Mwinyi: Viongozi wa dini mnanuka!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,954
287,541
Mwinyi-Viongozi wa dini mnanuka
Imeandikwa na Halima Mlacha; Tarehe: 11th October 2011 @ 20:00

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, amesema viongozi wa dini kutoka Tanzania wanatia aibu na kuchangia Watanzania kunuka nje ya nchi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.

Mzee Mwinyi alitoa kauli hiyo jana mbele ya viongozi hao na kusimulia mkasa uliomkuta yeye binafsi wa kupekuliwa kupita kiasi katika kiwanja cha ndege nje ya nchi, akishukiwa kuwa kiongozi wa dini kutoka Tanzania anayesafirisha dawa za kulevya.

Alikuwa akizindua Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Athari za Dawa za Kulevya jana Dar es Salaam katika hafla iliyoandaliwa na asasi ya kiraia ya American International Health Alliance (AIHA).

“Ninachokisema kuna maneno mengi ya aibu yanasemwa kuhusu Watanzania, aibu zaidi hata kwa wacha Mungu wa Tanzania sasa hawaaminiki, wanatumia fursa walizonazo kuficha na kusafirisha dawa za kulevya.

“Nilikuwa naenda Ujerumani hivyo nililazimika kubadili ndege katika moja ya nchi huko ughaibuni, wakati wa kupanda ndege ya pili tukaanza kukaguliwa. Ilipofika zamu yangu, nilikaguliwa sana, lakini hawakutosheka, nikaingizwa kwenye chumba cha pembeni, nikavuliwa viatu na koti wakanikagua kwa mashine na mwisho wakanipapasa mwili mzima,” alisema Mzee Mwinyi.

Alisema alikumbana na kadhia hiyo pamoja na hadhi yake ya kidiplomasia kwa vile tu alikuwa ameshikilia tasbihi (rozari) mkononi, jambo lililofanya ahisiwe kuwa ni kiongozi wa dini anayesafirisha dawa za kulevya.

“Yule aliyenikagua alikuwa akifanya kazi yake, amenifundisha, lakini nataka mjue Watanzania wenzangu kuwa tunanuka huko nje,” alisema Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa wakati wa utawala wake.

Mzee Mwinyi alilazimika kutoa mkasa huo uliompata miaka mingi iliyopita bila kutaja mwaka wala uwanja husika mbele ya viongozi hao wa dini mbalimbali ili kufikisha ujumbe kwao kuwa Tanzania inanuka kwa kuhusishwa na dawa za kulevya.

Alisema mmoja wa wasaidizi wake alijaribu kumnusuru katika hali hiyo kwa kumtahadharisha ofisa wa uwanja huo wa ndege kuwa huyo anayemkagua ni mwanadiplomasia.

“Lakini bwana yule alimjibu tena kwa ukali ‘I don’t care’ (sijali), wakaendelea kunikagua wanavyotaka baadaye nikajiuliza kwani imekuaje wakanikagua vile, nikagundua kuwa ni kwa vile nimebeba tasbihi,” alisimulia Mzee Mwinyi.

Alisema alionekana kama mwanadini anayetumia alama ya tasbihi ili apitishe dawa za kulevya kirahisi, jambo ambalo lilimsikitisha na wakati anaondoka uwanjani hapo, alilazimika kumkabidhi yule ofisa aliyemkagua tasbihi yake kama zawadi.

Kauli hiyo ya Mzee Mwinyi, imetolewa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa dini kukemea uhalifu huo na kutahadharisha kuwa sasa biashara hiyo imeaanza kuvutia viongozi wa dini.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, kwenye ibada maalumu ya kupewa kuwekwa wakfu Mhashamu Askofu John Ndimbo wa Jimbo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kunakuwa na sheria moja yenye nguvu itakayoziba mianya yote inayojitokeza katika sheria za dawa za kulevya.

Alisema kwa sasa sheria zilizopo zina mianya mikubwa ambayo inasababisha mapapa wa biashara hiyo na vipapa vidogo vinavyokamatwa kuishia kulipishwa faini ya Sh. milioni moja na kutoka.

“Sheria inasema wazi ukikamatwa na dawa za kulevya unalipishwa mara tatu ya gharama ya mzigo wa dawa hizo, kifungo cha miaka 30 au maisha lakini hivi kweli mmeshawaona watu wakifungwa kwa kosa hilo, lazima kuwe na marekebisho katika sheria hizi,” alisema

Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, alisema kikosi kazi maalumu kilichopo chini ya Tume hiyo kimekamata watu wengi wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.

Takwimu zinaonesha mwaka 2008 hadi mwaka huu, watuhumiwa 22,814 walikamatwa nchini na 67 nje ya nchi huku idadi ya dawa zilizokamatwa ikiongezeka.

Kwa mujibu wa Shekiondo, dawa zilizokamatwa zimeongezeka kutoka heroine kilo 100 kutoka mwaka 2000 hadi 2009 hadi kilo 154 mwaka jana na mwaka huu; na cocaine kilo 57 mwaka 2000 hadi 2009 hadi kufikia kilo 191 mwaka 2010 hadi mwaka huu.

Baraza hilo la Viongozi wa Dini kazi yake ni kuhamasisha vijana kuepuka biashara na matumizi ya dawa za kulevya na linaongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum.

 

RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
Kwa nyakati zetu hizi, kushikilia tasbihi kwenye uwanja wa ndege ni ishara ya ugaidi na hivyo kushitukiwa ni dhahiri! Mahali popote duniani tasbihi mkononi zinashitukiwa! Wanajua ndio swala yako ya mwisho kisha ujilipue ili ukafaidi mabikira huko ahera! Waislamu hata kama ni diplomats na viongozi wa dini hawaaminiwi tena kwa sababu ya kujihusisha na ugaidi na biashara ya madawa ya kulevya!
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
huyu mzee kila akisogea kwenye microphone huwa anaongelea mambo ya kukuza na kuendeleza uislam tu.

hasemi lolote kuhusu masuala ya nchi ambayo yanaathiri maisha ya watanzania wote bila kujali dini zao.
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,438
8,380
Ile List ya Wauza MAdawa ya Kulevya na Watumiaji ingewekwa wazi wautuhumiwa wangeshtakiwa na kumalizwa harufu isingenuka sana duniani kuwa tz imegeuka kituo cha kupitisha madawa majuzi nilikuwa airport mzigo kidogo ulizidi weight bongo wakataka rushwa wenye ndege turkish amani Rushwa husababisha yote haya Haikemewi hadi ukaona sura ya anaeikemea kama anamaanisha
 

The dirt paka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
371
65
Mzee yuko kiitikadi sana unadhani kila mtu akianzd kusimama na kuipromoti dini yake katika masuala ya kitaifa na kisiasa nini kitafuata?
Kunuka kukizidi wagawe manukato na marashi ya pemba katika kampen zao lakini kuna jambo huyu mzee halielewi kuwa ni heri ajivike kandambili kuustiri mwili wake kuliko kupoteza muda kujaribu kuipamba dunia kwa carpet.
 

Jituoriginal

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
363
30
Huyu babu hana sifa ya kuwaponda viongozi wa dini kwani nani asiyeyajua wa Mama sitti na mzee Lyatonga.
 

ngwini

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
482
89
huyu mzee kila akisogea kwenye microphone huwa anaongelea mambo ya kukuza na kuendeleza uislam tu.

hasemi lolote kuhusu masuala ya nchi ambayo yanaathiri maisha ya watanzania wote bila kujali dini zao.

acha kuropoka..hapo amezungumzia uislam wap? Kazungumzia dini kwa ujumla.
 

SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Ninashaka kama viongozi wa madhehebu yote ya dini walihudhuria semina hiyo, kwani naona kama ilikuwa ni kausanii fulani hivi.
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
35,167
35,067
wawataje kuna nini wanachoogopa, inawezekana viongozi wanapewa % ndo maana wanaogopa kuwataja, tumechoka kusikia viongozi wa dini, kwani hawana majina???????????
 

kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,350
279
Hao viongozi wa dini ni akina nani? maana ishakuwa chorus sasa,,,,,,,,
Wataje majina yao kama hawawezi wakae kimya
 

NASSOR

Member
Jun 29, 2011
7
2
Mnapojqadili suala muhimu jaribuni kuondoa udini yaani kila mtu anafikiria dini yake.
Hapa ninachokiona ni jazba za watu na dini zao, kuna viongozi wa dini wanashughulika na madawa ya kulevya lakini watu hawataki wanan'gan'gania uislamu.
Jadili madawa ya kulevya utaona dini zote mbili wanahusika na madawa ya kulevya
 

RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
Mnapojqadili suala muhimu jaribuni kuondoa udini yaani kila mtu anafikiria dini yake.
Hapa ninachokiona ni jazba za watu na dini zao, kuna viongozi wa dini wanashughulika na madawa ya kulevya lakini watu hawataki wanan'gan'gania uislamu. Jadili madawa ya kulevya utaona dini zote mbili wanahusika na madawa ya kulevya
Sasa si uwataje?
 

Mrdash1

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,378
331
Mnapojqadili suala muhimu jaribuni kuondoa udini yaani kila mtu anafikiria dini yake.
Hapa ninachokiona ni jazba za watu na dini zao, kuna viongozi wa dini wanashughulika na madawa ya kulevya lakini watu hawataki wanan'gan'gania uislamu.
Jadili madawa ya kulevya utaona dini zote mbili wanahusika na madawa ya kulevya

Wakiristo siku zote wamesema hao viongozi wa dini watajwe hadharani, hakuna kiongozi wa kiislam aliyetoa kauli kama hiyo. wakiristo wako wazi lakini waislam iko janja na danganya danganya sana
 

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Huyu Mdini kachanganyikiwa nini? au anajaribu ku-netralise maneno ya Kikwete maana wanajuwa hasira za Maaskofu juu ya Kikwete na CCM maana tokea Kikwete awatukane maaskofu hadi leo ameshindwa kuthibitisha maneno yake badala ya kutapatapa bila ushahidi na hatua yoyote.

Sasa wanamtumia Mwinyi ilionekane kuwa ni dini zote viongozi wake wana nuka, hii haisaidi labda Kikwete atubu aombe samahani kwa kuwatukana Maaskofu lasivyo laana yake bado itaendelea kuila CCM kama ukoma. Mwinyi anajuwa CCM ikifa leo yeye na wanae na Rizi ndio waathirika wa kwanza hivyo lazima ajiingize katika sakata hili, ila ajue kuwa mimi ninavyojuwa Maaskofu hasa wa kikatoriki ni wasomi na wanavyombo vyao ndani na nje ya nchni wanaweza kujuwa na kung'amua kuwa Mwinyi anafanya hadaa na kejeli kama alivyofanya Kikwete kuwaambia Maaskofu kuwa wanauza madawa ya kulevya, tunasubiri saa na tarehe ambayo Kikwete atagumdua kosa lake na kuomba samahani lasivyo bado na bado.
 

Wed

JF-Expert Member
Mar 7, 2011
315
266
Yapo mambo mawili hapa.

1. Huyu Mzee alikaguliwa kwa ajli ya TASBIHI yake mkononi - walimthania ni mlipua mabomu.

2. Mbona hajawakemea BAKWATA wananuka kwa kuhongwa pilau ili waisaidie CCM kushinda kura kama ilivyotokea kule Igunga ?
 

Mzelokotwa

Member
Aug 14, 2011
21
6
Hii ni dharau kubwa sana dhidi ya uafrika, huu ni ubaguzi wa rangi, mzee wetu amedharirishwa kupita kiasi, mzee Mwinyi ni rais mstaafu wa tanzania na dunia nzima inajua.Anapodharirishwa kiongozi wetu nasi kama watanzania tumedharirishwa pia, badala ya kuijadili kwa kina tunaishia kujificha kwenye kichaka cha dini! hayo waliyo fanya kwa mzee wetu wanaweza kuyafanya kwa Clinton? Aibu.........!
 

Fasir

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
222
267
Yapo mambo mawili hapa.

1. Huyu Mzee alikaguliwa kwa ajli ya TASBIHI yake mkononi - walimthania ni mlipua mabomu.

2. Mbona hajawakemea BAKWATA wananuka kwa kuhongwa pilau ili waisaidie CCM kushinda kura kama ilivyotokea kule Igunga ?
Hoja muflis na inaakisi upeo wako mdogo... Cha ajabu zaidi kuna viumbe wanakuita baba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom