Mwigulu Nchemba ni kiboko ya chadema; afanya kufuru Songea.

kitambiheshima

JF-Expert Member
May 27, 2013
452
116
Jana Naibu katibu mkuu wa ccm Mwigulu Nchemba amekabidhi kadi za ccm kwa wanafunzi 200 wa vyuo vikuu Songea, amewapokea wanachama watatu walioihama chadema na kujiunga na ccm.
- Slaa ni mwongo kwa kusema kuwa bomba la gesi linajengwa kuelekea Ulaya.
- Chadema wanapewa fedha na wafadhili wasioitakia mema nchi hii. Amesema kama chadema imekosa fedha za kuitishia kikao cha halmashauri kuu, wamepata wapi fedha za kukodi chopper mil. 40 kwa siku?.
-Ameelezea sababu ya ccm na watanzania wengi kutaka muungano wa serikali mbili kuwa ndiyo muungano wenye maslahi ya taifa. Ametoboa ukweli wa msimamo wa vyama vya upinzani kutaka serikali tatu kuwa ni kutaka muungano uvunjike kwasababu ya uroho wa madaraka. Amesema, ukiondoa ccm, vyama vingine havina sura ya muungano hivyo vinataka muungano uvunjike vikidhani vitatawala kirahisi kwenye vipande vya muungano.
-Ameichana chadema live kuwa mtaji wa chama hicho ni matatizo ya watanzania. Amesema chadema hupenda kuona mambo yakienda mlama ili wapate ajenda ya kuzungumza. Alisema kuwa wamezoea kuwaandamanisha watanzania wakati watoto wao wanawaficha majumbani.

-Viongozi wa chadema wanahongwa majumba Ulaya na mabwana zao wa magharibi ili kuleta machafuko ndani ya nchi. Alisema kuwa tangu maandamano na mikutano ya chadema imeanza watanzania zaidi ya 10 wamepoteza maisha kwa kuwatoa sadaka na kusingizia jeshi la polisi.

- Alipongeza hekima na busara za Rais Kikwete kuwa pamoja na chokochoko za upinzani wanazotumwa na mabwana zao kuzifanya ili kuivuruga nchi, bado amewapiga bao. Ametolea mfano wa katiba mpya akisema anashindwa kuwaelewa wapinzani ambao waliahidi katiba mpya kwa muda wa siku mia na wengine wakasema tayari wanayo rasimu mfukoni, leo wanasema muda uliotengwa na serikali ni mdogo!.

-Alisema kuwa ccm imebaini janja ya upinzani na hasa chadema kuwa kelele zoooooote si chochote bali ni kutaka nchi ivurugike, uroho wa madaraka na rasilimali za nchi kwa kutumiwa na mabwana zao.

Alisema kuwa iwe muungano wa serikali moja, mbili, tatu ama nne, chadema ilishapigwa bao siku nyiiiiingi!
 
lamsingi kati ya hayo aliosema nilioona ni ilo la kuadamana alipohoji kuhusu watoto wao mengine yaleyale tuliyoyazoea kuyasikia kutoka kwake.
 
Kumbe gaidi bado halijaota akili mpya pamoja na kupewa Uwaziri wa Kimagumashi? Sasa, yeye kazi yake ni kusaidia kuwaletea Watanzania maisha bora na kuwatoa kutoka kwenye rindi la umasikini au kupambana na Chadema?
 
Unataka asiiseme chadema??

wakati chadema hao ndo waongo na ndo wanaoivuruga nchi,akili yako inahitaji uchunguzi wa kina kama unashindwa kung'amua vitu vidogo kama hivi.
 
Hawa ndio wanajiita wasomi nchini, labda mi sijaelewa vizuri hebu mnionyeshe wapi kaongelea matatizo ya wana songea au hata taifa, ina maana kwa sisi watu ambao hatuitaji sana mambo ya siasa ingebidi tuondoke kwenye huo mkutano
 
Hicho ni chama chakavu hata kama kikija na sera ya kugawa 1m kwa kila mtanzania kila siku.
Tunaitaji chama mbadala.
Kama hata Ikulu huwa inabajeti ya kununua fanicha kila mwaka, iweje ccm itunyonye miaka 100?!
Inamana wana hati miliki ya Tanzania?
 
