Haya mambo ya wanawake wa sasa hivi na nikifikiria kuajiriwa ofisini natamani hata nitafute genge langu la nyanya.
Mtu upo kazini na umeajiriwa serikalini, unajinyima kisa mwanamke na mtoto wasikose. Unakuja kulea na mtoto akifika miaka kumi anaanza kumlisha sumu juu yako, au anajua si wako wewe hujui mtoto anakupa mahaba ya kinafiki maana keshalishwa sumu juu yako. Tena akifanya kosa, hamgusi anakuachia wewe umpige kwa sifa kama baba unatandika hapo wee, kumbe ndiyo unatega bomu hujijui
Mtoto unasomesha kwa kutumia nguvu nyingi hadi anapata kazi, wewe unaangukia ustaafu huna mbele wala nyuma zaidi ya kutegemea pensheni.
Unamchukua mkeo hadi nyumbani kwa mwanao, unakaribishwa sebuleni. Unatulia na kuangalia filamu ikuzubaishe, mtoto anaenda jikoni na kumpa mama yake laki mbili. Akija sebuleni anakutoa 40000 anakwambia hali ngumu, hapo sumu zile alizolishwa zinafanya kazi.
Mnatoka na kuondoka, mkeo pasipo mshipa wa aibu anakueleza hajapewa hela mtoto alisema atakupa wewe.
Loh! Sallalah kile kiarobaini elfu chako kinakamuliwa huku laki mbili zake kaziweka kibindoni.
____
Au ukute umemsomesha sana, kumbe si wako na amemlisha sumu tayari. Unategemea nini hapo?
UKIWA NA MRADI WAKO HAKUNA KUSTAAFU, UTAJILIA HATA AKIPATA KAZI HUYO WEWE BADO UTAKUWA NA MAHALI PA KUJISHIKIZA UNAWEZA EPUKA. SI KWAMBA NASHAURI TUSIAJIRIWE AU KUSOMESHA WATOTO WETU. BALI TUSIISHI KWA MATARAJIO KUTOKA KWA MTU. TIMIZA WAJIBU WAKO TU
****
INGAWA MENGI HAYAHUSIANI NA MADA HIYO LENGWA, ILA TUJITAFAKARI KWA UMAKINI NA HUYO BWANA ASHUKURU MUUMBA KAJUA MAPEMA. LA SI HIVYO ANGEKUJA KUFA NA UGONJWA WA MOYO