Mwili wa Omar Bongo kuzikwa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwili wa Omar Bongo kuzikwa leo

Discussion in 'International Forum' started by Richard, Jun 16, 2009.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mwili wa alekuwa raisi wa Gabon Omar Bongo unatarajiwa kuzikwa asubuhi hii katika makazi ya raisi huyo mkongwe barani Afrika.

  Tayari wageni mbalimbali akiwemo raisi Sarkozy wa Ufaransa ambayo ni mkoloni wa zamani wa Gabon, raisi wa zamani wa Ufaransa wamekwishawasili mjini Libreville.

  Wageni wengine ni pamoja na raisi wa Senegal na waziri wa mambo ya nje wa Uganda.

  Makamu wa raisi Dr. Ali Shein anaiwakilisha Tanzania katika shughuli hio.

  Omar Bongo Odimba alitawala nchi hiyo ndogo lakini yenye utajiri mkubwa wa mafuta kwa miaka arobaini na moja. Alifariki katika zahanati moja nchini Spain kwa kile kinachosadikika kuwa ni ugonjwa wa kiharusi.

  Mwanae wa kiume aitwae Ben Ali Bongo ambae ni waziri wa ulinzi ndie anatarajiwa kushika wadhifa wa uraisi ulioachwa na mareehemu baba yake. Pia mtoto mwingine wa kike aitwae Juli kupitia mume wake ambae ni waziri wa fwedha nae anafikiriwa.

  Hali ni shwari katika jiji la Libreville na vitongoji vyake na wananchi wamekuwa wakitafakari hali ya baadae ya nchi yao ya Gabon baada ya kuondokewa na Omar Bongo.

  Pata habari zaidi kupitia link ifuatayo ambayo ni kwa lugha ya kifaransa:

  http://www.gabonews.ga/gestion_video/reportage_deces_omar_bongo_2009.php

  Kwa wale walio na uwezo wa kupata channel ya France News 24, inatangaza maziko hayo katika link ifuatayo:

  http://www.france24.com/en/
   
  Last edited: Jun 16, 2009
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sayonara and good riddance!!
   
Loading...