Mwili wafukuliwa kutokana na kuzikwa kimakosa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwili wafukuliwa kutokana na kuzikwa kimakosa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Mwili wafukuliwa kutokana na kuzikwa kimakosaAdvertisement
  [​IMG]


  Monday, May 25, 2009 10:14 AM
  MWILI wa Jacob Sembeta [74] uliozikwa Wilayani Hai Kilimanjaro umefukuliwa baada ya kugunduliwa ulizikwa kimakosa sehemu si husika.Tukio hilo la aina yake lilitokea May 15, mwaka huu, huko Hai Mkoani Kilimanjaro chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko amesema kuwa mwili huo ulichukuliwa kimakosa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Machame na kwenda kuzikwa sehemu ambayo haikuhitajika azikwe marehemu huyo.

  Alisema mwili huo ulichukuliwa na familia ya Nkya na kujua kuwa ni ndugu yao na kuacha mwili wa ndugu yao na kwenda kuuzika katika kijiji cha Nronga Machame huku wakijua ni ndugu yao husika.

  Kamanda huyo aliendelea kusema kuwa, familia ya Sembeta ilipofika hospitalini hapo na kutaka mwili wa ndugu yao ili waende kuzika walibaini mwili walioonyeshwa na msimamizi wa chumba hicho kuwa si wao.

  Ndipo walipotoa taarifa katika chumba hicho na mmoja wa wasimamizi katika chumba hicho cha maiti kukiri kuwa kuna watu walitangulia asubuhi walikuja kuchukua mwili na kusema huenda watakuwa wamebadilisha mwili.

  Wanandugu hao walipofuatilia walibaini kuwa mwili uliochukuliwa na kuzikwa ndio ulikuwa mwili wa ndugu yao.

  Ndipo walipopeleka taarifa hizo katika kituo cha polisi na polisi kutoa amri kuwa waufukue na kuuzika mwili huo mahali ambapo walipaandaa ili kumaliza utata huo.

  Hivyo wanandugu hao waliufukua mwili huo chini ya ulinzi mkali wa polisi wa Mkoa na kuuchukua kwa kuuzika upya mahali ambapo walipanga.

  Wale waliochukua mwili ule awali nao walilazimika kurudi tena hospitali kwa ajili ya kuchukua mwili wa ndugu yao na kwenda kuanza mazishi upya.
   
Loading...