Mwisho wa kulala 30/10/2010

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
47
Watu wanasema mwisho wa kulala ni 30-10-2010. RFA alfajiri hii wanasema majina yamebanduliwa Shinyanga. Fuatilieni udhalimu huu. Huku haya yakiendelea Prof. Lipumba amwunga mkono Dr. Slaa.

Kila mtu anawajibu wa kutimiza; mpiga kura kupiga na kulinda kura (safiri uende kupiga kura hata kama ni mbali vipi), mawakala kupata ujasiri na kutowasaliti wa Tanzania kwa gharama yeyote, askari wapendwa kujua kuwa nguvu ya wananchi haizuiliwi kwa risasi wala maji ya kuwasha, asiye na kadi ya kupiga kura au ambaye umri wake haujafika alinde nyumba za wapiga kura. Baada ya matokeo tushangilie kwa amani.

MUNGU BARIKI TANZANIA, AFRIKA NA WOTE WAKAAO HUMO.
 
ni kweli kabisa usemayo na ni hekima kubwa. mie tayari nina suti mbili mpya na ghali sana. moja nitavaa kwenye sherehe za kuapishwa rais jakaya kikwete kwa muhula wa pili na nyingine nitavaa siku ya kuapishwa kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano kwa mara ya kwanza maishani mwangu

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Ni tarehe na mwaka ambayo watanzania kwa ujumla wanatakiwa kujikomboa kutoka kwenye makucha ya kunyanyaswa,kupuuzwa na wakoloni weusi(CCM). Vyama vyote makini vya upinzani vimesema vitatoa huduma za jamii bure,vitapiga vita ufisadi na kupunguza gharama za serekali ili walau wananchi wapate huduma hizo wao CCM wanasema hivyo haviwezekani jamani ni siku muhimu kwetu kuchagua mabadiliko.

"INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO UHAI WAKO UKO KWENYE KURA YAKO"
 
ni kweli kabisa usemayo na ni hekima kubwa. mie tayari nina suti mbili mpya na ghali sana. moja nitavaa kwenye sherehe za kuapishwa rais jakaya kikwete kwa muhula wa pili na nyingine nitavaa siku ya kuapishwa kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano kwa mara ya kwanza maishani mwangu

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

chupi, tisheti, kofia, kanga, nk ya chama haina nafasi kwa watanzania wazalendo wa nchi hii. kinachotakiwa ni uzalendo wa kutetea rasilimali za nchi hii ndio sbb ya kusherehekea.

kwa bahati mbaya sana chama chetu kimekuwa kikitumia mavazi kama kivutio cha kuwanasa watanzania.
kwa uhakika, obama suit unayozozungumzia pamoja na sare za kampeni za chama chetu na vyama vingine vinavyotumia 'sanamu' za namna hiyo, siku zake za kuraruliwa na watanzania kuvalishwa vazi rasmi la uzalendo, zimefika!!!
 
Usingizi tutaendelea kuupata, hatuna shida.
Hureeeee Tanzania kwa utulivu na amani
:yield:
 
ni kweli kabisa usemayo na ni hekima kubwa. mie tayari nina suti mbili mpya na ghali sana. moja nitavaa kwenye sherehe za kuapishwa rais jakaya kikwete kwa muhula wa pili na nyingine nitavaa siku ya kuapishwa kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano kwa mara ya kwanza maishani mwangu

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Safari bado tunayo ndefu, kura hazijapigwa tayari mshajitangazia ushindi.
 
Back
Top Bottom