Kusema kweli hotuba ya Nchemba iliwakuna wengi ambao walionekana kugutushwa na ukweli ambao walikuwa hawaujui. Kila alipokuwa akiumwaga ukweli huo, ilisikika sauti ya mshangao kutoka kwa watu..... alaaaa kumbe! Kiukweli wanasongea wameielewa chadema na malengo yake nyuma ya pazia.
 
Akili Ndogo huyu!
Maana kila kitu Chadema Chadema.

Hata umasikini Nchi hii umeletwa na Chadema.

.
Huyu jamaa mwigulu ana kiwango kikubwa cha ukichaa kichwani mwake.
Sijaweza hadi leo kumtofautisha na Savimbi ama osama toka aandae mipango ya kurusha bomu kwa wananchi wasio hatia kanisani Olisati na kwenye mkutano wa hadhara Arusha.
.
 
Hicho ni chama chakavu hata kama kikija na sera ya kugawa 1m kwa kila mtanzania kila siku.
Tunaitaji chama mbadala.
Kama hata Ikulu huwa inabajeti ya kununua fanicha kila mwaka, iweje ccm itunyonye miaka 100?!
Inamana wana hati miliki ya Tanzania?

Kwa bahati nzuri lengo hilo pia alilitolea ufafanuzi kama nilivyoeleza. Lengo la chadema linajulikana. Siyo kuwaletea watanzania maisha bora bali kutawala tu na kubadilisha tu utawala. Tubadilishe utawala inapolazimu na kisha tuwe na mipango. Siyo kukurupuka na kuwaza kuiondoa ccm madarakani wakati hujajipanga au una mipango isiyotekelezeka, utang'olewa madarakani hata kabla ya miezi sita.
 
Ukimwacha zitto kabwe hakuna kiongozi mwingine wa chadema ambaye anaweza kufika uwezo wa kiakili wa mwigulu hata mmoja hata robo ya akili tu.
 
Kama ni swala la uroho wa madaraka nani mwenye uroho aliyekaa miaka 50,bila kufanya cha maana katika elimu, maji, barabara na afya au ni yule ambaye yy hajawahi kushika madaraka ya nchi. Mie hapo nashindwa kujua jamaa hyu Nchemb akili iko au hakuna. Mnapo ng'ang'ania mshike madaraka tambua huo ndo uroho wa madaraka siyo anayetaka kuanza. Uroho ni pale unapokuwa hutaki kuachia kwa wengine ulicho nacho tayari.
Na kama watawala kweli mnajua Chedema ndo wameua watu kweny mikutano yao na hakuna hatua mliochukuwa then bila aibu unalalamika publically na ww. .. Ni kwamba mmepoteza ID ya kutawala. Shame on you.. yaani unajua wameua.. ebo.. then mmeogopa kuchukuwa hatua.. Matamshi mengine tuone aibu kusema mbele ya jamii. Au mbele za watu wanaofikiri.
 
Tumia akili vizuri chama hata kama kitakaa madarakani kwa miaka 100 kwa demokrasia hakuna shida lakini chadema ni ubabe hakuna uchaguzi.
 
.
Huyu jamaa mwigulu ana kiwango kikubwa cha ukichaa kichwani mwake.
Sijaweza hadi leo kumtofautisha na Savimbi ama osama toka aandae mipango ya kurusha bomu kwa wananchi wasio hatia kanisani Olisati na kwenye mkutano wa hadhara Arusha.
.
Nadhani umechanganyikiwa hujui kuwa waliorusha bomu ni wewe,lema na mbowe au unajifanya zimekuruka?
 
Back
Top Bottom