kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
WAKATI naisoma taarifa ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, iliyochapishwa na Gazeti la Guardian la Uingereza, nilishtuka.
Nilibaki nikitafakari uzito wa yaliyoandikwa kwenye gazeti hilo kongwe nchini Uingereza, habari hiyo jana ikiwa gumzo katika magazeti ya kila siku ya hapa nchini. Binafsi, nilijiuliza maswali yaliyokosa majibu.
Jambo la kwanza nilijiuliza ni huyu Dk. Hoseah ninayemfahamu ambaye ameamua kuzungumza kwa uwazi kuhusu masuala ya ufisadi na gazeti hilo au mwandishi ameongeza mengine aliyokuwa akiyajua juu ya ufisadi?
Nilizama kwenye tafakuri na kuhoji ni nini kimemfanya Dk. Hoseah kuweka wazi kuwa Rais Jakaya Kikwete, ndiye chanzo cha baadhi ya vigogo waliotajwa kushindwa kuchukuliwa hatua katika sakata la rushwa wakati Watanzania wanaamini kwamba mtawala huyo mkuu ni kinara wa kutetea wanaohusika na rushwa nchini?
Nimefika hatua ya kujiuliza hayo kutokana na Dk. Hoseah, kudaiwa kuwa ndiye chanzo cha tuhuma nyingi za ufisadi kushindwa kufanyiwa kazi-kesi kubwa za rushwa zinazowahusu viongozi wakuu wastaafu ili mradi kuwepo na dhana ya kuwasahaulisha wananchi.
Sasa niliposoma taarifa ile na kutokana na baadhi ya viongozi kuwaamini zaidi waandishi wa nje tofauti na waliopo nchini huku wakijikuta wanawapa nafasi kubwa na kuzungumza nao inakuwaje leo Mkurugenzi wa TAKUKURU kudai kuwa mwandishi yule kaongeza maneno yake, je aliyoyasema yeye ni yapi?
Je, anatueleza kuwa hakuhusika na zile taarifa na kwamba kuna uwezekano mwandishi kazipika habari zile? Kwa jinsi ninavyomfahamu Dk. Hoseah hana uwezo wa kumtaja Rais Kikwete kuwa anazuia kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kama amemtaja basi namuomba awe jasiri.
Ujumbe wangu kwako Dk. Hoseah ni kwamba hata kama uliyazungumza maneno hayo, huna haja ya kukanusha kwa kuwa huo ndio ukweli halisi uliopo kwa vigogo kushindwa kuchukuliwa hatua ingawa ninakumbuka jinsi na wewe ulivyosimama kidete mwezi mmoja uliopita kwa kuvaa joho rasmi la kumtetea Andrew Chenge, mbunge wa Bariadi Magharibi kwamba hana kashfa za ufisadi.
Hii labda ilitokana na kuwahi kukwaruzana na kupishana kauli na aliyekuwa Spika wa Bunge Samuel Sitta, ndiyo maana uligeuka msafishaji wa Chenge na kudai kuwa hapakuwa na ushahidi unaoonyesha alihusika na rushwa katika ununuzi wa rada, ambayo iliigharimu serikali ya Tanzania zaidi ya sh bilioni 40.
Ulimsafisha ili kumpa nafasi mbunge huyo aendelee na harakati za kuwania uspika katika Bunge la sasa hata hivyo hakufika mbali alibwagwa vibaya na chama chake (CCM).
Hivi Dk. Hoseah, kwanini usiwe na ujasiri hata kama umezungumza acha tufahamu hivyo kuwa Rais Kikwete ndiye anayechelewesha wahusika kukamatwa na kutoshughulikiwa.
Acha wakubwa zako wafanye uamuzi maana kwa sasa TAKUKURU imepoteza uelekeo, imegeuka chombo cha kuwatetea wala rushwa, badala ya chombo cha kuwashughulikia, usiogope ni wakati muafaka.
Kwa kauli zilizopo kwenye gazeti lile, wakati wako wa kujiuzulu kuongoza taasisi hiyo kwa kushindwa kutunza siri umefika, huu ni mwisho wako wa kuendelea kutetea watuhumiwa wa rushwa, naamini hakuna anayeweza kufahamu kuwa mwanadiplomasia yule kakulisha maneno bali wakubwa wako watajua umeropoka tu.
Kwa jinsi ufisadi ulivyofanyika ndani ya nchi huku kukiwa na tabaka kubwa kati ya walionacho na wasionacho kungekuwa na kila wajibu wa kuwakamata waliohusika na kuwashughulikia lakini kwa muonekano wa wazi Dk. Hoseah hana meno ya kufanya hayo kwa kuogopa kukiuka matakwa ya wakubwa wako.
Kuna uwezekano wa maneno hayo kusemwa naye lakini alizungumza na mwanadiplomasia huyo kumtaka asiyaandike, katika uandishi tunaita off record. Badala yake amekiuka taratibu baada ya kuona kuna umuhimu wa masuala hayo kupelekwa kwenye jamii ili ipate kufahamu sababu ya kesi kukaliwa.
Hata Dk. Hoseah akatae lakini ukweli unajulikana kwamba ni wazi vita vya rushwa, wanaoguswa ni watu waliokuwa na utajiri hivyo kumuwia vigumu kushughulikia ndiyo maana amekuwa akijaribu kuwasafisha wahusika.
Ofisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) iliwahi kulazimika kutoa taarifa za kupinga kitendo hicho na kudai suala hilo bado linashughulikiwa jambo lililoifanya jamii kuelewa wazi kuwa TAKUKURU imepoteza uelekeo katika kuchunguza rushwa nchini; leo hii Dk. Hoseah amepata wapi meno ya kumsema Rais Kikwete hadharani?
Ni jambo la kushangaza lakini yote hayo ni wazi Mungu ameamua kuwaonyesha Watanzania yale waliyokuwa wakiyafikiria siku zote sababu za kushindwa kuchukuliwa hatua vigogo walioingiza nchi hasara na kuamua kujilimbikizia mali na kuwaachia umaskini wa kutupwa Watanzania.
Je, inawezekana Rais Kikwete ameamua kwa makusudi kumwambia Dk. Hoseah asishughulikie hizo kesi kwa kuwa anaweza pindi atakapoondoka madarakani kuingizwa katika tuhuma kama hizo?
Ninaamini mazungumzo ya Dk. Hoseah aliyafanya na mwanadiplomasia wa Marekani, Purnell Delly, jijini Dar es Salaam Julai 14 mwaka 2007, yaliwekwa kwenye rekodi hivyo kama anataka kutetea kibarua chake amuonyeshe mkubwa wake kile alichokiongea ambacho anakiamini kiko tofauti ili abaki katika wadhifa huo wa kuendelea kuvaa vazi la kusafisha watuhumiwa wa rushwa.
Lakini, jamii iliyoweza kumshinda adui ujinga kwa kupata elimu angalau ya kujua kusoma na kuandika ataelewa kuwa maneno yale umeyaongea lakini hukutaka kuyaweka hadharani; huna budi sasa upumzike ili tupate kiongozi atakayeweza kusimama kidete kushugulikia wabadhirifu na walioiingiza nchi hasara katika dimbwi la umaskini uliokithiri.