Mwinyi ataka wacha Mungu waongoze taifa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Mwinyi ataka wacha Mungu waongoze taifa
Send to a friend
Sunday, 21 August 2011 21:36

07mwinyi.jpg
Ibrahim Yamola
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema nchi inatakiwa kuongozwa na viongozi wanaofuata maadili ya dini.Kauli ya Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa inakuja kipindi ambacho nchi inatikiswa na matukio makubwa ya ufisadi na ukiukaji maadili ya uongozi wa umma.Akizungumza kwenye hafla ya mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu yaliyoshirikisha nchi 10 za Afrika yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Mzee Mwinyi alisema kiongozi mwenye maadili ya dini ataongoza kwa kumuogopa Mungu.

“Ili kuwapata viongozi waliokuwa wema na wenye kuongoza kwa usawa na haki, ni lazima watoke katika maadili ya kidini,” alisema Mwinyi.Alisema sababu za kuwapata viongozi wenye maadili ya kidini ni kwamba wataongoza kwa kumwogopa Mungu na hawatafanya kama wajuavyo.

Alisisitiza: “Viongozi watakuwa wanaongoza kwa kumwogopa Mungu, hivyo kuwa na usawa na kuleta maendeleo katika taifa letu.” Katika hafla hiyo, Mwinyi aliwataka wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo kwani huo ni wajibu wa kila mwananchi.“Kila mtu anao wajibu wa kuchangia maendeleo ya Tanzania na siyo ombi. Ni lazima kwa kila mtu kuonyesha juhudi binafsi ili kuliweka taifa letu sehemu nzuri ya maendeleo,” alisema Mwinyi.

Rais huyo wa zamani alisema hata mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu wakuu wacha Mungu watafanya kazi yao kwa kumwogopa Mungu na njia mojawapo ya kuwapata ni kuhifadhi Qur’an tukufu.

Mara baada ya kuwataja makatibu wakuu katika orodha ya viongozi wanaotakiwa kuwa na maadili ya ki-Mungu, watu waliohudhuria hafla hiyo waliangua kicheko na kumlazimu kukatisha hotuba yake hiyo na kusema: “Kwa kuwa nia yangu ilikuwa kumkaribisha mgeni rasmi tu hivyo ngoja nimwachie nafasi aje kutoa nasaha zake.”
Mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal aliwataka Waislamu kutumia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kusoma na kuielewa Qur’an tukufu.

Dk Bilal aliwataka wanazuoni wa Kiislamu nchini kutafsiri na kufikisha mafunzo ya Qur'an tukufu kwa jamii yote.
Ujumbe katika kitabu hicho kitukufu, alisema unaweza kuleta tofauti kubwa katika jamii kama utaeleweka vema na kufuatwa, akawaonya Waislamu kuacha kupoteza muda kwa kupiga domo badala yake waketi chini na kuisoma na kuielewa Qur'an.

“Ni lazima tutenge muda kuisoma na kuishi kwa misingi ya Qur'an. Tunakosa baraka nyingi za Mwenyezimungu kwa kuacha kufanya hivyo ... kitabu kinaamrisha upendo na haki kwa wote,” alisema Dk Bilal.

Awali, Mratibu wa Mashindano hayo, Othman Kaporo alisema mashindano hayo yalianza kufanyika tangu mwaka 1995 yakishirikisha wakazi wa Dar es Salaam pekee.

“Tulianza kwa kuwahusisha washiriki kutoka Mkoa wa Dar es Salaam pekee, lakini mwaka jana nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki zilihusika na kwa mwaka huu tumeshirikisha nchi 10 za Afrika,” alisema.
Kaporo alizitaja nchi zilizoshiriki mashindano hayo ni Ethiopia, Sudan, Kenya, Msumbiji, Uganda, Nigeria, Burundi, Somalia, Misri na wenyeji Tanzania.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha washiriki wavulana wenye umri kati ya miaka 15-18. Mshiriki kutoka Sudan Juhuddin Adam alishika nafasi ya kwanza na kupata zawadi ya Sh5 milioni.Mshiriki kutoka Zanzibar, Kombo Bahi Makame alishika nafasi ya pili na kupata zawadi ya Sh3 milioni na mshiriki kutoka Misri Mohammad Sad Tawfiq alishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh2 milioni.

Alisema ni wakati sasa umefika kwa wazazi kuweka kipaumbele katika elimu ya dini ili kuwapata viongozi watakaokuwa na maadili na kuwa na jamii inayomwogopa Mungu

“Kama tutawalea vizuri watoto wetu kwa kuwapa elimu ya kidini, tutakuwa na jamii yenye maadili bora kwani hivi sasa tunaona wenyewe jamii yetu inakoelekea” alisema Kaporo.

