Mwili kutoa harufu (body odor): Chanzo, jinsi ya kuzuia na matibabu yake

Nenda S.H AMON ama Maduka y a vipodozi ulizia deodorant ni maalumu kwa ajili ya VIKWAPA. Utasahau hiyo harufu.
 
sugulia limao kabla ya kuoga asubuhi acha kwa muda then oga endelea na shughuli zako nimeambiwa inasaidia pia
 
yaani hapa prince pepe amemamliza kila kitu. kunuka kwapa kunaendana na kua na jasho lenye harufu kali, au mkojo kutoa harufu kali. yote hii inatokana na kuzorota kwa mfumo wa taka mwili katika mwili wako. sasa kwasababu ya concentration ya hizo taka mwili ndo maana harufu inakuwa kali. ukitaka kuprove hii, angalia mkojo wako ni upi unakuwa na harufu zaidi, ule unaoelekea kwenye weupe au ule wa kahawia?! mkojo unavyozidi kuwa wa kahawia ndivyo unavyozidi kuwa na harufu.
so the same kwa jasho, unavyozidi kuwa na takamwili nyingi, concentration katika jasho inaongezeka na ndiyo na harufu inakuwa kali. asikwambie mtu!!! perfumes siyo dawa hata kidogo, dawa ni kubadili mfumo wa maisha yako, sasa zingatia mambo matatu yafuatayo
1. kunywa maji ya kutosha kwa siku, na usinywe maji mengi, zaidi ya nusu lita kwa mara moja!!!! hapana, kunywa walau glasi nane za maji sawa na lita mbili kwa siku, zigawe vizuri tu ili uhakikishe kuwa zinatimia kwa siku moja
2. fanya mazoezi ya kutosha yatakayo hakikisha unatoka jasho la kutosha ili taka mwili ziishe, kumbuka kwenye mfano wetu wa mkojo, kadri mkojo unavyokuwa clear ndivyo na harufu inavyopungua
3. angalia msosi unaotupia, vyakula vyenye asidi (uric acid) na jamii ya nyama husababisha taka mwili nyingi. ndo maana kwa mfano mkojo au jasho la mlevi linanuka vibaya sana. so kula matunda na mbogamboga za kutosha. hizi ni bora sana kuliko nyama na bia

after 3 to 5 dys lete majibu. trust me hii kitu ni nzuri na ya kweli, mi binafsi imenisaidia sana, na wengine nilowashauri wakazingatia imewafaa saana

akido
Nimekusoma shukrani mzee.
 
Mkuu Pelham 1 Angalia hii Tibu kikwapa chako kwa dawa hii

jinsi.jpg





Hakikisha unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira

ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapani hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku, unaweza kutumia sabuni au anti-bacterial na maji ya moto.

Safisha nguo katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na mafuta, vaa mashati safi. Inapendekeza kuvaa mavazi yenye

nyuzi za asili, kama vile pamba na hariri ili kusaidia kunyonya unyevunyevu na kuruhusu ngozi kupumua.

Wakati unafanya mazoezi, tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevunyevu kwapani ili kuzuia harufu mbaya.
Vinega ‘siki' na mafuta ya chai ' tea tree oil'

Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant. Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni anti-bacterial.
Limao

Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.
Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu. Tumia kisha unipe feedback.By MziziMkavu
 
Kinyesi kimejaza tumboni mkuu, huenda unapata choo baada ya muda, hali inayofanya uchafu uliooza kulundikana tumboni.

Kwanza shughulikia tumbo lako liachie uchafu angalau mara mbili kwa siku.
 
Kinyesi kimejaza tumboni mkuu, huenda unapata choo baada ya muda, hali inayofanya uchafu uliooza kulundikana tumboni.

Kwanza shughulikia tumbo lako liachie uchafu angalau mara mbili kwa siku.
........... mkuu baolojia ya wap hy ya kixaxa,ya kufikirika au utaniiiiiiii
 
Hakikisha pia unanyoa nywele zote vizuri ktk makwapa kupunguza uchafu wa jasho kulundikana katika makwapa ndugu.
 
Aloe Ever-Shield Deodorant

Ina Aloe vera ya asili inayoua vijidudu na inayoondoa harufu mbaya katika makwapa.
Haina chumvi chumvi za Aluminium wala anti-perspirant(haizibi vitundu vya ngozi).
Chumvi za Aluminium ni sumu na huaribu mfumo wa fahamu, huvuruga kiwango cha calcium
kwenye mwili na hivyo huathiri parathyroid gland. Parathyroid gland ikizidi husababisha maumivu,
magonjwa ya akili na constipation. Pia husababisha miwasho, majipu na vimbe.
Haina alcohol na haiharibu ngozi wala kuziba vitundu, pia haichomi na hutumuka hata baada ya
kunyoa nywele za makwapani.

FAIDA: Huondoa harufu mbayana hufanya ngozi iwe laini na inaweza kutumiwa kwa muda mrefu

Gharama yake ni sh 14000/- tu tuwasiliane kwa email healthwealthfirst@gmail.com kama utakuwa unaihitaji
 

Attachments

  • DEODORANT.bmp
    131.9 KB · Views: 84
Jaribu pia kutumia deodorant zinasaidia kupunguza hali hiyo

Study-Says-Deodorants-Do-Not-Cause-Breast-Cancer.png
 
Nina Rafiki Yangu Anasumbuliwa Sana Na Kikwapa. Muda Mwingi Mwili Wake Unatoa Harufu Mbaya Licha Kuoga Mara Kwamara. Afanyeje?
 
Mkuu.@mtwa mkulu Kama ni wewe au Rafiki yako ana matatizo ya kikwapa fuata

ushauri wangu huo hapo chini:


Hakikisha unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira


ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapani hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku, unaweza kutumia sabuni au anti-bacterial na maji ya moto.

Safisha nguo katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na mafuta, vaa

mashati safi. Inapendekeza kuvaa mavazi yenye


nyuzi za asili, kama vile pamba na hariri ili kusaidia kunyonya unyevunyevu na kuruhusu ngozi kupumua.

Wakati unafanya mazoezi, tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevunyevu

kwapani ili kuzuia harufu mbaya.


Vinega ‘siki' na mafuta ya chai ' tea tree oil'


Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant.

Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni

anti-bacterial.


Limao


Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa

lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.


Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu. Tumia kisha unipe feedback
 
Back
Top Bottom