwambia mtu aache kutumia jiko la umeme,jokofu hasichome nyama kwa Oven kisa tu tannesco wameongeza gharama kwa kufanya hivyo hauwakomoi wao bali unajikomoa mwenyewe kwa kujinyima uhuru cha muhimu hapa ni kutafuta mbinu ya kuifanya serikali itambue kilio hiki.
 
Ni wazi hukufuatilia bajeti ya magamba...ni kwamba sirikali imeamua kuanzisha kodi hiyo ya sh.1000 kwa mwezi kwa kila kadi inayotumika na itakatwa na makampuni moja kwa moja ktk line zetu na si makampuni yanabeba hiyo pesa bali ni magamba yetu hay..........usiwalaumu watu wa makampuni japo ni wazi kuwa tunaumia sana.asante.
 
eee bhana umenistua , kwa hiyo matumizi yangu ya siku yasizidi jero siyo ! Vipi kwa wale wanaotumia kabaang ?
 
Hiki ulichokiwasilisha hakina tofauti na kumwambia mtu aache kutumia jiko la umeme,jokofu hasichome nyama kwa Oven kisa tu tannesco wameongeza gharama kwa kufanya hivyo hauwakomoi wao bali unajikomoa mwenyewe kwa kujinyima uhuru cha muhimu hapa ni kutafuta mbinu ya kuifanya serikali itambue kilio hiki.

Mkuu, hata bila kuambiwa ni kwamba ataacha kutumia jiko la umeme na kurudi kwenye mkaa kwa kushindwa kulimudu na wala siyo kwa kupenda. Kuna baadhi ya watu ambao majiko yao ya umeme yako stoo na wala siyo kwa kupenda. Hata hizi cm wako ambao watapunguza mitandao au wengine kuachana nazo. Unafahamu ni Watz wangapi wanaishi kwenye abject poverty halafu leo uwape kodi ya cm?
 
Hapana,ebu tulipe hizo kodi,ni muhimu hata kwa ajili ya corporate social responsibility
 
Mgomo wa jumla kwa saa 24/36 watumiaji simu ni pigo la aina yake kwa serikali,makampuni na washenzi wengine!mpo tayari?maana ninyi wenzangu malalamiko bila kitendo si uungwana!
 
Bia wanaongeza kila mwaka na bado mnakunywa.wameongeza kwenye simu imekuwa nongwa.huku tukubali tu imekula kwetu we weka jero yako wanachukua ukiweka tena wanachukua hadi ifike hela yao ndo unakuwa huru.kumbuka unaweza susa hata mwezi siku unataka kuwasiliana ndio utajuta.kama umekwepa miezi mitatu we weka kabisa zaidi ya buku tatu zao ili itakayobaki ndio utumie kuwasiliana.inauma lakini ndio kweli yenyewe hiyo.
 
Hasira zetu sote tuzielekeze magambani,ndo wamekosa fikra sahihi za namna bora ya kutengeneza wigo wa vyanzo vya kodi bila kumdhuru na kumdhalilisha mtumiaji haswa hohehahe mtu wa chini."smtm ninahisi CCM ni DHAMBI".
 
Mkuu, hata bila kuambiwa ni kwamba ataacha kutumia jiko la umeme na kurudi kwenye mkaa kwa kushindwa kulimudu na wala siyo kwa kupenda. Kuna baadhi ya watu ambao majiko yao ya umeme yako stoo na wala siyo kwa kupenda. Hata hizi cm wako ambao watapunguza mitandao au wengine kuachana nazo. Unafahamu ni Watz wangapi wanaishi kwenye abject poverty halafu leo uwape kodi ya cm?

Usiende mbali, Binafsi nilikuwa full kujiachia na majiko, Pasi na Taa usiku kucha enzi hizo uniti moja ni Tshs 54. Lakini tangu uniti moja imezidi Tshs 150 kwa sasa baba ni baadhi tu ya taa ndio zinawashwa tena kwa masaa machache. Pasi inawashwa kwa masharti na Jiko la umeme na vifaa vingine nimewaachia buibui nao wapate makazi. Mwendo mmoja kukimbizana na magunia ya mkaa kwa sasa. Kupandisha kila siku bei hizo za unit ni kuendelea kuamsha wizi wa umeme.
Kwa hali hii, ndio maana Sasa TANESCO mapato yamepungua na shirika linajiendesha kwa hasara.

Kwa sasa haya makampuni Acha waanzishe hizo kodi, Lakini kama ni wazalendo na wakweli wataleta takwimu hapa kuwa kila kampuni inaweza kupoteza hadi 20% ya wateja. Hao watumiaji 25milioni ni double counting, wengi wana laini kuanzia 2 na kuendelea. Hivyo watachagua baadhi tu line na zingine kutupwa.

Hizo za Minkabang, we angalia kuna shirika Tz lililojifanya ni Executive kama Aritel?. waliwacheka Tigo kuwa ni ya wanafunzi lakini na wao leo ofa kibao baada ya kuona hadi maprofesa walianza kuhamia tigo na mtandao kupoteza wateja.
 
walotutwisha ni mitandao au sererkali...? kwani serekali inashidwa kuwaambia walipe wao...?sijui kama utanielewa masawali yangu...? yaani kodi inafaidisha kampuni za simu au serekalai...?
 
Back
Top Bottom