Nimekuwa nikufuatilia mijadala/hoja mbalimbali ya/za Mwigulu; nimegundua kwamba jamaa yuko sahihi ila watu wengine ndo huwa hawamwelewi. Nitatoa mifano michache tu.
Namba moja:
Akichangia bungeni hoja ya Rais kuwa mdini, Mwigulu alisema "awamu ya kwanza Tanzania hakukuwa na udini, ikaja awamu ya pili pia hakukuwa na udini, imekuja awamu ya tatu pia hakuna udini, sasa tujiulize mwenye hii awamu ya nne udini nani kauleta?"
Alipofika hapo Tundu lissu alisimama kutaka kutoa hoja na Spika alipomzuia alipinga likazuka zogo then akatolewa nje, hoja ikaisha.
Hapa ni wazi Mwigulu alikuwa anakubaliana na hoja ya Rais kuwa mdini kwani watoa hoja walisema rais wa awamu ya nne ameleta udini.
Namba mbili:
Kwenye kikao cha bunge kilichopita, Mwigulu alikuwa analalamika "hivi mimi jamani nina mkosi kuwa mtanzania? yani kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni anamwomba kamishina wa bunge amtumie tiketi mbunge aliepo ziara ya kiserikali marekani, ili akatishe ziara na badala yake aende Dubai ili akaponde nae raha"
Hii inaonesha kabisa Mwigulu anaona nchi haiendi sawa.
My take: Chuki binafsi dhidi ya Mwigulu ndizo zinazofanya watu kuona kila anachoongea ni kibaya tu