Mwisho wa Ubaya Aibu

Mwisho wa Ubaya Aibu

Haya mambo ya wanawake wa sasa hivi na nikifikiria kuajiriwa ofisini natamani hata nitafute genge langu la nyanya.

Mtu upo kazini na umeajiriwa serikalini, unajinyima kisa mwanamke na mtoto wasikose. Unakuja kulea na mtoto akifika miaka kumi anaanza kumlisha sumu juu yako, au anajua si wako wewe hujui mtoto anakupa mahaba ya kinafiki maana keshalishwa sumu juu yako. Tena akifanya kosa, hamgusi anakuachia wewe umpige kwa sifa kama baba unatandika hapo wee, kumbe ndiyo unatega bomu hujijui

Mtoto unasomesha kwa kutumia nguvu nyingi hadi anapata kazi, wewe unaangukia ustaafu huna mbele wala nyuma zaidi ya kutegemea pensheni.

Unamchukua mkeo hadi nyumbani kwa mwanao, unakaribishwa sebuleni. Unatulia na kuangalia filamu ikuzubaishe, mtoto anaenda jikoni na kumpa mama yake laki mbili. Akija sebuleni anakutoa 40000 anakwambia hali ngumu, hapo sumu zile alizolishwa zinafanya kazi.

Mnatoka na kuondoka, mkeo pasipo mshipa wa aibu anakueleza hajapewa hela mtoto alisema atakupa wewe.
Loh! Sallalah kile kiarobaini elfu chako kinakamuliwa huku laki mbili zake kaziweka kibindoni.

____

Au ukute umemsomesha sana, kumbe si wako na amemlisha sumu tayari. Unategemea nini hapo?

UKIWA NA MRADI WAKO HAKUNA KUSTAAFU, UTAJILIA HATA AKIPATA KAZI HUYO WEWE BADO UTAKUWA NA MAHALI PA KUJISHIKIZA UNAWEZA EPUKA. SI KWAMBA NASHAURI TUSIAJIRIWE AU KUSOMESHA WATOTO WETU. BALI TUSIISHI KWA MATARAJIO KUTOKA KWA MTU. TIMIZA WAJIBU WAKO TU

****
INGAWA MENGI HAYAHUSIANI NA MADA HIYO LENGWA, ILA TUJITAFAKARI KWA UMAKINI NA HUYO BWANA ASHUKURU MUUMBA KAJUA MAPEMA. LA SI HIVYO ANGEKUJA KUFA NA UGONJWA WA MOYO
Umeongea ya kweli mkuu. Ndio wadada wengi wa sasa walivyo. Ile value ya baba hataki ionekane kwa mwanae.
 
Ndio kawaida yao. Au wanasema baba ako alikufa kumbe walivurunda wao.
Huyu baba mzazi anae. Sio Michael. Tuseme aliwapa Michael na Rodgers mtoto. Sasa Michael akajua yeye sio baba mzazi akajitoa akabaki Rodgers anamuhudumia mwanae. Labda Rodgers nae ndo asihudumie
 
Inawezekana kabisa. Hasa kama ni ujauzito wa kwanza sababu hakuna kinachobadilika
aiseee!! basi kwangu mimi itakuwa ni vigumu sana kuificha mimba ya miezi miwili.. yaani nisione dalili hata moja kwa muda wote tunaokutana na wewe? na elimu yangu ya shule za kata ila nimeelimika vya kutosha kiasi cha kutokukosa uelewa kwa jambo dogo kama hilo.
 
Wamekutana mara moja kavu jamaa akatimka nchini. Kwahiyo mpaka mwanamke anajifungua hayupo bongo alikua anatumiwa picha za mtoto mchanga kumbe wakati huo mtoto ana miezi miwili
 
Mtoto atajisikia vibaya sana. Nilimuuliza Michael hakuna jinsi ya kumshtaki huyo mama maana kamfanya fala muda mrefu sana. Miaka mitatu anahudumia japo na yeye alishahisi kapigwa changa la macho
Tukio kama hili linaweza kusababisha chuki kali sana kati ya mama na mtoto ukubwani, pale mtoto atakapoambiwa kwamba mama yake aliwahi kumtumia kama bidhaa ya kujipatia pesa kwa kuwalaghai wanaume wawili akiwabebesha majukumu ya uzazi pasipo wanaume hao kujua, na baadae ndio akaamua kumuuza kwa mwanaume mmoja ambae sasa hivi ndio anamuita baba. Na kwanza akishafahamu hilo tukio anaweza kuanza kuhisi yawezekana hata huyo wa sasa sio baba yake mzazi na hasa kama kuna mapungufu kwenye mahusiano yao.

Huyo michael atakama ataenda kushitaki kwa ninavyofahamu mimi sana sana atalipwa fidia tu ambayo itakuwa kwa namna ya makadirio na huyo baba mtu ambae ndio amekabidhiwa mtoto!! halafu unahudumia miaka mitatu bila kugundua chochote huyo nae alikuwa karogwa.
 
Labda alipigwa juju kweli
Tukio kama hili linaweza kusababisha chuki kali sana kati ya mama na mtoto ukubwani, pale mtoto atakapoambiwa kwamba mama yake aliwahi kumtumia kama bidhaa ya kujipatia pesa kwa kuwalaghai wanaume wawili akiwabebesha majukumu ya uzazi pasipo wanaume hao kujua, na baadae ndio akaamua kumuuza kwa mwanaume mmoja ambae sasa hivi ndio anamuita baba. Na kwanza akishafahamu hilo tukio anaweza kuanza kuhisi yawezekana hata huyo wa sasa sio baba yake mzazi na hasa kama kuna mapungufu kwenye mahusiano yao.

Huyo michael atakama ataenda kushitaki kwa ninavyofahamu mimi sana sana atalipwa fidia tu ambayo itakuwa kwa namna ya makadirio na huyo baba mtu ambae ndio amekabidhiwa mtoto!! halafu unahudumia miaka mitatu bila kugundua chochote huyo nae alikuwa karogwa.
 
Wamekutana mara moja kavu jamaa akatimka nchini. Kwahiyo mpaka mwanamke anajifungua hayupo bongo alikua anatumiwa picha za mtoto mchanga kumbe wakati huo mtoto ana miezi miwili
Hee basi afanye kuhesabu alitoa sadaka, kama ana uchungu sana akachukue fidia
 
Back
Top Bottom