Mwigulu Nchemba: Ninayo VIDEO ya Viongozi CHADEMA wakipanga mikakati ya mauaji nchini...

Pamoja na kwamba ni kweli chadema kimejaa wahuni lakini tuhuma za mauaji kwao ni uongo.
Labda CCM ndio inapanga kuua. in fact, ina rekodi nzuri tu ya mauaji.

Naanza kuichikia sana serikali ya CCM, kwa kuwaacha huru watu wanaopanga mauaji,mtu anaukalia ushaidi wa kuhatarisha amani
 
kama ni kweli basi ntaichukia saaana ccm, hivi kweli kiongozi wa taifa anakaaje na video ya kesi ya mauaji ...kwa nini mpaka anaenda kwenye tv show hajaipeleka polisi ili hao cdm wahusika wapanga mauaji washughulikiwe ipasavyo??????

halafu anatangaza kwenye tv show kama vile ni video ya sinema ya holywood!

acheni kuweweseka subirini,time will tell...hakuna aliye juu ya sheria,wote watakaoonekana kwenye video hiyo ambayo inafanyiwa kazi na vyombo vya usalama wataburuzwa mahakamani soon,msianze kulalamika tena,ni mahakama hizi hizi zilizompa ushindi yule mwizi mstaafu wa magari wa arusha ndio zitatumika kuwashughulikia wauaji hao
 
Hiv tujiulize kwa jinsi ambavyo Nchemba haipendi CDM si angekua ameshaitoa hyo CD?.Kiongozi mkubwa kama huyo kutoa maneno hayo kwenye media n hatari sana,kwa nn asiupeleke huo ushahidi kwenye vyombo vya usalama?
 
Heri ya mwaka mpya JF,

Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu mkuu CCM Bara amedai kwamba anayo CD inayoonyesha CHADEMA ikipanga mauaji.

lakini makamanda mkumbuke kwamba katika mkutano mkuu wa nane wa CCM kule Dodoma waliandaa mikakati mingi, mkakati wa kwanza ni kuizushia CHADEMA tuhuma mbalimbali pamoja viongozi wake wakuu ili badala ya kuendelea na mkakati wa kuwaunganisha watanzania kwa kujua haki zao kwa ujumla somo la uraia basi wabaki kujibu propaganda za CCM.

Kwa mfano: Kadi ya Slaa, CHADEMA kimepuuzia ambapo hiyo propaganda ilitolewa na nape na wapenda mabadiliko wanasonga mbele, haya Mwigulu kaja na CD ya mauaji hapohapo kasahau wauaji polisi, bado Kinana atakuja na lake na Mangula naye atakuja na lake.

Lakini CCM watambue kwamba watanzania wa leo sio wa miaka ishirini iliyopita, watanzania wanataka kusikia elimu bora, afya bora, ajira kwa vijana, wasomi wasaminiwe. Angalia katika nchi ambayo afrika inaongoza kwa kuzalisha wajinga wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu yaani (KKK) ni TANZANIA.

Yeye Mwigulu na CCM yake anajisifia kujenga barabara ambako ni mkopa kutoka bank ya dunia, kwasasa serikali ya Tanzania inadiwa tirioni 20 nani atalipa hizo fedha kama sio walipa kodi, afya wakinamama wanajifugulia chini madawa mengi feki, shule hazina walimu wala madawati vitabu hakuna maabara kweli kuna elimu bora Tanzania?

Mtanzania, amka tetea kodi yako.
 
Heri ya mwaka mpya wote.
Leo asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI Naibu katibu mkuu ccm bara ndgu. Mwigulu Nchemba ametoa kauli nzito ya kwamba ANAYO NA ANAMILIKI CD YENYE VIDEO ya jinsi viongozi wa chadema walivyokaa na kupanga mikakati jinsi ya kutekeleza mauaji nchini.
Kama kiongozi kama huyu anajihakiki kuwa anao ushahidi mkubwa kiasi hicho, kwa nini sasa vyombo vya usalama vikae kimya kwa jambo kama hilo?
Kwa upande wa Viongozi wa CHADEMA ni wakati wenu sasa wa kuweka jambo hilo wazi na kulichukulia hatua stahiki.
Wito wangu kwa viongozi muwe makini na maneno yenu mnapokuwa kwenye media.


Mh. Mnyika na chama kwa ujumla tunakuomba shughulikia hili, tunaposema watu wanatishia usalama wa nchi ni kama hawa akina Mwigulu, kwani huyu anatofautiana nini na Ponda! ameongea kauli nzitonzito ambazo hakika zinahitaji kuzifanyia kazia, narudia na mimi amesema analiongea hili wazi kabisa kwamba ana cd inayoonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga na kutekeleza mauaji mkiliacha hili litaleta impact kubwa tena negatively.
 