Tizameni watanzania kila watu fulani wanapochukua dola kunakuwa na sintofahamu nyingi kwa hiyo tutafute ni mungu gani? Mzee ruksa anasema
 
Angemalizia basi mungu yupi anayetakiwa abudiwe na hao waongozaji? Kuachia tu kauli hewani nayo inaleta utatazaidi, hata hivyo yule kijana alisha muhukumu tumsamehe. Uko kwenye shughuli ya dini fulani halafu unaongea kauli kama hizi iliueleweke vipi? Kazi ipo.
 
mungu gani huyo wamche?
maana kama ni misikitini, makasani na mibuyuni hawa watu wanaenda ati?
wengine hata kwa kina sangoma wanatinga na wanawategemea sana kama miungu yao?
 
Pengine tunahitaji kuichambua hotuba ya Mwingi kwa makini.
Alikuwa anamaanisha nini hasa alipoyasema haya?
 
Hongera mzee wetu kwa kuliona hili,hali ilivyo sasa ni mbaya.Sio siri kwamba waabudu shetani wamekamata nchi,na tusipoamka watatumaliza.
Mwinyi ataka wacha Mungu waongoze taifa
Send to a friend
Sunday, 21 August 2011 21:36

07mwinyi.jpg
Ibrahim Yamola
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema nchi inatakiwa kuongozwa na viongozi wanaofuata maadili ya dini.Kauli ya Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa inakuja kipindi ambacho nchi inatikiswa na matukio makubwa ya ufisadi na ukiukaji maadili ya uongozi wa umma.Akizungumza kwenye hafla ya mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu yaliyoshirikisha nchi 10 za Afrika yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Mzee Mwinyi alisema kiongozi mwenye maadili ya dini ataongoza kwa kumuogopa Mungu.

“Ili kuwapata viongozi waliokuwa wema na wenye kuongoza kwa usawa na haki, ni lazima watoke katika maadili ya kidini,” alisema Mwinyi.Alisema sababu za kuwapata viongozi wenye maadili ya kidini ni kwamba wataongoza kwa kumwogopa Mungu na hawatafanya kama wajuavyo.

Alisisitiza: “Viongozi watakuwa wanaongoza kwa kumwogopa Mungu, hivyo kuwa na usawa na kuleta maendeleo katika taifa letu.” Katika hafla hiyo, Mwinyi aliwataka wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo kwani huo ni wajibu wa kila mwananchi.“Kila mtu anao wajibu wa kuchangia maendeleo ya Tanzania na siyo ombi. Ni lazima kwa kila mtu kuonyesha juhudi binafsi ili kuliweka taifa letu sehemu nzuri ya maendeleo,” alisema Mwinyi.

Rais huyo wa zamani alisema hata mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu wakuu wacha Mungu watafanya kazi yao kwa kumwogopa Mungu na njia mojawapo ya kuwapata ni kuhifadhi Qur’an tukufu.

Mara baada ya kuwataja makatibu wakuu katika orodha ya viongozi wanaotakiwa kuwa na maadili ya ki-Mungu, watu waliohudhuria hafla hiyo waliangua kicheko na kumlazimu kukatisha hotuba yake hiyo na kusema: “Kwa kuwa nia yangu ilikuwa kumkaribisha mgeni rasmi tu hivyo ngoja nimwachie nafasi aje kutoa nasaha zake.”
Mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal aliwataka Waislamu kutumia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kusoma na kuielewa Qur’an tukufu.

Dk Bilal aliwataka wanazuoni wa Kiislamu nchini kutafsiri na kufikisha mafunzo ya Qur'an tukufu kwa jamii yote.
Ujumbe katika kitabu hicho kitukufu, alisema unaweza kuleta tofauti kubwa katika jamii kama utaeleweka vema na kufuatwa, akawaonya Waislamu kuacha kupoteza muda kwa kupiga domo badala yake waketi chini na kuisoma na kuielewa Qur'an.

“Ni lazima tutenge muda kuisoma na kuishi kwa misingi ya Qur'an. Tunakosa baraka nyingi za Mwenyezimungu kwa kuacha kufanya hivyo ... kitabu kinaamrisha upendo na haki kwa wote,” alisema Dk Bilal.

Awali, Mratibu wa Mashindano hayo, Othman Kaporo alisema mashindano hayo yalianza kufanyika tangu mwaka 1995 yakishirikisha wakazi wa Dar es Salaam pekee.

“Tulianza kwa kuwahusisha washiriki kutoka Mkoa wa Dar es Salaam pekee, lakini mwaka jana nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki zilihusika na kwa mwaka huu tumeshirikisha nchi 10 za Afrika,” alisema.
Kaporo alizitaja nchi zilizoshiriki mashindano hayo ni Ethiopia, Sudan, Kenya, Msumbiji, Uganda, Nigeria, Burundi, Somalia, Misri na wenyeji Tanzania.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha washiriki wavulana wenye umri kati ya miaka 15-18. Mshiriki kutoka Sudan Juhuddin Adam alishika nafasi ya kwanza na kupata zawadi ya Sh5 milioni.Mshiriki kutoka Zanzibar, Kombo Bahi Makame alishika nafasi ya pili na kupata zawadi ya Sh3 milioni na mshiriki kutoka Misri Mohammad Sad Tawfiq alishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh2 milioni.

