Mwisho wa kizazi na nguvu ya Mungu

Kipimo cha utii ni uaminifu. Na Mungu ametupatia uhuru na miongozo ya hakika, kazi kwetu kufuata
Kama tuu vile unavyokosa uaminifu kwa wanaokuzunguka

Hiki nadharia ya "kipimo cha utii ni uaminifu" mbona ni kama fallacy!? mathalani, nnapotii sheria za barabarani nnakua na uaminifu juu ya nini!? leo hii watu wanatii sheria za kidini sababu ya hofu wanayojengewa na mungu kwa kuambiwa adhabu za huko mbele(vitisho) au ahadi za kufikirika maana hazina uthibitisho wa kuja kutimiziwa(ulaghai). mpaka hapo hakuna uaminifu katika huo utii hivyo hiyo ni hoja dhaifu sana!

unasema "mungu ametupatia uhuru na miongozo hakika" vipi jamii zilizoendelea bila hata kumjua mungu ila tu kwa kufata falsafa zao za kimaisha tu!? kwa misingi ya virtue!?

mwisho pia hata mungu bado haijawahi thibitishika ndo maana dini zinaongezeka kila siku kwa kutumia hiyo LOOP HOLE!
 
Mungu anaweza kila kitu.

Mungu hapangiwi chochote.

okay, sijampangia lakini huoni hata kwa kutumia logic rahisi ni kua si sawa kwa yeye kushindwa kusamehe!? tena ukizingatia ana ji brand kua ni muweza wa yote,mjuzi wa yote na mwingi wa kusamehe! anaji contradict au wewe huoni mkuu!?
 
Katika hali ya tafakuri ya kawaida, Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote akiwemo kiumbe binadamu!

Kizazi cha binadamu hufanya watu kuongezeka kila kukicha. Ongezeko la watu na kizazi kuendelea kuwepo duniani ni kwa sababu ya tendo la ndoa/ngono. Yaani kiumbe hai binadamu na yote yanayomkuta ni sababu ya kufanya tendo hilo. Kitendo cha mwanamke kukutana na mwanaume ndo kinafanya binadamu na matatizo yaliyopo yaendelee kuwepo. Vitu vyote unavyoona binadamu anafanya, binadamu yule ni kwa vile alizaliwa, naye atazaa tena binadamu mwenye tabia na matendo yake, yawe mazuri au mabaya.

Ninachotaka kusema ni kuwa jeuri ya Mungu au nguvu za Mungu kufanya yote haya yanayomkuta binadamu ni kumuumba binadamu na hali au namna ya kuweza kufanya mapenzi au tendo la ndoa ngono. Tendo lile ndo maana aliliweka kwa namna ambayo kiumbe binadamu linamfurahisha akili na mwili. Kwa maneno mengine, tendo lile lisingekuwa linasisimua mwili na akili za binadamu, naamini watu wasingezaliana na kuongezeka. Hiyo ndo jeuri ya Mungu na hapo ndo mtego wa Mungu kwa binadamu.

Siku binadamu duniani wakiligundua na kupata upeo na uwezo wa kuliacha tendo lile miaka na miaka, dunia ingekuwa na history nyingine na mabadiliko ya nguvu Mungu yangejitokeza. Mthalani, binadamu duniani wakikubaliana kuacha kuzaa na kuzaliana miaka almost Mia au Mia mbili ili waliopo waishe naamini Mungu angejipanga upya. Lazima angetokea na kuumba ulimwengu mpya. Binadamu duniani nzima nikubaliane, na viumbe wengine ikitokea nao wakajikuta wanafanya hivo nadhani Mungu angepata akili nyingine. Bahati mbaya au nzuri ni kama tendo lile ni kama sehemu ya akili au roho au utu wa mtu, ni kama ndo maisha yenyewe. Lkn ingewezekana tungeacha kuzaa na kuzaliana miaka na miaka tuone kutatokea nini- duniani.

Ndo maana nikasema, jeuri ya Mungu kwa binadamu ni kufanya tendo la ndoa au ngono kuwa na hali ya burudani and it's like uncontrollable urge.
Kwa maneno mengine ni kuwa ngono ni tendo la maana kubwa sana katika concept ya uumbaji. Janja ya Mungu ni hapo...... Ebu tujaribu kama miaka 150, Mungu aumbe upya !
mnara wa Babeli ulianza hivi hivi
 
okay, sijampangia lakini huoni hata kwa kutumia logic rahisi ni kua si sawa kwa yeye kushindwa kusamehe!? tena ukizingatia ana ji brand kua ni muweza wa yote,mjuzi wa yote na mwingi wa kusamehe! anaji contradict au wewe huoni mkuu!?
Hebu Soma VIZURI hapa chini..

Mungu Anaweza yote, Anaweza Kuumba, Anaweza Kuchukua uhai wa kiumbe alichoumba, Anaweza kusamehe na anaweza kutoa adhabu.

Lakini licha ya uweza alionao bado Mungu utumia uweza na Mamlaka yake kadiri ya mapenzi yake.. Anaweza kukupa adhabu ya ugonjwa ili umrudie yeye, na anaweza kukufanya uumrudie yeye bila adhabu..

Hufanya yote kadiri ya mapenzi na mipango yake kwetu.
 
Hebu Soma VIZURI hapa chini..

Mungu Anaweza yote, Anaweza Kuumba, Anaweza Kuchukua uhai wa kiumbe alichoumba, Anaweza kusamehe na anaweza kutoa adhabu.

Lakini licha ya uweza alionao bado Mungu utumia uweza na Mamlaka yake kadiri ya mapenzi yake.. Anaweza kukupa adhabu ya ugonjwa ili umrudie yeye, na anaweza kukufanya uumrudie yeye bila adhabu..

Hufanya yote kadiri ya mapenzi na mipango yake kwetu.

Okay, sasa yeye anapungukiwa na nini nisipomrudia!?. maana kama anaweza kunipa masaibu na nkamrudia na nisipone ina maana hana faida kwangu! hii ni logic rahisi sana tena sana ambayo mtoto wa miaka 12 anaweza kujiuliza ba kung'amua kua jibu ulilotoa ni matokeo ya indoctrination!

na pia unaweza kunipa Mungu ni nani ni nini!? kuna uthibitisho wowote wa uwepo wake!? au walau hizo nguvu zake!?
na pia ukimaliza hapo nambie ni mungu yupi maana wako wengi sana zeus,Allah, buddha,Thor l,Yesu, Osiris nk
 
Shida watu huwa mnadhani tunda walilokula Adam na Eva ni ngono;

Tunda walilokula ni tunda halisi la mti uliokuwepo kwenye bustani ya Edeni.

Mungu aliwaagiza kuzaana mara tu ya kukamilisha uumbaji wa wote wawili, ina maana aliwaruhusu kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kukamilisha uumbaji wao na SI KWAMBA walianza kufanya tendo la ndoa baada ya uasi wa sheria (kula tunda walilokatazwa na Mungu)

Msiwe hivyo jamani, tunda hilo katika maandiko siyo fumbo bali ni lugha Moja kwa moja na dhahiri kabisa.
 
Shida watu huwa mnadhani tunda walilokula Adam na Eva ni ngono;

Tunda walilokula ni tunda halisi la mti uliokuwepo kwenye bustani ya Edeni.

Mungu aliwaagiza kuzaana mara tu ya kukamilisha uumbaji wa wote wawili, ina maana aliwaruhusu kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kukamilisha uumbaji wao na SI KWAMBA walianza kufanya tendo la ndoa baada ya uasi wa sheria (kula tunda walilokatazwa na Mungu)

Msiwe hivyo jamani, tunda hilo katika maandiko siyo fumbo bali ni lugha Moja kwa moja na dhahiri kabisa.

Kuna uthibitisho wa ukweli wa haya maandiko!? na uthibitisho wa uwepo wa yalikotoka kama inavosemekana!?

najaribu kuhoji basis itakayotupa legit ya story yako hii ili isiwe kama mapokeo ya hekaya kama hekaya zingine za majinamizi yatakayotutafuna nyama kama ukichekewa kurudi jioni nyumbani
 
Okay, sasa yeye anapungukiwa na nini nisipomrudia!?. maana kama anaweza kunipa masaibu na nkamrudia na nisipone ina maana hana faida kwangu! hii ni logic rahisi sana tena sana ambayo mtoto wa miaka 12 anaweza kujiuliza ba kung'amua kua jibu ulilotoa ni matokeo ya indoctrination!

na pia unaweza kunipa Mungu ni nani ni nini!? kuna uthibitisho wowote wa uwepo wake!? au walau hizo nguvu zake!?
na pia ukimaliza hapo nambie ni mungu yupi maana wako wengi sana zeus,Allah, buddha,Thor l,Yesu, Osiris nk
Fungua mada yako nije nikugonge hukohuko maana maswali yako ni mengi na yako nje ya mada.

Fungua mada yako, nitag.
 
Hahahahah, naiona hofu imeinuka ndani yako.

Mimi sijakereka, na wala sitamani yakukute mabaya, LAKINI tuangalie yafuatayo..

Tabia ya ujeuri ni tabia ya mwanadamu, Je wewe unayo jeuri au hauna?

Kama unayo.. Basi malizia sentensi hii kimyakimya "Jeuri yako...." Hahahah asanteee.

Duniani hapa tunaishi na watu wengi, nilivosema Jeuri yako itakuponza nimeshangaa unasema Mungu hayupo hivo na wakati sijasema Kama Mungu atakupa adhabu au atakubariki.. Hahahaa, narudia tabia yako itakuponza.

Hutaki? Haya Basi ngoja nikuridhishe sawasawa na kauli yako... Maneno yako yatakuponza.
Hiyo ni hali ya kujiwekea mipaka ya kufikiri au kuwaza nje ya kawaida
 
Kuanzia atomi hadi nyota vimeumbwa kutokana na mahesabu na kanuni maaluumu. Utaratibu wa ndani ya kanuni zinazojulikana za Fizikia, Kemia astronomy na Biolojia huchanganya akili za binadamu.

Hewa ni mchanganyiko wa Naitrojeni (78%), Oksijeni (21%) na noble gas ambayo ni 1% . Yaani; Hewa si kitu kimoja bali ni mchanganyiko. Kwa asilimia hizo za juu, Oksijeni angezidi kipimo cha 21% ingeweza kuyachoma mapafu yetu. Na angekuwa chini ya 21% asingeweza kuchoma rutuba za damu na isingewezekana binadamu na wanyama kuishi na kipimo hicho hakibadiliki kutoka kwenye sehemu kwenda nyengine hata mvua ikinyesha.

Unajua tabaka la viumbe liko kwenye mpangilio wa kushangaza, na wanasayansi kila mwaka wanakuja wanavumbua sheria mpya zinazoendana na mpangilio huo. Na ulimwengu ulitokea na upo na upo na unaendelea kushangaza.

Muumbaji wa mpangalio huo ni lazima mda wote yupo hai, mwenye kutaka, mwenye kusikia kila kitu, mwenye kuona kila kitu, mwenye kusema, mwenye kuumba. Kwa sifa kama kifo, ujinga, kutoweza au kuondolewa na wengine, kulazimishwa, uziwi, upofu na ububu ni sifa zenye kasoro kama hizo haziwezi kuwa za muumbaji ambaye ni Mungu.

Kila kitu zaidi ya Muumbaji (Mungu) kinaitwa uumbaji. Kinachoitwa kwa sasa maumbile. Viumbe vyote havikuwepo ikiwemo space/The Universe. Muumbaji ndiye aliyeviumba vyote. Viumbe vyote ni kitu kinachoweza kutokea hali ya kuwa hakikuwepo mwanzo na ni kitu kinachotokea baada ya kutokuwepo. Yaani; vinaweza kutokea hali ya kuwa havikuwepo na vilevile vinatokea baada ya kutokuwepo.

Ulimwengu(the Universe) wote na viumbe waliomo wote ni kitu kilichotokea baada ya kutokuwepo. Kama haikuathiriwa na nguvu fulani basi ingebaki katika hali ya kutokuwepo na isingiweza kutokea. Kwa kuwa haiwezi kujiumba yenyewe, isingeweza na haiwezi kimaumbile kujiumba yenyewe basi isingeweza kutokea.

Hivyo, aliyefanya hayo ni lazima awe awepo. Na muda wote alikuwepo na hana mwanzo. Maana yake kuwepo kwake hakujatoka kwenye kitu kingine bali kitu chenyewe, hii inaashiria kwamba Muumbaji ambaye ni Mungu yupo na hakuumbwa na kitu kingine.

Kwa maana: Ni lazima awepo, daima yupo. Amekuwepo tokea tokea na hakutokana na chochote na hatosita kuwepo. Na ni kitu kamwe hakiwezi kutokea kama yeye na haijaweza kutokea.

Sasa wewe binadamu una nini cha special? Au hao viumbe wengine wana nini cha special? Yaani utampunguzia nini Mungu? Umelitafakari jambo lililo juu ya ufahamu wako? Kama Mungu anachukua roho za viumbe vyake mnatafsiri kifo ndiyo mwisho wa uhai wenu ninyi binadamu msipozaana mtampunguzia nini?

Hujui kuwa Mungu ni kiburi?

Hana mshirika, hana baba wala mama, hakuzaliwa, hana mtoto kwa sababu mtoto ni upungufu. Wenye watoto huhitaji ni kurithiwa kwa chochote wanachomiliki. Ikiwa ni mfalme atahitaji wa kurithi ufalme wake, ikiwa ni tajiri atahitaji wa kurithi utajiri wake. Mungu hafi wala hazeeki, sasa ahitaji mtoto wa nini?! Mungu ni mkwasi! Anajitosheleza yeye mwenyewe ndiyo maana hana ndugu wala mshirika. Yaani kiburi kweli kweli.
I see.... nimeipenda na urefu wake, hoja nzuri katika lugha/kiswahili kisicho rahisi!

Kwa maneno mengine ambayo ni generally; katika hali ya kawaida SISI BINADAMU NI VIUMBE WADOGO KUJUA HATA NGUVU NA UWEZO WA MUNGU, JINSI ALIVYOUMBA BINADAMU WAKE NA MAKUSUSUDI YAKE.....
Mantiki ya kusema vile hapo juu ni kwa nini shida na mateso duniani yamezidi na hakuna msaada toka kwa Mungu; hivyo basi tuachane na uzazi na kuzaliana ili shida zikome, na huyo muumba aanze upya!
 
Possible!
Level ya kufikiri hivyo, wameshaifikia Wazungu kwa kugeuza tendo la ndoa kuwa burudani badala ya kuzaliana na wanazaa wanapotaka. Hali hii imesababisha tishio la ku expire kwa jamii ya Wazungu kwani hawaongezeki na mwisho wa siku watafutika ulimwenguni
 
Mkuu wazo lako zuri ungekwepo kabla ya wazazi wako ingekua safisanaa ila sio mbaya anza kulifanyia kazi sisi tupo nyuma yako
Teh teh teh! 1/4bn za watu duniani, nitafanikiwa kweli? Ndo maana nikasema hii nguvu(janja au jeuri) ya Mungu muumba si mchezo! Binadamu duniani imetushinda
 
Unawaza vizuri sana ndugu! Kuna Maswali tata na mengi yahusuyo toka uasi wa Lucifer, kushushwa kwake duniani, kukutana na Eva na yaliyoendelea. Mambo mengine ni fiction tu- history of Christianity and it's Bible hugusia baadhi ya maswali/ mapungufu hayo
Kwahiyo Mungu alizidiwa ujanja na Adam & Eva kwa msaada wa ushawishi wa shetani!?

Pia Mungu muweza wa yote anaejua mwanzo namwisho alishindwa kujua kua Adam ataasi!? kama alishindwa kujua manaake sio mjuzi wa yote na tafsiri ni kua anajipa sifa za uongo Upande wa pili kama anajua yote inaleta ukakasi sana kwanini alikua disappointed mpka kukasirika na kuwatimua huko peponi!


Hii story ya Adam&Hawa(eva),mungu na shetani, na historia ya kuasi kwa shetani vyote vina ukakasi sana, vitabu hivi vya dini vinakubali kua mwanadamu ni kiumbe dhaifu hivyo anahitaji imani na msaada wa Mungu katika maisha yake hapa duniani, vilevile vitabu hivyohivyo vinadai kua Mungu alimuumba mwanadamu akiwa kamili na asie na madhaifu kabisa, ukitafakari kwa kina utaona hata shetani alikua sawa kukataaa kumsujudia adam, na alipomshawishi adamu kuasi ni wazi kua alimthibitishia mungu kua kiumbe chako ni dhaifu!

Hii story pia ina contradict na sifa ya mungu kua ni mwingi wa kusamehe!
 
Ni sawa na mtoto kumtishia baba kujiua akidhani anamkomoa.......
Binadamu tusipozaana tutakufa then tunapotea kwenye uso wa dunia halafu baasi. Nadhani maisha Duniani yanaweza kuendelea pasipo sisi.
Kama hivo basi tuachwe huru, mambo ya kuambiwa shida za duniani ni sababu ya mambo ya dhambi mara shetani mara sijui Mungu anapanga yeye yaachwe ! Yaani maisha yetu yawe huru kama anavyosema
 
Back
Top Bottom