Mwisho wa yote mwenye busara ni mfalme

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,655
Kitu kibaya binadamu anachoweza kufanya ni kutumaini mambo mabaya kutokea kwa binadamu mwenzake, badala ya kumuombea kheri. Kwa kumuombea kheri na wewe pia unajiombea kheri. Kunasababu gani ya kunung'unika mwenzako anapofanikiwa ?

Hatuwezi kubaki wote sehemu tulipo ni lazima wengine watasonga mbele . Hatuwezi kuwa wote matajiri na hatuwezi kuwa wote maskini pia. Lakini kuna kitu kimoja ninakijua na kukiamini.

Maisha yetu wote yako mikononi mwa Mungu. Atupaye pumzi na mahitaji yetu ya kila siku. Atufanyaye tuweze kuendelea. Aliyetupa akili na mikono ya kufanya kazi na miguu ya kutembee huku na kule katika uso wa dunia kujitafutia. Ametupa macho ya kuona na moyo wa kupenda. Tunapenda wanawake wetu na tunapenda vitu tunavyozalisha kwa mikono yetu. Matumaini yetu yote yako mikononi mwa Mungu.

Kwa waliofanikiwa wanawajibu wa kuheshimu wengine na kuwaangalia wasionacho. Kwa njia hii tutafanya dunia yetu kuwa ya kupendeza.

Kuna uzuri ambao ni zaidi ya kila kitu. Ingawaje watu hawautambui lakini ni wenye thamani. Sio uzuri unaotokana na mavazi au kujiremba. Uzuri unaotoka ndani, ndani kabisa kwenye nafsi na roho ya binadamu.

Uzuri wa mawazo na uwezo wa akili wa kufikiri mawazo mazuri yasiyodhuru watu wengine na nafsi yako pia. Ingawaje watu wanahangaikia uzuri wa mavazi na kujiremba huu ni wa thamani mno. Pata huu kwanza na mwingine utafuata. Jenga vya ndani kisha jenga vya nje.

Fikiri mawazo mazuri na watakie mema wengine hiki ndicho ninachoweza kusema leo. Unaweza kusema ninayosema haya ndio ninayoyatenda? Mimi sio mkamilifu bado nahangaika kutafuta njia sahihi.

Lakini ninaweza kuona ninapoelekea na moyo wangu una matumaini nitafika huko. Ingawaje dunia imejaa mihangaiko mingi.

Unaweza kuwa mtu mwema watu wengine waka kukwaza na kukujaribu. Dunia imejaa mgongano wa mawazo na fikra.

Kwasababu kila mtu amepewa uwezo wa kufikiri kivyake na kuwa na mtizamo wake. Hatuko sawa katika busara. Kitu ninachoweza kusema tuvumiliane. Tunaweza kukwaruzana hapa na pale lakini mwisho wa siku tusameheane. Tukumbuke sisi sote ni binadamu.

Tuna kila aina ya watu katika dunia yetu ni lazima utambue na kuelewa. Kuna wabinafsi ambao wanajiangalia wao tu na hawafikirii kuhusu wengine. Kuna wagomvi, wezi na wenye hila. Vitu vyote hivi na tabia zote ni zao la fikra zetu. Ni jinsi tunavyotazama mambo. Na mtazamo wetu ndio unaongoza maisha yetu na kujenga aina ya maisha tuliyonayo. Kwahiyo kuwa mwangalifu na unachofikiri.

Ni muhimu kujua kwamba utajenga familia yako kutokana na mtazamo na fikra ulizonazo. Ambazo pengine umerithi kutoka kwa wazazi wako au jamii inayokuzunguka. Na fikra hizo huenda zisiwe sahihi.

Maisha yamekufunza nini? ni lazima ujiulize hilo kwa kipindi ambacho upo mpaka sasa duniani? bro maisha ni chuo kikuu na utashinda tu utakapokufa. Sahau kuhusu vyeti mnavyopata shuleni. Maisha halisi yako mtaani. Ni uwe mtumwa au mtu huru. Chuo kikuu unafundishwa skills za kazi. Lakini Duniani unafundishwa busara. Na usipokuwa na busara maisha yatakuadhibu vibaya uwe profesa au daktari. Mwisho wa yote mwenye busara ni mfame.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom