...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

Nape Nnauye

MP Mtama
Joined
Dec 26, 2012
Posts
99
Reaction score
408
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!


 
Last edited by a moderator:
Mkuu ziweke vizuri hizo link na youtube hazieleweki
 
Njoo na takwimu zenye kueleweka..sasa hicho ndio nini!!
 
Umejitahidi kuweka link vizuri lakin naskia makelele tu hakuna kinachosikika....
 
'ikulu siyo wodi ya wagonjwa', 'kwani hamuwaoni wagonjwa mahututi wanaotafuta urais mpaka makanisani'

nukuu kutoka kwa Nape ziarani Mara

chanzo:Mawio
 
Nape nilitegemea wewe kama Kiongozi utajutia kauli ulizotoa. Waliokuwekea kauli zako wamesahau hii ya siku za hivi karibuni uliyosema wenye akili timamu ni wale wanaosimamia msimamo wa serikali mbili, ikiwa na maana kuwa wasio waumini wa msimamo huo hawana akili timamu.

Rasimu ya Katiba imeletwa tujadili wote kwa kuheshimu uhuru wa mawazo. Wewe unasema sisi tusiounga mkono hoja za CCM hatuna akili timamu. Nilitegemea hili unalielewa hata baada ya kujadiliwa na vyombo vya habari na mitandao, kukomaa kwako kwa jambo hili sikuungi mkono.

Kila tamko lina gharama, lakini sisi tunakuambia kwenye mitandao tu. Subiri wazee kama watakuelewa au watanzania wengine watakaotafsiri kauli zako.
 
Haiwezekani kwenye mkutano mtu akazungumza within 11 minutes, hii video imechakachuliwa.

Kingine kinachonyesha video hii imechakachuliwa haijaanzia mwanzo wala haina mwisho ina maana mtu anaanza tuu kuongea from no where hakuna hata kuwasalimia wananchi hakuna?

Halafu unamaliza kuongea hata hakuna kuwashukuru wananchi? uongo mwingine mjipange kabla ya kupost


Na mwisho uombe msamaha kwa kuandika jina la mtu kwa kejeli
 
Hiyo clip ina dakika 11 tu
Haijaanzia mwanzo alipoanza kuogea,haionyeshi maneno yake ya mwisho wake akihitimisha,
The video is not proved not to be eddited
hatujaona ushahidi wowote wa aliepost na alierekodi kuonyesha haijafanyiwa edditing,
In that reason waandishi na wahariri wa magazeti mawili tofauti kukaa chini kutunga habari na kuandika habari zinazofanana sio rahisi
Hatujaona mlengwa akikiwaandikia demand note wahariri hao kukanusha kauli yake kama alivonukuliwa
Hatujaona hadhira aliyowahubiria nape wakikanusha hii habari hukutamka haya maneno dhidi ya wazee wetu.
Bado nasisitiza video iliowekwa hapa ni fake,it is modified to clear nape,
bora angekaa kimya...
Tutaitafuta clip nzima na suppoting evidences tutaziweka hapa jf.time will tell
 
hebu twambie kwa kuandika uliongea nini kuhusu wazee? maana hata link haieleweko zaidi ya kelele tupu.

Ina maana hukusema kuhusu wazee wetu?
 
Nape, kwangu mimi nakuona kama umepwaya mno kwenye kiti ulichopewa cha itikadi na uenezi. Hakika kwa kijana kama wewe kuwa unatoa threads kama hizi mitandaoni nakuona licha ya kupwaya kwenye kiti pia una tatizo la ufahamu wa siasa hasa za kisayansi!!
 
Nape haishii tu kumwita Dr. Slaa kibabu kwamba hana faida na asisikilizwe, amenukuliwa "wazee wanaopendekeza serikali 3 wanasumbuliwa na uzee na wanasubiri kufa", 'kama ni wanaccm ni oil chafu'

chanzo:Mawio

My Take:kama ni kweli
nape hana wazazi?
hana heshima na anajitabiria kifo ujanani na kutoufikia uzee
 
Kwisha ccm ...baba yangu ameapa kurudi ccm kwa ajiri ya vijana waharibifu kama wewe na nchemba
 
Kwa Ben Saatisa, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!


Hivi nape unadhani watu wanavyoibeza ccm ni nini sababu au mnaonewa...kutakuwa sehemu mmekosea sasa mlivyokuwa sikio la kufa hata miguno y andani kwenu (ccm ) hamsikii
 
Last edited by a moderator:
Makamanda wa Chadema wanaoinyima usingizi ccm wanazidi kuongezeka. Ben Saanane naye kumbe ni tishio mtaa wa lumumba. Sasa makamanda tuongeze kasi ya mashambulizi kwakuwa ccm inakaribia kuachana mwili na roho.
Dkt. Slaa na Kamanda Mbowe endeleeni na kazi hiyo hiyo nzuri ya kuwapika kiukomavu vijana wengi zaidi ili kazi yetu ipate kuwa ya uhakika na nyepesi zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kama wewe unajua imechakachuliwa, lete ya kwako ambayo haijachakachuliwa tuione.

Jenga hoja kwa evidence na siyo mihemko ya kibavicha.

Hizi kelele unazopiga ni kelele za debe tupu. Huoni huyo aliyeleta uwongo kuhusiana na hili swala ameamua kufunga thread yake haraka na kuukimbia uongo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…