Katafute ile Hotuba inayosadikika walitaka kumpindua akina kambona. Kusema sitaki kura zenu hiyo ndo deemokrasia ama ulitaka aseme je? kwamba kura zenu mnipe ila siongezi kipato chenu? Sahizi tulipofikia hizi kauli ndo zinatakiwa kwamba sifanyi hiki na kile na nitafanya hiki na kile sasa mpira unabaki kwako kusuka ama kunyoa.
Mkuu wangu unazungumza vitu ambavyo havifanani kabisa. Hotuba ya Nyerere kuhusu Mapinduzi ya kina Kambona yalihusu Mapinduzi na umwagaji damu na Nyerere aliwalenga wale waliotaka kupindua serikali yake. Hakuna sehemu hata moja alizungumzia kutohitaji kura za Wananchi wakulima au Wafanyakazi.
Pili, mimi nilikuwa Bongo wakati Kikwete akitoa hotuba ya kwanza akiwaomba wafanyakazi kutofanya mgomo... Hii ilikuwa kabla ya mei mosi. Ilikuwa makini na wengi wetu tulimuunga mkono na kuomba majadiliano yafanyike zaidi..Pia niliona mahojiano ya viongozi wa Tucta na star TV..Viongozi hawa walisema kwamba vikao vingi vimekwisha fanyika toka 2008 na hakuna muafaka wowote uliokwisha fikiwa wala hakuna dalili ya kuwepo makubaliano.
Nakumbuka mtangazaji mmoja aliwauliza kama huo haukua wakati mzuri kutokana na uchaguzi kuwepo karibu. Wakamjibu kwamba hakuna wakatimzuri wa kuipa pressure serikali kama wakati huu kwani wamekuwa wakizungushwa pasipo serikali kuzingatia hali ngumu ya maisha ya wafanyakazi ambayo inazidisha rushwa maofisini. Hili halina Ubishi iwe kwa mtazamo wowote ule, rushwa nchini limekithiri kutokana na mishahara midogo na kwa mtaji huo hatuwezi kuendelea hata kidogo.
Katika mazungumzo yaliyofuata rais mwenyewe hakuchukua hatua yoyote kujihusisha na mazungumzo yaliyofuatia. Tatizo la Kikwete ni ufuatiliaji wa maswala magumu..Hana muda wala hajali zaidi ya kuhudhuria sherehe na mazishi - Uswahili mtupu. sasa ilipofikia mei mosi na kutangazwa kwamba viongozi wote hawataalikwa shehere hizo, mzee wa kaya aka mind, na hata aliposikia tena mgomo aka panic na kutoa hotuba ya kijeuri pasipo kufikiria..
Hotuba ya Kikwete ya majuzi na hasa ule mfano wa Mbayuwayu ina maana wananchi na hasa Wafanyakazi hawana AKILI isipokuwa za kushikiwa. Na kibaya zaidi aliwataka wafanyakazi wafikirie zaidi kukosa Ajira zao namaisha yao baada ya mgomo kuliko adha ya mishahara midogo.. Ni ujeuri mkubwa sana inapofikia rais kuwatisha wananchi akitumia ajira na kwamba hawahitaji! atawafukuza kazi kwa kudai haki yao.. kimsingi huu ni Udikteta uliopitiliza..
Binafsi sikuamini na wala sitaki kuamini kwamba Kikwete alijiandaa kuyasema haya kwa wananchi..Nadhani hofu yake ya Upinzani toka ndani CCM ni moja ya hofu kubwa iliyomsukuma kuamiini kwamba Mgaya alitumwa na kuwa madai haya yalikuwa ya kisiasa sana badala ya Ukweli uliosimama. Kikwete hakufanya homeworkyake kujua hali halisi ya wafanyakazi napengine Ikulu kumejaa wasanii watupu ambao hawafanyi kazi zao ila kupiga majungu ya kutafuta mchawi kama ilivyo ktk vikao vya CCM...