Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,772
- 2,887
Mwili wa aliyekuwa Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro Mary Sulley umezikwa
, Machi 22, 2025 katika makaburi ya familia yaliyopo kijiji cha Mangafi,Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.
Mary Sulley alifariki Dunia Machi 18,2025 katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo, muda mfupi baada ya kutoka kwenye chumba cha Upasuaji.
Ibada ya mazishi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ikiwemo CCM na CHADEMA, Serikali na taasisi mbalimbali.
Akizungumza katika ibada hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rombo Antony Tesha amesema Mary alikuwa kiongozi shupavu na amesaidia kukijenga chama cha mapinduzi katika Wilaya ya Rombo.
Amesema waliishi kama familia moja ya CCM na walisaidiana , kushauriana ,na kuekelezana mambo mbalimbali kwa maslahi ya wana Rombo na siyo kwa maslahi yao binafsi.
“Mpaka umauti unamkuta mimi kama Mwenyekiti na yeye akiwa katibu hatujawahi kununiana ,sifa moja aliyokuwa nayo alikuwa ni mkarimu , mpole na usikivu , hakika huyu Mary Sulley tunayemuaga leo alikuwa ni mtu wa ajabu” amesema Tesha.
Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Mashariki Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT, Mchungaji Calvin Koola akizungumza katika ibada hiyo ameitaka jamii hasa wanasiasa kupendana na kuacha kutendeana mabaya.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ,Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolfu Mkenda pamoja na Mbunge wa Jimbo la Karatu Daniel Awack wamesema wamepoteza mtu mahiri katika Taifa.
Soma: TANZIA - Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, Marry Sule, Afariki Dunia akipatiwa matibabu