Mwili kutoa harufu (body odor): Chanzo, jinsi ya kuzuia na matibabu yake

TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MWILINI

how-it-works-bad-breath-01-af.jpg



Harufu mbaya ni kitu kisichompendeza mtu yeyote. Unapotoa harufu mbaya toka mwilini mwako, haikupendezi wewe mwenyewe wala mtu wa jirani. Kama kitu hukipendi wewe na ukakiona hakifai basi usimlazimishe mwenzio akipende au akione cha kawaida.

Harufu mbaya mwilini inatoka maeneo yote ya mwili kuanzia kichwani hadi miguuni.

Zipo sababu nyingi zinazomfanya mtu atokwe na harufu mbaya, inaweza kuwa uchafu, maradhi au maumbile.


Hali ya uchafu ipo wazi endapo mtu haogi, hafui au hanawi. Uchafu wa kichwani inaweza kuwa nywele au wigi au

kitu chochote kinachowekwa kichwani.Uchafu unaweza kuwa maeneo mbalimbali ya mwili.

Maradhi ya ngozi, kansa au vidonda vyenye maambukizi vinaweza kusababisha kutoa harufu mbaya au vitambaa vilivyofungiwa vidonda.


Kwa hiyo kundi la maradhi ni pana kwa kuwa tatizo la ngozi pekee linaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa.

Sababu za kimaumbile linawahusu zaidi watu wanene ingawa hata wembamba pia wanaweza kupatwa na tatizo hili kutegemea na harufu inatoka eneo gani la mwili.


Watu wanene hupatwa na matatizo ya kutoa harufu mbaya kama hawatazidisha usafi na kuhakikisha miili yao sehemu za mikunjo inakuwa mikavu. Sehemu hizo ni chini ya kifua au matiti, nyama za tumboni, chini ya tumbo, mbavuni, sehemu za siri na mapajani.


Unene pamoja na matatizo mengi yanayoweza kujitokeza pia huweza kusababisha magonjwa ya ngozi na kutokwa na jasho lenye harufu kali.


MAENEO YANAYOTOA HARUFU MBAYA
Sehemu yoyote ya mwili inaweza kutoa harufu mbaya kama tulivyoona hapo mwanzoni kuanzia kichwani hadi miguuni. Lakini yapo maeneo kama masikioni na puani pia harufu mbaya hutoka. Harufu za maeneo hayo mara nyingi haziwi kali.

KUTOKWA HARUFU MBAYA KINYWANI

Tatizo la kutokwa na harufu mbaya mdomoni au kinywani hutokana na matatizo mbalimbali kama kuwa na meno mabovu, magonjwa ya fizi, ulimi, fangasi za kinywani na uchafu kutokana na kutosafisha kinywa vizuri.

Wapo watu ambao kwa asili hutoa harufu mbaya kinywani pasipo kuwa na magonjwa ya kinywa na huwa makini kusafisha kinywa, lakini harufu haiishi.

Tatizo hili hutibika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina katika tabaka linalotandika ndani ya kinywa.
Wakati mwingine harufu mbaya ya kinywa husababishwa na ulaji wa vyakula, unywaji pombe, uvutaji wa sigara, bangi na ugoro.


KUTOKWA NA HARUFU MBAYA KWAPANI

Kutokwa na harufu mbaya kwapani au kunuka kikwapa inatokana na mambo mbalimbali hata kama unajisafisha mara kwa mara na kutoa vinyweleo vya kwapani.


Harufu ya kikwapa husababishwa na njia ambazo ngozi ya kwapani hupumua zinaziba, hivyo kusababisha njia za kutolea jasho kuwa chache na jasho kutoka kidogo kidogo na kujaa kwapani.

Hivyo kujaa na kulowesha nguo sehemu hizo, hali hii ikiendelea kwa muda mrefu husababisha bakteria aina ya ‘staphylloccocus’ kuanza kuishi hapo na jasho linalojirundika kukauka na kuganda, hivyo kutoa harufu mbaya.


Tatizo la kikwapa likiendelea kwa muda mrefu baadhi ya njia za jasho huziba kabisa na bakteria kujipenyeza.

Hapo ndipo unaweza kusumbuliwa na majipu ya mara kwa mara kwapani, kutokwa na vipele vikubwa kwapani na muwasho mkali baada ya kunyoa kwapani na hata vidonda vidogovidogo.

Matumizi ya baadhi ya pafyumu husababisha mzio ambapo kwapa litawasha sana kila wakati au utatokwa na vipele vingi au ngozi ya kwapani inabadilika na kuwa nyeusi sana huku ikitoka harufu mbaya. Tatizo hili linaweza kutibika hospitali.


HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI
Harufu mbaya sehemu za siri inaweza kuwa kwa wanaume na wanawake. Zipo sababu mbalimbali kwa wanaume ambazo zinahitaji uchunguzi wa kina na tiba.


Kwa wanawake harufu inaweza kutoka ukeni ikiambatana na uchafu au la. Harufu ya ukeni huwa mbaya inayofanana na shombo la samaki hutokana na kutokuwa makini kiusafi.


Maambukizi ya fangasi na bakteria, magonjwa ya zinaa, kisonono na kaswende ni sababu mojawapo.
Wapo wanawake ambao hutokwa na harufu sehemu za siri kutokana na mikunjo ya kwenye mapaja yao, hasa kwa wale wanene. Harufu pia inaweza kutoka katika sehemu ya haja kubwa na hii ni ya kinyesi endapo hutanawa vizuri au kuwa na maradhi sehemu hiyo.


NINI CHA KUFANYA?

Endapo utakuwa na tatizo hili la kutoa harufu mbaya maeneo tofauti ya mwili au unahisi mwenzio ana tatizo hili na anakukwaza, inashauriwa uwaone madaktari katika hospitali za wilaya kwa uchunguzi wa kina.

Tatizo hili linatibika na hupotea kabisa na kukuacha huru. Tatizo la kutokwa na majipu, vipele, kubadilika rangi ya ngozi kwapani, chini ya matiti na sehemu za siri, pia linatibika kabisa endapo utawaona wataalamu. Wahi mapema hospitali.

USHAURI WANGU:

Zifuatazo ni njia mbadala unazoweza kufanya kuweza kukabili tatizo.

Tumia sabuni zilizo na uwezo wa kupambana na bakteria (Anti bacteria soap). Baadhi ya sabuni hizo ni Dettol, Family, Protex au Dove.

Hakikisha unavaa nguo zilizotengenezwa kwa malighafi za pamba kipindi cha joto kwani zinasaidia kunyonya jasho linalotoka mwilini.

Badala ya kutumia kiondoa harufu (Deodorant), unaweza kufuta sehemu za mwili wako zinazotoa jasho kama kwapani kwa kutumia ‘white vinegar’ au ‘ apple cider vinegar’.

Kama tatizo linasababishwa na dawa unazotumia mwone daktari wako akupe njia mbadala ya kukabili tatizo au akubadilishie dawa.

Unaweza kuweka maji ya nyanya katika maji yako ya kuoga, kama unatumia sinki unaweza kukaa ndani ya maji yao kwa takribani dakika 15.

Paka poda ya watoto kwa ajili ya kukausha jasho kwenye shemu zenye mkonjo na kuondoa harufu mbaya mwilini.
Usirudia kuvaa nguo nguo za ndani wakati wa joto.

Nywele za kwapa zinapokuwa nyingi husababisha tatizo hilo, hivyo basi hakiksha unazinyoa mara kwa mara .
Ikumbukwe pia harufu hii huweza kusababishwa na soski chafu, wale wanaovaa soksi kwa muda mrefu na kuloa miguu, harufu hiyo ina uwezo mkubwa wa kusambaa mwili mzima . Ili Kuepuka tatizo ni vizuri kama utavaa soksi safi na usirudie kuzivaa na usafishe miguu yako vizuri. Ukiwa na Swali au Tatizo lako lolote la Siri usikose kunitafuta kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano

siki+ya+Apple..jpg


Siki ya
apple cider vinegar

 
Wana-JF Doctor! Kuna ndugu yangu ana harufu kali mwilini hasa akitokwa na jasho.Hana sehemu yoyote inayouma mwilini.Anasema inamnyima sana uhuru.SWALI:Je hii inasababishwa na nini?Kama kuna anayejua naomba anijuze,
naomba kuwasilisha.
 
Tatizo la wa Afrika wengi uwa hawatumii deodorant suruhisho hapo kuoga na kupaka hiyo kitu kwa kwapa
 
Ajitahidi kunywa maji mengi na matunda,ajitahdi kuwa msafi wa mwili na mavazi angalau aoge mara 2 kwa siku na asiwe anarudia nguo yoyote aliyoivua bila kufuliwa tena,atumie deodorant ktk makwapwa yakiwa masafi na iwe ya kuanzia 10,000 kuendelea au kama amudu hiyo bei zipo hata za 2,000 na kama awezi pia atumie limao,ndimu ama makoko ya sufuria la ugali yaliyolowekwaa matumizi ya hivi ni ukimaliza kuoga wajikausha maji alafu unachukua kipande cha limao,ndimu unaguguliiiaaa kwapani na unaweza vaa nguo bila kusuuza ila makoko lzm usuuze. Ahakikishe kichaka kakifye na ajiwekee destr kila wiki aondoe vichaka. Naamini akizingatia hayo atafaulu kama sio 100% basi 90% akosi
 
Mi Nimemuelewa Anatatizo La Harufu Kali Ya Mwili
Mbona Mnampa Ushari Wa Harufu Ya Kwapa?
 
Wana-JF Doctor! Kuna ndugu yangu ana harufu kali mwilini hasa akitokwa na jasho.Hana sehemu yoyote inayouma mwilini.Anasema inamnyima sana uhuru.SWALI:Je hii inasababishwa na nini?Kama kuna anayejua naomba anijuze,
naomba kuwasilisha.

hiyo ni hila ya kwapa.........kunuka bila kuoza........mwambie atafute hii dawa.......nilipo mimi inauzwa elfu 40.......sasa nyie sijui mpo wapi........
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    396.8 KB · Views: 467
Habari wana JF

Kuna jamaa yangu yeye hata akioga baada ya robo saa mwili unaanza kutoa harufu.

Pia kwapa lake, anajitahidi kulinyoa lakini harufu ipo, pia ukikaa naye unasikia harufu nyingine toka katika mapaja hapo inapokaa dushe aliwahi kuugua fangas na akatibu hizo za uvungu wa mapaja, jamaa jasho ikitoka kidogo tu huwezi kaa naye kochi moja.

Msaidien shida nini? Tiba vipi?



 
Habari wana jf
kuna jamaa yangu yeye hata akioga baada ya robo saa mwili unaanza kutoa harufu. pia kwapa lake, anajitahidi kulinyoa lakini harufu ipo, pia uki kaa naye unasikia harufu nyingine toka ktk mapaja hapo inapo kaa dushe aliwahi kuugua fangas na akatibu hizo za uvungu wa mapaja, jamaa jasho ikitoka kidogo tu huwezi kaa naye kochi moja. msaidien shida nini? tiba vipi?

kamwone dr wa ngoz (dernatology)
 
Mh! hicho kimbembe, je yeye anajielewa kuwa ana hilo tatizo? Kuna watu wengine wana majasho mabaya sana. Nilisikia watu wanadai kuwa eti ukipaka ndimu kwenye makwaba kabla ya kuoga inaondoa hiyo harufu. Lakini ngoja waje wataalam hapa watakupa majibu yenye kujenga
 
Mh! hicho kimbembe, je yeye anajielewa kuwa ana hilo tatizo? Kuna watu wengine wana majasho mabaya sana. Nilisikia watu wanadai kuwa eti ukipaka ndimu kwenye makwaba kabla ya kuoga inaondoa hiyo harufu. Lakini ngoja waje wataalam hapa watakupa majibu yenye kujenga

Anajijua kwani hua anajihisi hata yeye, unakuta hakai katikati ya watu lazima aji isolate pembeni mnapokua wengi
 
Kama unasumbuliwa na tatizo lolote la muonekano, harufu, rangi nk kwenye ngozi na mwili wako kwa ujumla basi sasa ndo muda wako wa kuondokana nalo na kufurahi.
Karibu sana tukusaidie kuondoa matatizo ya Chunusi, Makunyanzi, Michirizi, Makovu ya Chunusi, Mwili kuwa na rangi tofauti tofauti, Madoa, Makovu,Vipele na kadhalika.

Utahudumiwa popote Tanzania. Elimu, Ushauri, Bidhaa nk hutolewa.

Karibu sana.

Mawasiliano :
S&E BEAUTY SOLUTIONS
P.O.Box 40848
Dar es salaam
Tupo Ilala Bungoni na Upanga - Charambe/Hindu Street; Jirani na International School of Tanganyika
Simu : 0 659 528 724
0 784 082 847
E-mail : tecetra@gmail.com
Pia unaweza kutembelea ukurasa wetu wa facebook - S&E BEAUTY SOLUTIONS
card-ya-turuhusu-tukupendezeshe-jpg.327082
 
Back
Top Bottom