Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba Vs Kiltila Mkumbo jimbo la Iramba Magharibi

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Jimbo la Iramba limekuwa na vita vikali kati ya Mwigulu Nchemba (Mbunge wa sasa aliyewahi kuwa Waziri pia) na Katibu Mkuu wa sasa Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo. Wasomi hawa wamekuwa na msigishano wa hapa na pale na kufanya Jimbo sasa kuangalia zadi watu waofaa badala ya kuangalia nini kinapaswa kufanyika kwenye Jimbo letu la Iramba.

Hivi karibuni kulitokea msiba wa mtu maarufu Dr. Mwigulu akiwa njiani kuelekea katika msiba huo baada ya kuambiwa kuwa Prof. kitila kishafika kule yeye akaghairi kwenda. Ajabu sana!

Sasa hawa watu wawili wameunda Timu zao za kutaka Jimbo na tayair wameshalalamikiana kufanyiana hujuma. Inashanagaza wanaangalia nafasi badala ya nini wanapaswa kukifanya kwa manufaa ya Jimbo.

Mwigulu ameunda timu abayo inaongozwa na Diwani wa kwenye Kata yake na yule Diwani wa Kinampanda. Mwigulu pia ametengeneza mtandao unaohusisha watu kama Richard Mkumbo - Mchumi mwenzie yupo Ofisi ya Makamu wa Rais, Kanali Mstaafu wa Jeshi Kitundu, Katibu Mkuu wa Wizara aliyejiudulu hivi karibuni yule Kingu. Mwigulu pia anaungwa mkono na Mbunge Viti maalum Martha Mlata na pia anafanya mawasiliano ya karibu na Mwanasheria Kitandu Ugula ambaye wapo naye Chamani na wanatoka Kata moja. Huyu anategemewa katika kuongoza mikakati ya kisheria katika kampeni zake.

Kundi la Prof. Kitila linaoenekana kujipanga zaidi kwani wale walioumizwa na Dr. Mwigulu wakati akigombea Mwaka 2015 wanaungana naye ili kuhakikisha wanamtoa kwenye ubunge. Kundi hili linajumuisha watu kama kina David Jairo (Katibu Mkuu wa zamani Madini na Nishati), Timothy Lyanga, Jumbe Katala, Jesca Kishoa (ambaye inadaiwa anasubiri Prof. Kitila alianzishe naye ahamaie CCM kumfuata muwe wake Kafulila). Kuna pia ambao wanaonekana kutokuwepo upande wowote, kwa mfano kuna Eng. William Shila ambaye anapanga mikakati mikali ya kuchukua Jimbo akifanya mawasiliano ya karibu na Diwani wa Ulemo nyumbani kwao Engineer huyu.

Kuna pia akina Juma Kilimba mwenyekiti wa CCM mkoa ambaye wanapambana kivyao na kuhakikisha wanachukua jimbo, Kilimba anadaiwa ana mtandao mkubwa Kitaifa.
Kundi la Prof. Kitila lina mikakati mizuri lkn limekuwa likikwama kidogo kupenya kwa WanaCCM kwa sababu ya Jimbo husika kuonekana lina UCCM mwingi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna background ya kutosha na mtoto gullo shumbi
Acha waumane hata hivyo wamemuhurumia wanyiramba ni miaka 5 mitano tu
Huyu Shumbi ashukiru na mwisho najua kalamu ya mwenyekiti inamuhusu
Hilo analijua fika
 
maendeleo
 

Attachments

  • IMG-20200425-WA0013.jpg
    IMG-20200425-WA0013.jpg
    40.7 KB · Views: 1
Kidugu
Member

Joined Apr 19, 2020
rep.png
7
point.png
45

==========

Hii ID nna mashaka itakua ya kitila mkumbo mwenyewe.

Kama sio kitila basi wewe mleta mada unatakiwa ujue kitu kimoja, huo muda unaotumia kutafutia wengine chakula ungeutumia kutafuta pesa kwa ajili ya bibi yako kule kijijini.

Maendeleo hayaletwi na mwanasiasa, maendeleo yako yataletwa na wewe mwenyewe.

Stop being a stupid person!!

KARIBU JF.
 
Kwakweli hakuna mgombea mwenyw nguvu iramba kama Prof,hali ya Mqigulu imekuwa tete mmno hasa baada yankuonekana dhahiri anautaka urais na kuvunja kanuni za ccm,Anashirikiana na familia mmoja kubwa na wafanyabiashara akiamini anaweza kuwa Raid jambo ambalo kamwe haliwezi kutokea
 
Kwakweli hakuna mgombea mwenyw nguvu iramba kama Prof,hali ya Mqigulu imekuwa tete mmno hasa baada yankuonekana dhahiri anautaka urais na kuvunja kanuni za ccm,Anashirikiana na familia mmoja kubwa na wafanyabiashara akiamini anaweza kuwa Raid jambo ambalo kamwe haliwezi kutokea
Kwani kitila mkumbo alikua hataki urais? akiwa ACT ni nani alikua mgombea mwenza?
 
Kidugu
Member

Joined Apr 19, 2020
rep.png
7
point.png
45

==========

Hii ID nna mashaka itakua ya kitila mkumbo mwenyewe.

Kama sio kitila basi wewe mleta mada unatakiwa ujue kitu kimoja, huo muda unaotumia kutafutia wengine chakula ungeutumia kutafuta pesa kwa ajili ya bibi yako kule kijijini.

Maendeleo hayaletwi na mwanasiasa, maendeleo yako yataletwa na wewe mwenyewe.

Stop being a stupid person!!

KARIBU JF.
Kanywe uji wa mihogo.umetumwa na Yule anayechoraga mawe mkoa wa singida.mwambie anitaka kuaibika achukue fomu ya ubunge kwenye hili jimbo.akachore mawe ndio kazi aliyoichagua
 
Back
Top Bottom