Mwinyi Kazimoto awaomba radhi Watanzania

Mwinyi Kazimoto awaomba radhi Watanzania

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,519
Katika ukurasa wake wa Twita, Kiungo mahiri wa timu ya Simba na timu ya Taifa Mwinyi Kazimoto amewaomba radi Watanzania wote kwa kosa la kutoroka katika kambi ya timu ya Taifa,

Namnukuu hapa:

"Nikweli nimefanya makosa. Nikatika harakati zakutafuta maisha tu! Naomba WATANZANIA wezangu wanisamehe."

NB

Sisi sote ni binadamu hakuna aliyemkamilifu, ukosefu ni sehemu ya maisha ya binadamu, na aombae samahani amelijua na kujutia kosa lake,

Tumsamehe kijana wetu na arudi kulitumikia taifa letu na klabu yetu!
 
Angelikuwepo na asingelikuwepo yote sawa...hana kiwango cha kutisha kiasi kwamba pengo lake lilionekana.
Ningelikuwa ni Kim, huyo bwa mdogo habari za timu ya Taifa angezisikia na kusoma magazetini.
 
Mwinyi Kazimoto!kila la kheri!maana mpira wa bongo hauna future nzuri usipowekeza!tunakusamehe bure ila nidhamu mbele huko uendako!
 
Angelikuwepo na asingelikuwepo yote sawa...hana kiwango cha kutisha kiasi kwamba pengo lake lilionekana.
Ningelikuwa ni Kim, huyo bwa mdogo habari za timu ya Taifa angezisikia na kusoma magazetini.

hujamsamehe wewe. Kumbuka kusamehe na kusahau.
 
Sioni kosa lake. Mbona hata alipo kuwepo taifa star ilikuwa inafunga so tff isitaka kumbebesha lawama eti ndiye kasababisha timu kufungwa. Hata asingeomba msamaha sawa tu. Mia
 
Huyo ni kum replace na mmoja wa serengeti boy ili asiendelee kujidangaya kuwa ana kiwango kumbe kaisha tu.
 
Asamehewe, na adhabu stahiki apewe. iwe na simba au tff, ili iwe fundisho kwa wengine.
Haina haja ya kubembelezana wakati nchi ina vipaji kibao, kazi kung'ang'ania hao hao kila siku, ndio mana tunarud nyuma bdala ya kwenda mbele.
 
Simba si ilimfungia na baadhi ya mashabiki wakasema anacheza chini ya kiwango,wampe kibali tu
"Vox populi,Vox dei"
 
Hivi kuchezea timu ya taifa ni masilahi au heshima?
 
Huyo ni kum replace na mmoja wa serengeti boy ili asiendelee kujidangaya kuwa ana kiwango kumbe kaisha tu.
Ni vigumu nchi hii kwani wachezaji wake hawachaguliwi na kocha bali viongizi hivo hata huyu dogo kule alikoenda kapelekwa na kiongozi wake.
 
Kosa lake ni kuikimbia nchi akiwa ni miongoni mwa askari warioteuliwa kuipigania nchi kufuzu chan. ila ukweli ni kwamba hata kama angekuwepo asingebadili matokeo kwa kuwa uwezo wake umeshuka mno. Ni jukumu la TFF na Kim kuangalia na uwezo wa wachezaji wachanga. Msameheni huyo mwinyi akajiandalie maisha yake maana soka letu tunalijua wenyewe. Usipochacharika utaishia kuchoma mahindi baada ya kustaafu soka.
 
Asamehewe, na adhabu stahiki apewe. iwe na simba au tff, ili iwe fundisho kwa wengine.
Haina haja ya kubembelezana wakati nchi ina vipaji kibao, kazi kung'ang'ania hao hao kila siku, ndio mana tunarud nyuma bdala ya kwenda mbele.

Amefanya kosa akiwa timu ya Taifa, TFF imfungie kucheza boli ndani na nje ya nchi kwa mwaka mmoja tu, atakuwa amekwisha milele hadi kaburini.
 
Kwani alipoondoka aliwaaga Watanzania kwenye twitter? Kama ana nia kweli ya kuwaomba radhi Watanzania wenzake, angetafuta chombo cha habari kinachowafikia Watanzania wengi, Watanzania wangapi kati ya aliowasaliti wana akaunti za titter? Hajaomba radhi bado, kwa hilo mimi na wengi wenye mawazo kama yangu si Watanzania wenzake. Watanzania wenzake kwenye hili ni hao waliompandisha mkenge, ambao hana haja ya kuwaomba msamaha, maana ni wasaliti wenzake.
 
Back
Top Bottom