Mwinyi Zahera ni kafara tu

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Miaka sita iliyopita mwezi Desemba baada ya mechi ya Mtani Jembe kati ya Yanga SC na Simba SC mechi iliyotamatika kwa Yanga SC kuchabangwa magoli 3-1, aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Ernest Brands alifurushwa. Naam, alitimuliwa kwa tuhuma mbinu zake zimefikia ukomo kuipa mafanikio klabu hiyo kongwe zaidi nchini.

“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Baraka Kizuguto aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.

Nilipata kufanya mahojiano na kocha huyo mwenye haiba ya upole kuuliza amepokeaje hali ya kuvunjiwa mkataba wake na waajiri wake ? Brandts alichukua kama dakika moja akiwa kimya kabla ya kujibu swali langu kisha akajibu;

“Ni kawaida katika taaluma yetu kuvunjiwa mkataba pale waajiri wako wanapokosa imani na wewe lakini jambo moja linapaswa kufanyiwa kazi kwa vilabu vya ukanda huu wa Afrika Mashariki. Benchi la ufundi ili liwe bora ni lazima liheshimiwe na mapendekezo yake ya mara kwa mara kwa uongozi yafanyiwe kazi ili liweze kufanya kazi zake kwa ufasaha”

Nilitamani kuendelea kumuuliza Brandts lakini unyonge wake ulinifanya kutamka maneno mawili tu; “ Asante Mwalimu “

Nilitafakari sana kauli ya Brandts na utendaji wa viongozi mbalimbali wa soka ukanda huu wa Afrika Mashariki nikabaki nakuna kichwa.

“Huwezi kuwa na timu bora yenye ushindani endapo idara zote muhimu katika klabu hazifanyi kazi katika ufanisi mzuri. Kosa la timu huonekana haraka sana kuliko makosa ya kiutendaji ya klabu ambayo kwa namna moja ama nyingine hudhoofisha utendaji wa timu“, huyu alikuwa George Lwandamina aliyekuwa kocha wa Yanga, kauli yake muda mfupi baada ya kuachana na Yanga.

Huyu nae alinivuruga lakini kwa mbali nilianza kumuelewa.

“Nimeagiza kusajiliwa kipa kutoka Kenya lakini nimepewa kipa ambaye hakuwa katika mipango yangu. Kuna wachezaji kama watatu nimewataka sijawapata lakini nitajitahidi kwa walioleta na waliopo kuhakikisha tunapambana kubeba kombe ingawa imani imepungua“, Mwinyi Zahera dirisha dogo la usajili msimu wa 2018-19.

ZAHERA NI KAFARA TU

Soka ni taaluma kamili inayohitaji umakini katika utendaji wake ili kuleta matokeo chanya kama zilivyo taaluma zingine katika maisha yetu ya kawaida.

Msimu wa 2018-19 binafsi yangu nilipomuona Mwinyi Zahera katika benchi la Yanga SC na aina ya kikosi alichonacho ; kwa uthubutu nilitamka “ Yanga SC itakuwa tishio katika kinyang’anyiro cha ubingwa “. Kauli yangu iliishi katika uhalisia wake licha ya wengi kukikatia tamaa kikosi kile lakini ndio kilichowapa nafasi mwaka huu wa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika.

Mwinyi Zahera ni mmoja wa waalimu katika soka wanaojiamini na kuijua kazi yao ingawa ana tatizo la kutopokea ushauri kama anahisi yupo sawa hata kama mazingira yanambana. Ni kasumba tunkatika uumbaji kama binadamu wengine.

Kwa nini nasema Zahera hapa ni kafara tu?

Yanga kama klabu lazima wakae chini na watafute tatizo la msingi katika kusua kwao ili kama kung’oa mzizi au kutafuta tiba iwe ya kudumu na isimame kama mustakabali wa klabu .

Ni dhahiri Yanga wameingia katika ligi wakiwa bado hawapo sawa katika mfumo mzima wa kiuchumi ambao uliwafanya kupoteza wachezaji wao mahiri , wengine kugoma kwa kukosa stahiki zao na baadhi kuitumikia klabu wakiwa na nyuso za kukata tamaa. Masilahi popote pale ulipo ndio msingi wa ufanisi wa kazi yako hili tukumbuke. Inasemekana kwa sasa wachezaji karibu wote wazawa wanaidai klabu yao huku malipo yao yakiwa katika hatma ya viongozi.

Wengi wanakuja na hoja ya wachezaji wengi waliosajiliwa msimu huu ni mapendekezo ya mwalimu Mwinyi Zahera katika mkakati mzima wa kuisuka Yanga SC . Sahihi , sehemu kubwa ya kikosi ni mapendezo yake lakini idadi kubwa ya wachezaji aliowapendekeza hapa nchini kwa maana ya wazawa hakuwapata ili kupata mseto kamili wa kuisuka Yanga mpya.

“Popote pale duniani klabu hujengwa na wazawa kisha wachezaji kutoka nje huja kuboresha endapo wataweza kuendana na mfumo kwa haraka . Unapokosa back kubwa ya wachezaji bora wazawa wenye uchungu na timu yao basi tambua una kazi ya ziada kuufikia ubora ambao wengi wanautaka “ - Mwinyi Zahera

Hapa nilimuelewa sana huyu kocha ; Yanga ni moja ya klabu ambayo ina lundo la averaged players kwa maana ya wazawa hususani kikosi cha sasa . Hii ni moja ya sababu inawapa kazi sana kuiva kimbinu na kiufundi kwakuwa wengi wao wanakuwa katika mizani sawa na wachezaji wengi wa timu pinzani pengine hata kuzidiwa.

Haya yote yanatokana na Yanga kama klabu kukosa anticipation bora kiuchumi kuijenga timu yao . Utaniambia kulikuwa na kubwa kuliko na kamapeni zingine . Ni kweli wanachama walichanga na juhudi zilionekana kwa kutafuta wadhamini kama GSM lakini linapotokea suala la kushindwa tu kumalizana na Andrew Vicent mlinzi wao anaewadai milioni 45 kwa zaidi ya miaka miwili , hili linavunja moyo wa kiutendaji kwa wachezaji na pia wachangiaji mwisho wa siku Zahera anachokwa na wachezaji wenye njaa mazoezini na ubaya unakwenda kwake.

Kabla ya kumtupia mawe Zahera na mbinu zake , wanachama wafanye tathimini ya kina ya uwezo madhubuti wa klabu kuwa na misingi yake kiutendaji katika short term plans na long term plans.

Mafanikio hayaji kama maji , mafanikio yanahitaji uvumilivu na ustahimilivu. Mahasimu wenu wakubwa Simba SC walipotea katika ramani ya soka kimataifa kwa takribani miaka mitano . Walikaa chini na kujifanyia tathimini wakagundua mfumo wa uendeshaji timu ndio tatizo lao la kwanza la msingi wakalifanyia kazi na sasa mafanikio yanaonekana. Tangu wametoka katika mfumo wa umiliki kupitia wanachama na kuingia katika mfumo wa hisa, Simba wameweza kubeba ligi kuu mara mbili mfululizo, kufika robo fainali klabu bingwa Afrika , kuboresha miundo mbinu yao ; kwa sasa viwanja vyao vya Bunju vipo hatua za mwisho kuanza kutumika lakini pia wamejifunza kitu kikubwa cha uvumilivu . Walipotolewa na UD Songo hatua za awali kabisa klabu bingwa Afrika, walikaa chini kama klabu na kama timu na kukubaliana kutokuvurugana kutokana na hali hiyo na kujikita katika ligi na kocha wao huyo huyo na sote tunaona Simba wanavyoshinda kila mechi katika ligi hivi sasa.