Mbona unaweweseka na slaa kijana wametajwa viongozi wa chadema wewe moja kwa moja unakimbilia kwa slaa wako peke yake,kulikoni???na slaa angekua basha mi nasema vijana wengi sana humu angewaharibu!

Nape......Honey K.
 
vyombo vya usalama kazi yao ni nin? mpk sasa hawajachukua hatua yoyote juu ya kauli hyo?na kama uchunguzi unaendelea kwanin asiviachie vyombo vya usalama suala hili walikamilishe?
 
Ninao ushahidi. Sio wa madiwani ni viongozi wa kitaifa wa chadema. Nilishapeleka vyombo vya usalama. Wakimaliza kufanyia kazi nitaiweka video kwenye media

Mwigulu tunashukuru kwa kutokea hapa jamvini kwani huwezi weka hapa tukajionea
 
Hovi kweli mwigulu awe na cd then akae kimya kweli? Huyu jamaa ni wakuchunguza akili sio bure.
 
Heri ya mwaka mpya wote.
Leo asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI Naibu katibu mkuu ccm bara ndgu. Mwigulu Nchemba ametoa kauli nzito ya kwamba ANAYO NA ANAMILIKI CD YENYE VIDEO ya jinsi viongozi wa chadema walivyokaa na kupanga mikakati jinsi ya kutekeleza mauaji nchini.
Kama kiongozi kama huyu anajihakiki kuwa anao ushahidi mkubwa kiasi hicho, kwa nini sasa vyombo vya usalama vikae kimya kwa jambo kama hilo?
Kwa upande wa Viongozi wa CHADEMA ni wakati wenu sasa wa kuweka jambo hilo wazi na kulichukulia hatua stahiki.
Wito wangu kwa viongozi muwe makini na maneno yenu mnapokuwa kwenye media.
huyu jamaa ananipa mashaka kweli kama anapossess a genuine Bcom na MBA kutoka kwenye chuo kinachoheshimika ka UDSM. Hii ni kwa sababu akiwa na graduates (wanasiasa) wenzake kama akina Zitto, Myika, Mtatiro, January nk wanajaribu kujenga hoja lakini jamaa sijui ana matatizo gani!!!

Hapo kwenye red ujue amewahi kuja na hoja ya kutumiwa text na simu za vitisho kutoka namba alizozitaja lakini baada ya wadau kuleta hapa jamvini websites ambazo mtu yeyote anaweza kufanya lolote haijulikani hiyo kesi ilipoishia.

Cha ajabu zaidi inaonyesha ni jinsi gani ccm wana hali mbaya kiasi kwamba huyu mtu ndiye bora kati ya registered members 6,000,000 kuwa NAIBU KATIBU MKUU.
 
lema ,wenje,nyerere si walishatangaza kuanzisha M23 ya tanzania.... jamboo hilo liko wazi

Sasa kama ni kweli na jambo lipo wazi kwa nini wanaachwa wakiranda randa kitaani, kwa nini mpaka sasa hivi hawapo lupango....

yule mbunge wao wa arusha alisema maneno ambayo ni harmless kuliko haya ya tangazo la kuunda M23 na akavuliwa ubunge, i doubt kama hii ya tangazo la kuanzisha M23 ina ukweli....la sivyo wote wangekuwa jela by now

anyway mimi naona ingekua bora sana kama ccm wangeelekeza nguvu zao ku tekeleza miradi ya maendeleo ambayo waliahidi na wanaongelea kila siku kuliko kuongelea shutuma na mambo ambayo jeshi la polisi, mahakama na magereza wana jukumu na uwezo wa kushughulikia kikamilifu...
 
hahahaha angekuwa dk Slaa ndo kasema hayo saa nne tu tungeshasikia nchimbi kawatuma police wake waka muhoji ila kwa kuwa niii.........., imeonekana km rap tu
 
hapo ndio utajua udhaifu wa viongozi wa CCM
polisi ndio wanatakiwa kutuambia kuhusu huo ushahidi baada ya kumaliza upepelezi wao na kujiridhisha
na sio nchemba labda atuambie kama yeye ni msemaji wa polisi
hata hivo anajitapa na kuwapotezea watanzania muda wa kujadili hoja zenye msingi na sio huu uchafu
 
acheni kuweweseka subirini,time will tell...hakuna aliye juu ya sheria,wote watakaoonekana kwenye video hiyo ambayo inafanyiwa kazi na vyombo vya usalama wataburuzwa mahakamani soon,msianze kulalamika tena,ni mahakama hizi hizi zilizompa ushindi yule mwizi mstaafu wa magari wa arusha ndio zitatumika kuwashughulikia wauaji hao
Ningeshauri matumizi ya kiswahili kuzingatiwa, maana ya neno kuweweseka na context si sahihi nani anaweweseka hapa, maada inaongelea maelezo ya mwigulu kumiliki hiyo cd? but unatoa another serious allegation to mr. Lema
 
Back
Top Bottom