Mwili wakaa mochwari zaidi ya siku 35, ndugu wagoma kuuchukua

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,555
Familia ya Bulole wa Miyuji jijini Dodoma wamegoma kuchukua mwili wa ndugu yao, Richard Bulole ambao upo chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa ya Dodoma tangu Agosti 13, 2022.

Sababu za kususia mwili huo zimetajwa kuwa wanataka ukweli kuhusu kifo cha ndugu yao ambaye taarifa zinadai kuwa aligongwa na gari la Magereza makao makuu lakini utata ni namna mwili huo ulivyokabidhiwa hospitalini.

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo leo Jumapili Agosti 18, 2022 mdogo wa marehem, Bulole Bukombe amesema wamebaini utata huo lakini kuna mambo mengine hawawezi kusema lakini vyombo vya dola vitaujua ukweli kama watachunguza.

Amedai kuwa walioupeleka mwili huo hawakupita mapokezi kuandikisha badala yake walikwenda moja kwa moja chumba cha kuhifadhia maiti ambako huko pia hawakuandika taarifa zozote kama ilivyo utaratibu.

Hata hivyo Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, Mzee Nyamka amesema hana taarifa kama gari la Magereza lilipeleka mwili huo tarehe tajwa.

“Nipo nje ya Dodoma, lakini sijawahi kupokea taarifa kama gari la magereza lilisababisha kifo, au lilipeleka mwili wa mtu hospitali hata kwa kuokotwa, waulizwe wengine,” amesema Nyamka.

Bukombe ametaja hofu waliyonayo wanafamilia ni kuwa hawajui chanzo cha kifo cha ndugu yao.

Amesema kama kweli wahusika waliuokota mwili huo barabarani wasingeweka usiri kama walivyofanya na hata hospitali wangeandika taarifa za kujitosheleza.

“Mashaka yetu ni kwa nini wanajificha, familia inatilia shaka, kama walikuwa na nia njema walishindwaje kuandikisha pale kabla ya kuuhifadhi na kueleza walikouchukua,” alihoji Bulole.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Ernest Ibenzi amekiri mwili huo kuwepo hospitali tangu Agosti 13, 2022 na kubainisha kuwa palikuwa na mapungufu mahali kutokana na kupokea mwili bila kuweka kumbukumbu sahihi.

Dk Ibenzi amesema mwili huo ulipelekwa na askari magereza waliokuwa na gari lakini uzembe ulianzia kwa watumishi ambao hawakurekodi tukio hilo kama ilivyo kawaida.

“Huwa tunapokea miili na majeruhusi kutoka kwa Polisi lakini muhimu kuandikisha, huyu inaonyesha hawakuandika sijui kwa kuwaamini au kuna nini lakini tunatumia kamera zetu kutambua gari iliyomleta,” amesema Dk Ibenzi.

Amesema kuwa wanaendelea kuwapa ushirikiano ndugu wa marehemu huku wakitaraji kupeleka picha ya gari iliyopeleka mwili huo kwa watu wa magereza ili wakatambue nani alikuwa dereva siku hiyo.

Mwananchi
 
Ingekuwa pande za kwetu wangesema alikuwa panya road.
 
Back
Top Bottom