Yanga leo mnaweza kumuondoa Zahera lakini bado akaja mwingine kazi ikawa ngumu. Kwanza kabisa mnatakiwa kujiweka sawa katika mfumo bora wa kuendesha timu , mfumo ambao utatoa matunda chanya.

Zahera aligundua udhaifu wa mfumo wa Uongozi wa Yanga hadi kuna wakati akageuka yeye ndio kila kitu sasa haya si makosa ya kocha bali mfumo na Zahera hapa ni kafara tu.

Bado katika mizani kiufundi huyu kocha ni mzuri tu sema tayari wanachama , baadhi ya viongozi na wachezaji wameingiziwa kirusi cha kumuona kocha mbaya hivyo kila afanyalo linakwenda mrama.

Ni vyema kuijenga klabu yote ili atakapokuja Zahera mwingine akose la kuongea kama watangulizi wake . Nimalizie kwa quote ya Bob Marley ;

“Unapotaka kutoa tiba fikiria kwanza kinga“ Bob Marley 1977

Samuel Samuel
IMG-20191029-WA0005.jpeg
IMG-20191029-WA0015.jpeg
 
Uzuri ni kwamba Yanga inaongozwa na wanasiasa akina mwakalebele.
Unaamua kupeleka mechi mwanza kisa tu utani wa mashabiki kusema Simba itakua ilifukia kitu uwanja wa Taifa.
Badala ya kuangalia mapungufu ya timu ili yarekebishwe. Timu inaanza kuendeshwa kwa imani za kishirikina.
 
Samuel SamuelView attachment 1247672View attachment 1247673
Umeandika vizuri ila kusema Simba ina mfumo mzuri sio kweli..MO mpaka leo hajaweka 20B mezani...anatoa fedha zake mfukoni kuendesha timu kuna tofauti gani na wakati wa Manji Yanga...Manji alitaka kununua nyumba 50 maeneo ya jangwani ili ajenge Jangwani city..arena kubwa ila serikali ikamnyima kibali cha ujenzi...angalia vizuri mechi za VPL Simba alafu angalia mechi za VPL za Yanga...vitimu vinakamia sana mechi za Yanga alafu za Simba wanakimbiakimbia tu...Simba wanacheza mchezo mchafu wakisaidiwa na TFF na liko wazi msimu uliopita Yanga waliporwa points 10 kimkakati mpaka Zahera akalia sana...hata mechi ya raundi ya pili Yanga vs Simba kuna mabeki watatu wa Yanga walitoka kambini usiku bila ya kocha kuambiwa...Simba chezeni mpira ndio maana mlipoamua kucheza mpira bila ya figisu mkatolewa awali CAF champions...
 
Yani endeleeni kuota ndoto ka hizo mkiamka mnakuta Simba bingwa
 
Tuache kutafuta visingizio kwamba mnafanyiwa figisu na Simba,mpira hauchezwi chumbani,Yanga ukiangalia mechi zake haieleweki hata inacheza mfumo gani,tuwe wakweli timu haiko vizuri na Zahera hawezi kukwepa hizi lawama licha ya mapungufu ya uongozi pia,jaribu tu kuangalia pamoja na Simba kutolea hafua za awali lakini ukiangalia performance yao walicheza vizuri tu tofauti na Yanga!
 
Umeandika vizuri....nimewahi kuandika humu kuwa tatizo kubwa ni kuwa Yanga ina viongozi karibu wote wageni na hawajui 'saikolojia' ya soka...mpira unachezwa nje asilimia 60 na ndani ya uwanja asilimia 40....Simba nimabingwa wa mikakati hii...Yanga kuna baadhi na hasa baadhi ya viongozi ni wapiga kelele tu...Simba wana mtu mmoja mpiga kelele kwa vvita vya kisaikolojia lakini wana watu makini wasiozidi sita wanaofanya mipango yote ...Yanga kumerundikana watu wenye hulka ya misifa nakuvujisha siri za timu..
 
Tuache kutafuta visingizio kwamba mnafanyiwa figisu na Simba,mpira hauchezwi chumbani,Yanga ukiangalia mechi zake haieleweki hata inacheza mfumo gani,tuwe wakweli timu haiko vizuri na Zahera hawezi kukwepa hizi lawama licha ya mapungufu ya uongozi pia,jaribu tu kuangalia pamoja na Simba kutolea hafua za awali lakini ukiangalia performance yao walicheza vizuri tu tofauti na Yanga!
kweli mkuu...football ni mchezo wa wazi...hata chama langu Chelsea kipindi cha sarri Alonso aliflop mashabiki wakapiga kelele kocha ampumnzishe akawapuuza, timu ikawa inachezea vichapo...alivyomuweka bench Alonso na timu ikaanza kushinda.
Mashabiki na wanachama wa yanga wasipuuzwe...timu hata pass 3 haipigi...shishimbi siyo technical midfielder...kwanin amchezeshe namba 10 hata killing pass kupiga utata!....
 
Umeandika vizuri ila kusema Simba ina mfumo mzuri sio kweli..MO mpaka leo hajaweka 20B mezani...anatoa fedha zake mfukoni kuendesha timu kuna tofauti gani na wakati wa Manji Yanga...Manji alitaka kununua nyumba 50 maeneo ya jangwani ili ajenge Jangwani city..arena kubwa ila serikali ikamnyima kibali cha ujenzi...angalia vizuri mechi za VPL Simba alafu angalia mechi za VPL za Yanga...vitimu vinakamia sana mechi za Yanga alafu za Simba wanakimbiakimbia tu...Simba wanacheza mchezo mchafu wakisaidiwa na TFF na liko wazi msimu uliopita Yanga waliporwa points 10 kimkakati mpaka Zahera akalia sana...hata mechi ya raundi ya pili Yanga vs Simba kuna mabeki watatu wa Yanga walitoka kambini usiku bila ya kocha kuambiwa...Simba chezeni mpira ndio maana mlipoamua kucheza mpira bila ya figisu mkatolewa awali CAF champions...
Umeandika utumbo uliooza
 
Hata umtetee Mwinyi Zahera kiasi gani, lakini ukweli ni kwamba hawezi kukwepa lawama! Usajili wa dirisha dogo, ni kweli alishindwa kufanya usajili kwa sababu ya changamoto za kifedha!

Lakini msimu ulipokwisha, tulijulishwa ya kwamba usajili wote uliofanyika kwenye timu, ulitokana na mapendekezo ya mwalimu!

Sasa mtoa mada, unaweza ukatuambia ni wachezaji gani wa ndani ambao mwalimu aliwahitaji na uongozi ukashindwa kuwasajili?

Mimi lawama zangu nazipeleka kwa Mwinyi Zahera, Kamati ya usajili na viongozi wa timu! Hawa wote wanahusika kuwasajili wachezaji wengi wa kawaida na ambao siyo tishio kwa timu nyingine.

Ukiwaangalia Simba, unaona kabisa kuna kitu kimefanyika ingawa na wenyewe wamepoteza baadhi ya wachezaji wao muhimu kama James Kotei na Emmanuel Okwi. Wachezaji wao wanapambana vilivyo ndani ya uwanja na wana uchu wa mafanikio, kuliko wale wa Yanga!
 
Uzuri ni kwamba Yanga inaongozwa na wanasiasa akina mwakalebele.
Unaamua kupeleka mechi mwanza kisa tu utani wa mashabiki kusema Simba itakua ilifukia kitu uwanja wa Taifa.
Badala ya kuangalia mapungufu ya timu ili yarekebishwe. Timu inaanza kuendeshwa kwa imani za kishirikina.
Mwakalebela baada ya Ccm kumtosa kaamua kujikita Yanga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom