mzushi flani
JF-Expert Member
- Jan 20, 2020
- 1,627
- 2,468
Kipimo cha utii ni uaminifu. Na Mungu ametupatia uhuru na miongozo ya hakika, kazi kwetu kufuata
Kama tuu vile unavyokosa uaminifu kwa wanaokuzunguka
Hiki nadharia ya "kipimo cha utii ni uaminifu" mbona ni kama fallacy!? mathalani, nnapotii sheria za barabarani nnakua na uaminifu juu ya nini!? leo hii watu wanatii sheria za kidini sababu ya hofu wanayojengewa na mungu kwa kuambiwa adhabu za huko mbele(vitisho) au ahadi za kufikirika maana hazina uthibitisho wa kuja kutimiziwa(ulaghai). mpaka hapo hakuna uaminifu katika huo utii hivyo hiyo ni hoja dhaifu sana!
unasema "mungu ametupatia uhuru na miongozo hakika" vipi jamii zilizoendelea bila hata kumjua mungu ila tu kwa kufata falsafa zao za kimaisha tu!? kwa misingi ya virtue!?
mwisho pia hata mungu bado haijawahi thibitishika ndo maana dini zinaongezeka kila siku kwa kutumia hiyo LOOP HOLE!