Kuna dogo mmoja alikuwa na mpenzi na walidumu kwa muda wa miaka 3
Siku ya siku yule binti akamuambia yule dogo kuwa anataka kwenda Dodoma kwa dada yake kupumzika [HAWAKUWA WANAISHI PAMOJA LAKINI NYUMBANI KWA DOGO NA BINTI PALIKUWA KARIBU KIASI KWAMBA WALIKUWA WANAONANA KILA SIKU] Dogo alimruhusu na binti alikwenda
Zikapita siku 5 na kijana akapata habari kuwa mpenziwe alikuwa hajaenda Dodoma bali alikuwa Igunga kwa jamaa mwingine na kijana aliamua kumpigia simu mpenziwe kumuuliza na binti alikubali na alimuambia kuwa amsahau
Kijana alitaharuki na kuanza kuchanganyikiwa na alikaa siku mbili bila kula na siku ya tatu alikunywa sumu,bahati nzuri siku anakunywa kaka yake alikuwa amekwenda kumtenbelea na kwa muda aliofika ilikuwa ni kama dakika 5 tu tangu dogo anywe sumu
Kaka mtu alipofika akamkuta dogo yupo kwenye harakati za mwanzo za kuhangaika huku akitoa maneno ya kujilaumu ni kwanini amekunywa sumu,kaka yake bila kupoteza muda aliomba maziwa kwa jirani na bahati nzuri yakapatikana na alimnywesha na wakamkimbiza hospital na alipatiwa huduma
Baada ya siku 5 kijana aliruhusiwa kutoka hospital na maisha yakaendelea
Baada ya miezi 6 dogo alipata Dem mkali kuliko yule wa mwanzo na dogo akawa anafurahia sana maisha yake ya kimapenzi kuliko mwanzo kwani haya alikuwa akiyasema mwenyewe
Lakini siku moja alisema wazi kuwa kitendo cha kunywa sumu anakiona kama kilikuwa ni kitendo cha kijinga kuliko vyote alivyowahi kuvifanya kwenye maisha yake na anajilaumu sana kwani anayafurahia maisha kuliko alivyokuwa na mpenzi wa mwanzo!