Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,597
- 13,094
Wakuu heshima ziwe kwenu.
Huyu mwamba alikuwa mbunge wa upinzani . Aliyechaguliwa na kuaminiwa na watu wa jimboni mwake wakiwemo wale wa kanda maalumu ambao ni wengi jimboni humo.
Alichaguliwa kwa sababu watu waliamini kwenye mabadiliko ya kweli sio ya ki propaganda. Wapo walioumizwa, kufungwa na pengine kuuwawa kwa kulinda kura za mwita. Alishinda
Baada ya muda akautangazia umma kwamba anarejea nyumbani atii kuunga mkono juhudi. Wapo waliomsifia na kumpongeza hata kumpa unaibu waziri kama zawadi au kifuta jasho kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Ukisoma mitandaoni utaambiwa wabunge wa upinzani hawajaleta maendeleo majimbini hivyo hawafai hata kuitwa watanzania. aibu ya ubaguzi hii.
Nimekuwa nikipita jimboni kwa muunga mkono juhudi bwana Waitara.
Hali ya miundombinu jimboni humo inatia kinyaa. unashindwa kujua kwamba kweli hili ni jimbo lenye kupakana na uwanja wa ndege wenye mindege ya matrilion au nini.
Barabara zote ni mahandaki matupu kwanini hazitengenezwi wakati mbunge wake ameunga mkono juhudi?
Mwita umeshindwa Dar utaweza Tarime? Hutoshi