Alisema ni wakati sasa umefika kwa wazazi kuweka kipaumbele katika elimu ya dini ili kuwapata viongozi watakaokuwa na maadili na kuwa na jamii inayomwogopa Mungu

“Kama tutawalea vizuri watoto wetu kwa kuwapa elimu ya kidini, tutakuwa na jamii yenye maadili bora kwani hivi sasa tunaona wenyewe jamii yetu inakoelekea” alisema Kaporo.

Pengine tunahitaji kuichambua hotuba ya Mwingi kwa makini.
Alikuwa anamaanisha nini hasa alipoyasema haya?

Bahada ya kuona hali ya nchi inavyokwenda. kila sehemu ndani ya nchi kunanuka ufisadi. Huku maisha ya wananchi wa kawaida yakiendelea kuwa magumu.
 
Alipokuwa pale magogoni kipindi chake single za aina hii usingetegea kutoka kwenye kinywa chake wakati huo sitti mwinyi anajihusisha na biashara za madini na uingizaji nchini kwa bia ya aina ya stella wakati huo hakuwa na Mungu,anaibuka na maneno hayo saa hizi,ndio maana wachangiaji wanauliza Mungu yupi??????unafiki tu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
"When the righteous are in authority, the people rejoice: but when the wicked beareth rule, the people mourn." (Proverbs 29:2).
 
Hivi Tanzania sasa hivi inaongozwa na WAPAGANI? What exactly is this Mzee talking about?

I dont care kama mtu anamcha mungu au anatema mate, all I care ni kiongozi mwenye vision na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu guided by the law of this country. Hii habari ya mungu ni visingizio, wengine walituambia tumepata chaguo la mungu, look where we are now? Au mungu katugeuka?
 
Hongera mzee wetu kwa kuliona hili,hali ilivyo sasa ni mbaya.Sio siri kwamba waabudu shetani wamekamata nchi,na tusipoamka watatumaliza.
<br />
<br />
sijui na wazinifu wakishika nchi itakuwaje
 
Mie ninadhani alikuwa akiliongelea hili suala kwa ujumla. kwa imani yangu dini ya kweli ni ile inayohubiri amani ambayo ni matokeo ya uwepo wa haki na usawa. kama kuna dini nyingine inayosisitiza ufisadi hilo bado sijalifahamu
 
Hivi Tanzania sasa hivi inaongozwa na WAPAGANI? What exactly is this Mzee talking about?

"They honour Me with their lips but their hearts are far from Me..............their fear toward Me is taught by Commandment of men." Isaiah 29:13 & Mark 7:6

tunahaki ya kujiuliza huyu Mungu ni yupi?..................mbona hawa mafisadi nao wanaamini kuwa wanamwabudu Mungu yule yule?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Jibu lipo kwenye Colossians 2:23 "These things indeed have an appearance of wisdom in self imposed religion, false humility and neglect of the body, but are of no value against the indulgences of the flesh."

dini hizi ni kauka ni kuvae waumini ni bora liende.....................wengi wetu tumekuwa tunaamini mali, ubinafsi na mengineyo ambayo hayana rutuba za kiroho............
 
Africa sijui ili laaniwa na nani Mungu wangu!! Hata wasomi ambao wana PhD bado ni wapumbavu na hawajaelimika hata kidogo! Mtu aliwa kuniambia kuwa wazungu wanapenda Waafrica wapumbavu na wakitokea wanasifiwa na kupewa kila aina ya sifa na hata wasomi wetu wa wazamani kichwani hakuna kitu ila walikuwa wanapewa PhD kulingana na upumbavu alionao nao; ukiwa mpumbavu ndio unaipata haraka kuliko ukionekana una akili sana maana walitaka kutekeleza azma yao ya kutu tawala kwa awamu ya pili haraka sana, sasa nime amini kabisa.

Huyu hafai tena kuitwa Dr na mimi binafsi si mtambui tena kama ni Dr, nitamuita ndugu Bilali kunzia leo. Nilitegemea kama kweli ame elimika na anataka waafrica wajitegemee kialiki na kifikra aseme Quran zitafsiriwe kwa kiswahili, Kizigua, Kichagga, Kimasai, Kikwere, na hata Kimang'ati kwa wingi ili watoto waweze kuisoma na kuielewa haraka na wasipotezewe muda wa kusumbuka na utumwa wa kukalili kiarabu! tena yeye kumbe ndio mtumwa wa kiakili kuliko kawaida?

Hawa ndio aina ya wasomi tulionao? Bure kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom