Mwili wa mke wa Balozi Daraja waagwa jijini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwili wa mke wa Balozi Daraja waagwa jijini Dar

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Mar 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Dr. Salim Ahmed Salim (kulia) akimfariji Balozi Andrew Daraja kufuatia kifo cha mkewe Anna Mbago Daraja, wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake Kimara Temboni, jijini Dar es Salaam.  Rais Jakaya Kikwete, jana aliwaongoza viongozi mbalimbali wa serikali, mabalozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa mke wa balozi Mstaafu, Andrew Daraja, kabla ya kusafirishwa kwenda Tanga kwa mazishi leo.
  Marehemu Anna Daraja (65) inadaiwa aliuawa kwa kuchomwa kisu na mhudumu wa shambani kwake, James Mabakuri (22) Jumapili iliyopita
  Miongoni mwa waliohudhuria shughuli ya kuuaga mwili ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Balozi Salim Ahmed Salim na mke wake Amne na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Paul Rupia.
  Wengine ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, mabalozi na mabalozi wastaafu. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Patrick Tsere.
  Rais Kikwete aliwasili nyumbani kwa Balozi Daraja saa 6:59 mchana akiongozana na mkewe, Salma kabla ya kuuaga mwili na baadaye ilifanyika ibada fupi ambayo iliongozwa na Padre Kiongozi wa kanisa la Anglikana la St. Albano, Aidan Mbulinyingi, akisaidiana na Padre John Solomon.
  Padre kiongozi Mbulinyingi, aliwakumbusha watu kufanya matendo yanayompendeza Mungu na kutubu dhambi zao mara kwa mara.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ah, pole ndugu, Mungu akupe faraja
   
Loading...