Mwingira anatimiza lile andiko la enzi za Ayubu kipenzi cha Mungu. Ayubu naye alisemewa mengi mabaya na marafiki zake ambao nao walikuwa wanapiga vifua vyao kwamba wanamjua Mungu sana kuliko hata Ayubu hao ni Eliphaz, Bildad na Zophar. Kumsema Ayubu walikuwa wanaegemea Jina la Mungu pia. Lakini mabishano yao hatimaye Mungu mwenyewe akajatoa hitimisho kwa kwaambia live watu hao kwamba wao ndio wamekosea na Ayubu ndiye aliyesema kweli kuhusu Mungu, akawarudi na kumpandisha juu sana chati Ayubu (Ayub 41:8-9) unaweza kusoma mlango mzima ukipata nafasi. Biblia Takatifu ambayo Mwingira anapata upofu kuiona inasema hivi: "Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwainua wanyenyekevu wa moyo"
Anayo haki kuongea Mwingira anayejiita Nabii na Mtume mfanya biashara maarufu nchini anayetumia nguvu kazi ya wale wanaomwendea kumsikiliza kwenye viunga vyake alivyowekeza, ambaye naambiwa anatembelea gari lenye zaidi ya milioni 200 katikati ya waumini wake masikini kabisa, akikusanya kila senti kutoka mifukoni mwao kwa jina la sadaka kwa Mungu na kujinufaisha yeye mwenyewe, akiwachukia wote wanaoinukia kutumiwa na Mungu kwa kuwa hawatoki kanisani kwake, akikandamiza uelewa wa walio chini yake wasijenyenyuka wakampita yeye. Anatafuta umaarufu huyo, anahofia watu watamkimbia naye atamasikinika haraka. Roho za namna hiyo zipo nyingi na zitaendelea kuja tu, kama Kakobe naye anavyolinganisha tiba ya Loliondo na DECI. Wanafiki hao wala hawafai kusikilizwa. Roho ya Mungu hijipiganishi yenyewe. Kama kweli watu hao ni watumishi waaminifu wa BWANA, wangekuwa na hekima angalau kidogo tu kukwepa kuingia kwenye mtego wa kutafuta na kujilimbikizia sifa. Sio sahihi kkwao kumhukumu babu na kumpangia adhabu ya kifo kwa kusema roho inayodaiwa na Ambilikile kutoka kwa Mungu ikimtuma afanye anachofanya kutibu watu ni ya kishetani. Wamekuwa kama panya wamenaswa kwenye mtego ilhali walidhani wao peke yao ndio wanatumiwa na Mungu kupeleka habari za kheri kwa viumbe vya Mungu. Si ajabu kama Mungu atakuwa amewakataa hao kama Sauli alivyokataliwa na Daudi asiyetegemewa akapakwa mafuta na kuwa mfalme wa Israel. Sauli hakutulia kimya akatafuta kila njia amwue Daudi, lakini kwa kuwa MUNGU alitoa kibali kwa Daudi akafa Sauli mwenyewe baada ya kuingia mkenge kumwinua Nabii Samwel kutoka kuzimu na kusemezana naye, akapata maneno asiyotarajia. Ndivyo Mwingira na Kakobe wanavyofuata nyayo za kale pasipo wao wenyewe kufahamu.
Kama kweli MUNGU ndiye aliyemruhusu Ambilikile Mwaisapila kufanya afanyayo, HAKIKA hatawaacha wamneneayo mabaya wadumu, bali atajilipiza kisasi kumtetea mja wake, kwa maana kisasi ni chake BWANA. Dhambi zote zinaweza kusamehewa, lakini kumkufuru Roho Mtakatifu KAMWE hasamehewi mtu, ndivyo KRISTO mwenyewe alivyoonya. Ikiwa Mwingira anamwamini KRISTO basi na ajitambue kwamba amepotea upeo, ajiangalie na kauli zake. Babu sijamsikia akihubiri watu waende kwake na wala hajitangazi ili watu wengi wamfuate. Wanaokwenda kutoa shukrani anawaambia waende kanisani kwao wanakosali wakatoe sadaka huko. Mwingira sasa naanza kuamini kwamba yanayosemwa kuwa jamii ya mateka wa kiroho inawezekana kuwa, kwa sababu kila anayemwamini Mungu anaweza kutenda dhambi sana tu lakini wanaogopa kumsema Mungu vibaya hata kwa utani. Jazba anayoitumia kumdhalilisha babu sio ya kawaida. Babu wala hajibu mapigo, anajua anachokifanya, yupo mtetezi wake atakayewashukia wabaya wake kama nyuki.
Tumwachie Mungu anayejua kujitetea. Mwingira na Kakobe wana maisha ya peponi wangali duniani, wanawazuia wengine waione baraka za Mungu kwa vitisho vingi, waumini wao masikiniiiiiii wanaonuka kwa umasikini huo, lakini wamekusanya kila kilicho cha thamani na kuwapelekea watu hawa ambao chai ya rangi ni historia kwao, wakati waumini wao hata hiyo chai ya rangi wakiipata wanadhani ni muujiza. Jamani, mimi sijui tunapelekana wapi. DECI wanayodai waliiombea kufa na ikafa wanakosea, it was a situational circumstance. Miongoni mwa walionufaika na DECI ni waumini wao na labda hata wao wenyewe hao waropokaji. Hawataki wengine waone paradiso wakingali duniani kama wanavyoifaidi wenyewe. Lakini ole wao, maana wataangukia pua wasipojichunguza na kumlilia Mungu awasafishe nia zao mbaya na kuachana na kiburi cha rohoni, wakajivisha nafasi ya Uungu kama Shetani alivyofanya na akatelemshwa kuzimu. Wanapohubiri wasisahau kujihubiri na wao wenyewe, hata Paulo Mtume wa Kweli alijisemea asijewahubiri wengine wakaenda mbinguni na yeye akakataliwa. Paulo aliliona hilo ambalo Mwingira na Kakobe bado wamepofushwa. Utamwombeaje mtu kufa wakati anachokifanya hata wapagani wanakiri kwamba Mungu yumo kwenye huduma hiyo? Watajitenganisha vipi na wayahudi waliobobea kidini waliomsaliti Yesu na kumwua? Hao ndio aina ya Mwingira na Kakobe. Ona Pengo anavyotoa maoni kwa mashaka, anajua ubaya wa kupingana na Mungu, anatoa maoni yake kwamba hana cha kusema ila anabaki kushangaa, kwani akili yake inapingana na imani yake na kwa hekima aliyopewa na Mungu anasita kusema vibaya juu ya huduma hiyo hadi Mungu atakapomdhihirishia ukweli.
Yatosha. Vipofu na waendelee kuwa vipofu, wenye macho na waendelee kuona, wanaomtafuta Mungu waongeze bidii na kumuuliza ukweli wa jambo hili naye atawajibu. ZIjaribuni kila roho.