The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,469
- 17,309
Dini inasema Mungu ni pendo, mungu ni upendo, mungu anatupenda watu wote, Mungu anampenda kila mtu na kwa upendo usio na kifani.
Dini inasema mungu ni yule yule asiebadilika, jana, leo na hata milele. Sasa twende na kauli ya Mungu ni pendo, kwa maana kwamba mungu hatakuja kubadilika, ni pendo milele na milele.
Dini inaenda mbali zaidi inasema Mungu atakuja kuwachoma moto watu na atawashushia hasira na ghadhabu zake zote( kwa maana kwamba Mungu atabadilika na kua katili sana). Kwa msingi huo sina ya kwamba Mungu ni yule yule asiebadilika ni ya uongo.
Dini inasema jehanamu iliandaliwa kabla ya kuumbwa misingi ya ulimwengu, kwa maana kwamba kabla binadamu hajaumbwa mungu alishaumba jehanamu ya kuwachomea moto hivyo ule moto kule jehanamu uko kabla ya binadamu. Na Mungu alishajua watu gani atawachoma moto, hata ufanyeje utachomwa tu moto.
Swali la kujiuliza, Mungu anaetupenda kama watoto wake, atakujaje tena atuchome moto? Hata binadamu hawezi kumchoma moto mtoto wake asiemoenda, sembuse anayempenda?